Skip to main content

Posts

WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2022 AWAMU YA PILI

  JESHI la Kujenga Taifa (JKT), tunatoa siku tatu kwa vijana walioitwa kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2022, ambao hawajaripoti mpaka sasa kuripoti makambi waliyopangiwa ya JKT mara moja. Pia tumetoa nyongeza ya majina ya vijana waliohitimu elimu ya kidato cha sita mwaka 2022 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2022. Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali, Hassan Mabena anatoa wito kwa vijana waliochaguliwa wa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria mwaka 2022 Awamu ya Pili ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi wiki ijayo na yataendeshwa kwa muda wa miezi mitatu.  Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele anawataka kuripoti makambini vijana wote walioitwa kuhudhuria Mafunzo ya JKT Kwa Mujibu wa Sheria kwa mwaka 2022, ambao hawajaripoti mpaka sasa mripoti makambi ya JKT mara moja. Vijana  waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti makambi ya JKT yaliyo karibu na maeneo wanayoishi. "Vijana wote waliochaguliwa  

SUMAJKT YAKABIDHIWA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA JAMII YA WAKAZI KUTOKA NGORO NGORO

Taasisi ya Hifadhi ya Ngorongoro ( Ngoro ngoro Conservation Area Authority ( NCAA)  imekabidhi Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga  Taifa ( SUMAJKT) Mradi wa Ujenzi wa nyumba 400 eneo la  Msomela mkoani Tanga kwa  ajili ya Makazi ya jamii ya kimasai kutoka  Ngorongoro mkoani Arusha. Akikabidhiwa Mradi huo tarehe 21 Juni 2022, Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT kanali Petro Ngata amesema kuwa, SUMAJKT ipo tayari kukamilisha kazi hiyo kwa wakati  na kwa ufanisi.                                       "Shirika hili limekuwa likipokea kazi mpya na zilizoshindwa na kampuni nyingine  na kuzikamilisha kwa weledi wa hali ya juu"alisema Kanali Ngata. Nae Mhandisi Joshua Mwankunda kutoka NCAA amesema tayari wamekwisha kamilisha mahitaji muhimu ya awali ikiwemo Michoro, Barabara, Shule, mipaka pamoja na njia za mawasiliano. Mhandisi Joshua ameeleza kuwa tathmini ya mradi huo inaonesha Utagharimu Fedha za Kitanzania Shilingi Bilioni Tisa(9). "Tunaimani kubwa na SUMAJKT kwa ute

KWA MAHITAJI YA OFISI ZA KISASA NA KUMBI KARIBU SUMAJKT HOUSE

SHIRIKA la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) linapangisha  jengo la kisasa ambalo  Limegharimu zaidi ya Bilioni mbili (2) katika kuhakikisha kuwa linafikia viwango vya kisasa. Jengo hilo la kitega uchumi lenye ghorofa tano katika jiji la Dodoma litachangia kasi ya ukuaji wa uchumi nchini. Jengo hilo lijulikanalo kama ‘SUMAJKT HOUSE ’ , lililopo  eneo la Ipagala Mashariki katika kiwanja namba 130 jijini Dodoma, barabara kuu kutoka jijini Dar es Salaam, lina baadhi ya ofisi zitazopangishwa kwa Taasisi mbalimbali ikiwemo Benki, Mashirika na watu binafsi kwa matumizi ya kiofisi. Ghorofa  ya chini na Mezza nine katika jengo hilo itakuwa maalumu kwa ajili ya kupangisha Benki mbalimbali zitakazokuwa na uhitaji, ambapo miundo mbinu yake imejengwa kwa kuzingatia  Ghorofa ya kwanza itatumiwa kwa ofisi za SUMAJKT .  Ghorofa ya pili na ya tatu itakuwa na ofisi zitakazopangwishwa kwa wahitaji. Aidha, ghorofa ya nne itatumika kwa ukumbi kwa matumizi mbalimbali kama mikutano, shereh

WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2022

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linawaita vijana waliohitimu elimu ya Sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2022 kutoka shule zote za Tanzania bara kuhudhuria Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria. Sanjari na wito huo, JKT limewapangia makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 03 hadi June 2022. Vijana walioitwa wamepangwa katika kambi za JKT Rwamkoma-Mara, JKT Msange-Tabora, JKT Ruvu-Pwani, JKT Mpwapwa na Makutupora JKT-Dodoma, JKT Mafinga-Iringa, JKT Mlale-Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba-Tanga, JKT Makuyuni-Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila -Kigoma, JKT Itaka-Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa -Rukwa, JKT Nachingwea-Lindi na JKT Kibiti-Pwani na Oljoro JKT-Arusha. Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (Physical disabilities) waripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo. JKT inawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo.     1. Bukta ya

“NAENDELEZA KAZI NINAZOZIJUA”- MEJA JENERALI MABELE

 Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT ) Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele tarehe 19/5/2022 ametimiza mwaka Mmoja madarakani huku akiendelea kutekeleza vema  azma ya Jeshi la Kujenga Taifa kujilisha pamoja na malezi ya vijana. Aidha tarehe 19 Mei 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alimteua kwa kipindi hicho akiwa  Brigedia Jenerali Rajabu Nduku Mabele kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afsa mtendaji mkuu wa SUMAJKT  Hatua iliyokuja kufuatia  aliyekuwa Mkuu wa Jeshi hilo, Meja Jenerali Charles Mbuge kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera akichukua nafasi ya Brig Jenerali Marco Elisha Gaguti aliyehamishiwa Mtwara. katika kipindi cha Mwaka mmoja akiwa madarakani Meja Jenerali Mabele ameendelea kutekeleza Majukumu yake kwa weledi ikiwa ni pamoja na kuliongoza vema Jeshi la Kujenga Taifa na Shirika lake la Uzalishaji Mali SUMAJKT. Shirika la Uzali

MWAKA MMOJA WA MKUU WA JKT NA AFISA MTENDAJI MKUU SUMAJKT KATIKA UONGOZI WAKE

KATIKA KUTIMIZA MWAKA MMOJA WA UONGOZI WA MKUU WA JKT NA AFISA MTENDAJI MKUU SUMAJKT HAYA NDIO YALIYOJIRI. SHIRIKA LA UZALISHAJI MALI LA JESHI   LA KUJENGA TAIFA (SUMAJKT) LINAENDELEA KUPIGA HATUA KATIKA SEKTA YA VIWANDA, SEKTA YA UJENZI, UHANDISI NA USHAURI, SEKTA YA HUDUMA NA BIASHARA, SEKTA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI. KATIKA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA WA UONGOZI WA MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA NA AFISA MTENDAJI MKUU WA SUMAJKT MEJA JENERALI RAJABU NDUKU MABELE SHIRIKA LIMEPATA MAFANIKIO MBALIMBALI . KWANZA KATIKA SEKTA YA VIWANDA. NOVEMBA 04, 2021 SHIRIKA LILIZINDUA KIWANDA CHA KUTENGENEZA TAA  SUMAJKT SKYZON COMPANY LIMITED SAMBAMBA NA UZINDUZI WA MAGARI NA ZANA NA KILIMO MLALAKUWA JIJINI DAR ES SALAAM. VILE VILE OCTOBA 29, 2021 MEJA JENERALI MABELE ALIZINDUA KIWANDA CHA UTENGENEZAJI MABATI SUMAJKT ROOFING COMPANY LIMITED AMBACHO HIVI SASA TAYARI KIMESIMIKWA MITAMBO JIJINI DODOMA. AIDHA SHIRIKA LIMEPIGA HATUA KATIKA SEKTA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI. PIA KUSIMIKWA MITAMBO YA KUTENGENEZA

