Skip to main content

HII NDIO SIRI YA MAFANIKIO YA KIWANDA CHA USHONAJI NGUO SUMAJKT GARMENTS COMPANY LIMITED




Katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali kupitia mageuzi ya viwanda Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) halikubaki nyuma katika sekta ya viwanda.

Miongoni mwa viwanda vilivyoanzishwa mwaka 2017 SUMAJKT Garments ni kiwanda kimojawapo ambacho kinafanya vizuri katika soko la ushindani na kimekuwa kimbilio la jamii kutokana na umahiri katika kazi ya ushoni.

SUMAJKT Garments Company Limited inafanya vizuri katika shughuli za ushonaji nguo na Kupitia Video hiyo utapata kujua shughuli zote za ushonaji nguo sambamba na kudarizi  vinavyofanyika  kiwandani hapo. 

Mnamo tarehe 2/02/2022 Kamera za SUMAJKT TV zilifika kiwandani hapo kufuatilia mchakato mzima wa ushonaji nguo na kupitia video hiyo hayo ndio yaliyojiri.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Sylvester Ntandu pamoja na Maafisa wasaidizi wake wanakuelezea utendaji kazi wa kiwanda hicho.

SUMAJKT Garments Company Limited kinashona mavazi ya aina mbali mbali zikiwemo nguo za watu binafsi, sare za vyombo vya ulinzi na usalama, sare za shule, sare za makampuni na taasisi mbali mbali. 

Pia kiwanda kinadarizi nembo za aina mbali mbali pamoja na kuchapa nguo.

Aidha, Kiwanda hicho kimekuwa kikiunga mkono juhudi za serikali kwa kutoa ajira kwa vijana sambamba na fursa ya kujifunza kwa vitendo bure .
 
Kiwanda kipo Mgulani JKT Dar es Salaam, kwa mawasiliano zaidi piga 
Simu namba +255 718 488 234 au 
Barua Pepe: info@sumajkt.go.tz





















Comments

Popular posts from this blog

UJUE MRADI WA UFUGAJI SAMAKI KWA KUTUMIA MATENKI- SUMAPONICS

 Katika video ni  mradi wa ufugaji wa samaki sato  unaojulikana kwa jina la SUMAPONICS uliopo  Mbweni JKT Dar es Salaam Tanzania.  Huu ni mradi mmojawapo kati ya miradi mingi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT). SUMAJKT Tv imetembelea mradi huo 11 March 2022 na kupata kuzungumza na Mkurugenzi Mwendeshaji wa mradi huo , na wengine kama inavyoonekana hapo. UFUGAJI SAMAKI WA MATENKI KWA KUZUNGUSHA MAJI (RE – CIRCULATION  AQUACULTURE SYSTEM – RAS) MBWENI JKT Ufugaji wa samaki kwa njia za mabwawa unahitaji rasilimali nyingi hasa ardhi, maji mengi na nguvu kazi kubwa ili kupelekea njia ya ufugaji samaki kwa matenki kwa kuzungusha maji (Recirculating Aquaculture System- RAS). RAS NI NINI? RAS ni mfumo wa kufuga samaki kwa kuzungusha maji ili kutoa uchafu pamoja na kuwaongezea hewa ya ziada samaki waliopo kwenye matenki. RAS ZA SUMAJKT Hizi ni RAS zinazotengenezwa katika mradi wa SUMAPONICS ambazo zina uwezo wa kutoa samaki wenye uzito...

KAMPUNI YA USAFI SUMAJKT CLEANING AND FUMIGATION YAPONGEZWA

Video hiyo ni Meneja wa kituo cha mabasi cha Mbezi Luis Bwana Mayira Mkama akipongeza Kampuni ya Usafi SUMAJKT Cleaning and Fumigation kwa huduma nzuri wanayotoa.  Katika mahojiano na SUMAJKT TV tarehe 09 April 2022 Meneja Mayira alisema  kuwa SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co. Limited wanatoa huduma nzuri kituoni hapo kutokana na kuwa na Watendaji wa kutosha pamoja na vitendea kazi vya kutosha tofauti na makampuni mengine ambapo mwanzoni huleta wafanyakazi wengi na baadae hupungua na eneo la kufanya usafi ni kubwa. Aidha ameeleza kuwa Uongozi wa Mbezi Luis Bus Terminal umekuwa ukishirikiana na kampuni hiyo katika kuhakikisha jukumu hilo linatimizwa ipasavyo. Meneja Mayira amezisihi kampuni zingine za usafi kuiga mfano kwa SUMAJKT. SUMAJKT Cleaning and Fumigation Company Limited ni kampuni tanzu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) iliyojizatiti katika utoaji wa huduma ya usafi na unyunyiziaji dawa.  Kampuni imejizatiti katika utoaji wa hudum...

MWAKA MMOJA WA MKUU WA JKT NA AFISA MTENDAJI MKUU SUMAJKT KATIKA UONGOZI WAKE

KATIKA KUTIMIZA MWAKA MMOJA WA UONGOZI WA MKUU WA JKT NA AFISA MTENDAJI MKUU SUMAJKT HAYA NDIO YALIYOJIRI. SHIRIKA LA UZALISHAJI MALI LA JESHI   LA KUJENGA TAIFA (SUMAJKT) LINAENDELEA KUPIGA HATUA KATIKA SEKTA YA VIWANDA, SEKTA YA UJENZI, UHANDISI NA USHAURI, SEKTA YA HUDUMA NA BIASHARA, SEKTA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI. KATIKA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA WA UONGOZI WA MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA NA AFISA MTENDAJI MKUU WA SUMAJKT MEJA JENERALI RAJABU NDUKU MABELE SHIRIKA LIMEPATA MAFANIKIO MBALIMBALI . KWANZA KATIKA SEKTA YA VIWANDA. NOVEMBA 04, 2021 SHIRIKA LILIZINDUA KIWANDA CHA KUTENGENEZA TAA  SUMAJKT SKYZON COMPANY LIMITED SAMBAMBA NA UZINDUZI WA MAGARI NA ZANA NA KILIMO MLALAKUWA JIJINI DAR ES SALAAM. VILE VILE OCTOBA 29, 2021 MEJA JENERALI MABELE ALIZINDUA KIWANDA CHA UTENGENEZAJI MABATI SUMAJKT ROOFING COMPANY LIMITED AMBACHO HIVI SASA TAYARI KIMESIMIKWA MITAMBO JIJINI DODOMA. AIDHA SHIRIKA LIMEPIGA HATUA KATIKA SEKTA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI. PIA KUSIMIKWA MITAMBO YA KU...