Skip to main content

UJUE MRADI WA UFUGAJI SAMAKI KWA KUTUMIA MATENKI- SUMAPONICS


 Katika video ni  mradi wa ufugaji wa samaki sato
 unaojulikana kwa jina la SUMAPONICS uliopo 
Mbweni JKT Dar es Salaam Tanzania. 
Huu ni mradi mmojawapo kati ya miradi mingi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT).


SUMAJKT Tv imetembelea mradi huo 11 March 2022 na kupata kuzungumza na Mkurugenzi Mwendeshaji wa mradi huo , na wengine kama inavyoonekana hapo.

UFUGAJI SAMAKI WA MATENKI KWA KUZUNGUSHA MAJI (RE – CIRCULATION 
AQUACULTURE SYSTEM – RAS) MBWENI JKT


Ufugaji wa samaki kwa njia za mabwawa unahitaji rasilimali nyingi hasa ardhi, maji mengi na nguvu kazi kubwa ili kupelekea njia ya ufugaji samaki kwa matenki kwa kuzungusha maji (Recirculating Aquaculture System- RAS).

RAS NI NINI?
RAS ni mfumo wa kufuga samaki kwa kuzungusha maji ili kutoa uchafu pamoja na kuwaongezea hewa ya ziada samaki waliopo kwenye matenki.

RAS ZA SUMAJKT
Hizi ni RAS zinazotengenezwa katika mradi wa SUMAPONICS ambazo zina uwezo wa kutoa samaki wenye uzito wa gramu 250 – 350 kwa muda wa miezi minne.
RAS hizi hupandwa mbegu za miezi miwili na mteja hufuga samaki kwa muda wa miezi minne.


AINA ZA RAS ZINAZOPATIKANA
1. RAS YA LITA 5000 (Family Package)
Hii ni Ras inayotengenezwa kwa mteja kwa ajili ya chakula nyumbani, huwa na tenki moja lenye ujazo walita 5000, na lina uwezo wa kubeba kg 125 yani idadi ya samaki 500 kwa wakati mmoja. Mfumo huu hupatikana kwa gharama za Tsh 5,500,000/= na huitaji eneo la ukubwa wa Sqm 12.

2. RAS YA LITA 10,000 (Standard Package)
Hii ni Ras inayotengenezwa kwa mteja kwa ajili ya chakula nyumbani na kwa biashara, huwa na tenki moja lenye ujazo wa lita 10,000 na matenki madogo ya mfumo wa kuchuja maji.

Ras hii ina uwezo wa kubeba kg 250 yani idadi ya samaki 1000 kwa wakati mmoja, mfumo huu hupatikana kwa gharama za Tsh 9,500,000/=

3. RAS YA LITA 30,000
Hii ni RAS inayotengenezwa kwa ajili ya ufugaji samaki wa kibiashara, mfumo huu una matenki mawili ya kufugiasamaki yenye ujazo wa lita 10,000 na lita 20,000. 
Mfumo huu unaruhusu kuvuna kg 600 kila baada ya miezi miwili, hii ni kutokana kwamba mfugaji atapanda vifaranga 2000 vya miezi miwili katika tenki la lita 10,000 na baada ya miezi miwili atahamisha kwenda kwenye tenki la lita 20,000 kisha baada ya miezi minne ataanza kuvuna kila baada ya miezi miwili. Bei ya mfumo huu ni Tsh 16,000,000/= ukubwa wa eneo ni Sqm 84.

GHARAMA ZA MIFUMO YOTE ZINAHUSISHA
Ujenzi kamili wa mfumo kasoro kufunika (Shades)
Mfumo wa kuzungusha maji
Chakula cha kuanzia (Kg 10)
Jedwali la chakula cha kulisha
Mzani mdogo wa kupimia samaki
Mafunzo ya ufugaji samaki pamoja na huduma za kitaalamu kila mwezi mpaka mteja atakapovuna kwa mara ya kwanza.
Mbegu ya awali ya vifaranga kulingana na mfumo uliochagua

FAIDA ZA RAS
Matumizi ya eneo dogo kulinganisha na mabwawa
Mavuno makubwa katika eneo dogo
NI rahisi kuhudumia 
Ni mfumo mzuri katika utunzaji wa mazingira
Gharama zake za ujenzi ni nafuu.