KAMPUNI YA USAFI SUMAJKT CLEANING AND FUMIGATION YAPONGEZWA

Video hiyo ni Meneja wa kituo cha mabasi cha Mbezi Luis Bwana Mayira Mkama akipongeza Kampuni ya Usafi SUMAJKT Cleaning and Fumigation kwa huduma nzuri wanayotoa.  Katika mahojiano na SUMAJKT TV tarehe 09 April 2022 Meneja Mayira alisema  kuwa SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co. Limited wanatoa huduma nzuri kituoni hapo kutokana na kuwa na Watendaji wa kutosha pamoja na vitendea kazi vya kutosha tofauti na makampuni mengine ambapo mwanzoni huleta wafanyakazi wengi na baadae hupungua na eneo la kufanya usafi ni kubwa. Aidha ameeleza kuwa Uongozi wa Mbezi Luis Bus Terminal umekuwa ukishirikiana na kampuni hiyo katika kuhakikisha jukumu hilo linatimizwa ipasavyo. Meneja Mayira amezisihi kampuni zingine za usafi kuiga mfano kwa SUMAJKT. SUMAJKT Cleaning and Fumigation Company Limited ni kampuni tanzu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) iliyojizatiti katika utoaji wa huduma ya usafi na unyunyiziaji dawa.  Kampuni imejizatiti katika utoaji wa huduma za usafi kat

HII NDIO SIRI YA MAFANIKIO YA KIWANDA CHA USHONAJI NGUO SUMAJKT GARMENTS COMPANY LIMITED

Katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali kupitia mageuzi ya viwanda Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) halikubaki nyuma katika sekta ya viwanda. Miongoni mwa viwanda vilivyoanzishwa mwaka 2017 SUMAJKT Garments ni kiwanda kimojawapo ambacho kinafanya vizuri katika soko la ushindani na kimekuwa kimbilio la jamii kutokana na umahiri katika kazi ya ushoni. SUMAJKT Garments Company Limited inafanya vizuri katika shughuli za ushonaji nguo na Kupitia Video hiyo utapata kujua shughuli zote za ushonaji nguo sambamba na kudarizi  vinavyofanyika  kiwandani hapo.  Mnamo tarehe 2/02/2022 Kamera za SUMAJKT TV zilifika kiwandani hapo kufuatilia mchakato mzima wa ushonaji nguo na kupitia video hiyo hayo ndio yaliyojiri. Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Sylvester Ntandu pamoja na Maafisa wasaidizi wake wanakuelezea utendaji kazi wa kiwanda hicho. SUMAJKT Garments Company Limited kinashona mavazi ya aina mbali mbali zikiwemo nguo za watu binafsi, sare z

MKUU WA JKT NA AFISA MTENDAJI MKUU WA SUMAJKT MEJA JENERALI RAJAB NDUKU MABELE AMPONGEZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMIRI JESHI MKUU MHE. SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUTIMIZA MWAKA MMOJA MADARAKANI

 SUMAJKT NI KITUO CHA BIDHAA NA HUDUMA BORA “Kazi iendelee” ni Kauli mbiu ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan alianza nayo tangu aapishwe kushika madaraka hayo ambayo kwasasa ametimiza mwaka mmoja. Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) halikubaki nyuma katika kuunga mkono kauli mbiu hiyo kwa vitendo, limekuwa sambamba na Serikali ya awamu ya sita kuhakikisha kazi zinaendelea kwa manufaa ya Shirika, JKT na Taifa kwa Ujumla. Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele ametoa pongezi zake za dhati kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kutimiza mwaka mmoja wa uongozi, Aidha amemshukuru kwa kuendelea kuliamini SUMAJKT na kulipatia kazi mbalimbali, kupitia kampuni ya ujenzi (SUMAJKT Construction Company Ltd) ikiwemo Mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dodoma, Mradi wa ujenzi wa ofisi za mtandao wa Ser

