Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT ) Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele tarehe 19/5/2022 ametimiza mwaka Mmoja madarakani huku akiendelea kutekeleza vema azma ya Jeshi la Kujenga Taifa kujilisha pamoja na malezi ya vijana. Aidha tarehe 19 Mei 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alimteua kwa kipindi hicho akiwa Brigedia Jenerali Rajabu Nduku Mabele kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afsa mtendaji mkuu wa SUMAJKT Hatua iliyokuja kufuatia aliyekuwa Mkuu wa Jeshi hilo, Meja Jenerali Charles Mbuge kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera akichukua nafasi ya Brig Jenerali Marco Elisha Gaguti aliyehamishiwa Mtwara. katika kipindi cha Mwaka mmoja akiwa madarakani Meja Jenerali Mabele ameendelea kutekeleza Majukumu yake kwa weledi ikiwa ni pamoja na kuliongoza vema Jeshi la Kujenga Taifa na Shirika lake la Uzalishaji Mali SUMAJKT. Shirika la Uzali