MRADI WA SUMAPONICS
Mradi huu wa ufugaji samaki na utengenezaji wa mifumo ya ufugaji samaki kwenye matenki yenye kuzungusha maji unapatikana  jijini Dar es Salaam eneo la MBWENI JKT.
Pamoja na hayo mradi wa SUMAPONICS unajihusisha na:-
Uuzaji wa vifaranga vilivyokuzwa
Mafunzo ya ufugaji samaki
Ujenzi wa mifumo mingine ya ufugaji samaki kama mabwawa na vizimba (Cage)
Uuzaji wa samaki wa kufuga

“UCHUMI WA VIWANDA KWA AJIRA NA BIASHARA ENDELEVU’’

Kwa mawasiliano zaidi: Tunapatikana kwa namba +255 767 188 066 au Email: sumaponics@sumajkt.go.tz
Pia Tovuti: www. sumajkt.go.tz 

Endelea kufuatilia SUMAJKTTanzania.blogspot.com  zijazo kwa miradi  mbali mbali ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT).
(NB: Bei tajwa zinaweza kubadilika kulingana na hali ya soko, uzalishaji n.k)
Karibuni

Comments

Popular posts from this blog

MWAKA MMOJA WA MKUU WA JKT NA AFISA MTENDAJI MKUU SUMAJKT KATIKA UONGOZI WAKE

KATIKA KUTIMIZA MWAKA MMOJA WA UONGOZI WA MKUU WA JKT NA AFISA MTENDAJI MKUU SUMAJKT HAYA NDIO YALIYOJIRI. SHIRIKA LA UZALISHAJI MALI LA JESHI   LA KUJENGA TAIFA (SUMAJKT) LINAENDELEA KUPIGA HATUA KATIKA SEKTA YA VIWANDA, SEKTA YA UJENZI, UHANDISI NA USHAURI, SEKTA YA HUDUMA NA BIASHARA, SEKTA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI. KATIKA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA WA UONGOZI WA MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA NA AFISA MTENDAJI MKUU WA SUMAJKT MEJA JENERALI RAJABU NDUKU MABELE SHIRIKA LIMEPATA MAFANIKIO MBALIMBALI . KWANZA KATIKA SEKTA YA VIWANDA. NOVEMBA 04, 2021 SHIRIKA LILIZINDUA KIWANDA CHA KUTENGENEZA TAA  SUMAJKT SKYZON COMPANY LIMITED SAMBAMBA NA UZINDUZI WA MAGARI NA ZANA NA KILIMO MLALAKUWA JIJINI DAR ES SALAAM. VILE VILE OCTOBA 29, 2021 MEJA JENERALI MABELE ALIZINDUA KIWANDA CHA UTENGENEZAJI MABATI SUMAJKT ROOFING COMPANY LIMITED AMBACHO HIVI SASA TAYARI KIMESIMIKWA MITAMBO JIJINI DODOMA. AIDHA SHIRIKA LIMEPIGA HATUA KATIKA SEKTA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI. PIA KUSIMIKWA MITAMBO YA KU...

KAMPUNI YA USAFI SUMAJKT CLEANING AND FUMIGATION YAPONGEZWA

Video hiyo ni Meneja wa kituo cha mabasi cha Mbezi Luis Bwana Mayira Mkama akipongeza Kampuni ya Usafi SUMAJKT Cleaning and Fumigation kwa huduma nzuri wanayotoa.  Katika mahojiano na SUMAJKT TV tarehe 09 April 2022 Meneja Mayira alisema  kuwa SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co. Limited wanatoa huduma nzuri kituoni hapo kutokana na kuwa na Watendaji wa kutosha pamoja na vitendea kazi vya kutosha tofauti na makampuni mengine ambapo mwanzoni huleta wafanyakazi wengi na baadae hupungua na eneo la kufanya usafi ni kubwa. Aidha ameeleza kuwa Uongozi wa Mbezi Luis Bus Terminal umekuwa ukishirikiana na kampuni hiyo katika kuhakikisha jukumu hilo linatimizwa ipasavyo. Meneja Mayira amezisihi kampuni zingine za usafi kuiga mfano kwa SUMAJKT. SUMAJKT Cleaning and Fumigation Company Limited ni kampuni tanzu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) iliyojizatiti katika utoaji wa huduma ya usafi na unyunyiziaji dawa.  Kampuni imejizatiti katika utoaji wa hudum...