KAMANDA JKT ZAMBIA ATEMBELEA VIWANDA SUMAJKT

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Tanzania Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele apongezwa na Mkuu wa JKT Zambia kwa kupiga hatua katika kusimamia  uzalishajimali . Kamanda wa Jeshi la Kujenga Taifa Zambia Luteni Jenerali Maliti Solochi tarehe 15 Machi 2022 ametembelea Kiwanda cha maji SUMAJKT Bottling Company pamoja na kiwanda cha ushonaji nguo SUMAJKT Garments Company katika eneo la Mgulani JKT Dar es Salaam kuona uzalishajimali na ametoa pongezi kwa namna Shirika linavyoendeshwa na kupiga hatua chini ya Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajab Nduku Mabele. Jenerali Solochi amesema kuwa JKT Zambia limekopi kila kitu kutoka JKT Tanzania ikiwemo uanzishaji wa viwanda na kwasasa jeshi lao lina baadhi ya viwanda ikiwemo kiwanda cha maji na kiwanda cha viatu. Jenerali Solochi ameongeza kuwa mahusiano haya ya kindugu kati ya JKT Tanzania na JKT Zambia yalianzishwa na Viongozi waasisi wake ambao ni baba wa taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Keneth Kau

UJUE MRADI WA UFUGAJI SAMAKI KWA KUTUMIA MATENKI- SUMAPONICS

 Katika video ni  mradi wa ufugaji wa samaki sato  unaojulikana kwa jina la SUMAPONICS uliopo  Mbweni JKT Dar es Salaam Tanzania.  Huu ni mradi mmojawapo kati ya miradi mingi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT). SUMAJKT Tv imetembelea mradi huo 11 March 2022 na kupata kuzungumza na Mkurugenzi Mwendeshaji wa mradi huo , na wengine kama inavyoonekana hapo. UFUGAJI SAMAKI WA MATENKI KWA KUZUNGUSHA MAJI (RE – CIRCULATION  AQUACULTURE SYSTEM – RAS) MBWENI JKT Ufugaji wa samaki kwa njia za mabwawa unahitaji rasilimali nyingi hasa ardhi, maji mengi na nguvu kazi kubwa ili kupelekea njia ya ufugaji samaki kwa matenki kwa kuzungusha maji (Recirculating Aquaculture System- RAS). RAS NI NINI? RAS ni mfumo wa kufuga samaki kwa kuzungusha maji ili kutoa uchafu pamoja na kuwaongezea hewa ya ziada samaki waliopo kwenye matenki. RAS ZA SUMAJKT Hizi ni RAS zinazotengenezwa katika mradi wa SUMAPONICS ambazo zina uwezo wa kutoa samaki wenye uzito wa gramu 250 – 350 kwa muda

MJIEPUSHE NA MAKUNDI YASIYOFAA-MEJA MWAKALEBE

  Kaimu Kamanda Kikosi Mgulani JKT Meja Heri Mwakalebe amewahasa wanafunzi wa kidato cha kwanza na waliohamia shule hiyo kuepusha na makundi yasiyofaa ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao. Meja Mwakalebe ameyasema hayo leo tarehe 4 Machi 2022, akiwa Mgeni Rasmi  katika ufungaji wa mafunzo ya ukakamavu na uzalendo kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza na wanafunzi waliohamia katika Shule ya Sekondari ya Jitegemee jijini Dar es Salaam. "Wanafunzi acheni kujihusisha na makundi yasiofaa ili kujiepusha kuingia katika vishawishi vya matumizi mabaya ya dawa za kulevya na tabia nyingine zisizofaa" alisema Meja Mwakalebe. Meja Mwakalebe amewataka wanafunzi hao kutumia muda wao kusoma ili kutimiza ndoto za maisha yao kwa kupata elimu bora ili kupambana na adui ujinga ambaye ni chanzo cha maradhi na umaskini. Vilevile, amewahimiza wanafunzi wa kike kujiepusha na vishawishi mbalimbali badala yake wajifunze kutoka kwa wanawake waliofanikiwa na kufanya vizuri kwa kuwa viongozi katika T

SUMAJKT YAKABIDHI HUNDI KUSAIDIA KUTANGAZA LUGHA YA KISWAHILI

Kaimu naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT), Kanali Shija Lupi amekabidhi hundi ya zaidi ya Milioni moja na laki nane (1,800,000/=) kwa Bwana Issack Kalumba ambaye anaendesha baiskeli katika nchi mbalimbali Barani Afrika kwa lengo la kuinua na kutangaza lugha ya kiswahili pamoja na utalii wa Tanzania kupitia majukwaa rasmi katika nchi hizo. Kanali Lupi alikabidhi hundi hiyo kwa Bwana Kalumba tarehe 04 March 2022 ofisini kwake Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa jijini Dar es salaam. SUMAJKT imetoa hundi ya kiasi hicho cha pesa kuunga mkono juhudi za Bwana Isaack Kalumba  ambaye alileta maombi SUMAJKT la kusaidiwa fedha hizo ili kuweza kutatua baadhi ya changamoto anazokutana nazo katika mzunguko wa Safari yake ya kuinua na kutangaza lugha ya kiswahili Barani Afrika. Bwana Isaack Kalumba ni Mtanzania anaeendesha baiskeli katika nchi mbalimbali Barani Afrika kwa lengo la kuinua na kuitangaza lugha ya kiswahili Afrika na kuunga mkono juhu

SUMAJKT GUARD LTD WAHITIMU MAFUNZO YA ISO

  Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Shija Lupi, amewataka wahitimu wa mafunzo ya uandaaji wa nyaraka kwa mujibu wa kiwango cha ubora (ISO 9001:2015) kufanya kazi kwa weledi na kuwa tayari kutoa elimu waliyoipata kwa wengine ambao hawakubahatika kuhudhuria mafunzo hayo.  Kanali Shija Lupi,  amezungumza hayo tarehe 11 Machi 2022 wakati  akifunga mafunzo ya ISO kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Petro Ngata, katika ukumbi wa mkutano Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa jijini Dar es Salaam. "Endeleeni kujifunza ili kuongeza tija ya Utendaji kazi ndani ya shirika la Uzalishaji Mali (SUMAJKT )".alisema Kanali Lupi Nae Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Ulinzi SUMAJKT Guard Ltd,  Kanali Joseph Masanja, amemshukuru Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, kwa kukubali kuendeshwa kwa mafunzo hayo.  Kanali Joseph Masanja, amefafanu

SUMAJKT YAKABIDHIWA MRADI WA UJENZI WA JENGO LA USAFISHAJI FIGO LUGALO

Kampuni ya ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited imekabidhiwa eneo  kwa ajili ya  Ujenzi wa Jengo la Usafishaji Figo, Ukumbi wa mkutano na Jengo la Uchunguzi wa magonjwa Lugalo  jijini Dar es Salaam.  Makabidhiano hayo yamefanyika  tarehe 11 machi 2022, ambapo maandalizi ya usafishaji wa eneo hilo la Ujenzi yameanza siku hiyo.  Eneo hilo litajengwa Ukumbi wa mkutano, Jengo la Uchunguzi wa magonjwa pamoja na Jengo dogo la  wagonjwa baada ya matibabu. Aidha lengo la mradi huo ni kuboresha huduma za Usafishaji Figo (Dialysis) na huduma nyingine zinazotolewa katika hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.  SUMAJKT kupitia Kampuni yake ya Ujenzi (SUMAJKT Construction Company Ltd) imeanza utekelezaji wa Ujenzi wa Miradi hiyo ambayo kukamilika ndani ya miezi sita. SUMAJKT kupitia Kampuni yake ya Ujenzi (SUMAJKT  Construction Company Ltd) imekuwa ikiaminiwa kwa kukabidhiwa miradi mbalimbali ya Ujenzi na Serikali pamoja na Taasisi binafsi kwa sababu ya kukamilisha Miradi hiyo k