Skip to main content

Posts

Showing posts from May, 2022

WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2022

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linawaita vijana waliohitimu elimu ya Sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2022 kutoka shule zote za Tanzania bara kuhudhuria Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria. Sanjari na wito huo, JKT limewapangia makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 03 hadi June 2022. Vijana walioitwa wamepangwa katika kambi za JKT Rwamkoma-Mara, JKT Msange-Tabora, JKT Ruvu-Pwani, JKT Mpwapwa na Makutupora JKT-Dodoma, JKT Mafinga-Iringa, JKT Mlale-Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba-Tanga, JKT Makuyuni-Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila -Kigoma, JKT Itaka-Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa -Rukwa, JKT Nachingwea-Lindi na JKT Kibiti-Pwani na Oljoro JKT-Arusha. Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (Physical disabilities) waripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo. JKT inawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo.     1. Bukta ya

“NAENDELEZA KAZI NINAZOZIJUA”- MEJA JENERALI MABELE

 Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT ) Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele tarehe 19/5/2022 ametimiza mwaka Mmoja madarakani huku akiendelea kutekeleza vema  azma ya Jeshi la Kujenga Taifa kujilisha pamoja na malezi ya vijana. Aidha tarehe 19 Mei 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alimteua kwa kipindi hicho akiwa  Brigedia Jenerali Rajabu Nduku Mabele kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afsa mtendaji mkuu wa SUMAJKT  Hatua iliyokuja kufuatia  aliyekuwa Mkuu wa Jeshi hilo, Meja Jenerali Charles Mbuge kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera akichukua nafasi ya Brig Jenerali Marco Elisha Gaguti aliyehamishiwa Mtwara. katika kipindi cha Mwaka mmoja akiwa madarakani Meja Jenerali Mabele ameendelea kutekeleza Majukumu yake kwa weledi ikiwa ni pamoja na kuliongoza vema Jeshi la Kujenga Taifa na Shirika lake la Uzalishaji Mali SUMAJKT. Shirika la Uzali

MWAKA MMOJA WA MKUU WA JKT NA AFISA MTENDAJI MKUU SUMAJKT KATIKA UONGOZI WAKE

KATIKA KUTIMIZA MWAKA MMOJA WA UONGOZI WA MKUU WA JKT NA AFISA MTENDAJI MKUU SUMAJKT HAYA NDIO YALIYOJIRI. SHIRIKA LA UZALISHAJI MALI LA JESHI   LA KUJENGA TAIFA (SUMAJKT) LINAENDELEA KUPIGA HATUA KATIKA SEKTA YA VIWANDA, SEKTA YA UJENZI, UHANDISI NA USHAURI, SEKTA YA HUDUMA NA BIASHARA, SEKTA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI. KATIKA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA WA UONGOZI WA MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA NA AFISA MTENDAJI MKUU WA SUMAJKT MEJA JENERALI RAJABU NDUKU MABELE SHIRIKA LIMEPATA MAFANIKIO MBALIMBALI . KWANZA KATIKA SEKTA YA VIWANDA. NOVEMBA 04, 2021 SHIRIKA LILIZINDUA KIWANDA CHA KUTENGENEZA TAA  SUMAJKT SKYZON COMPANY LIMITED SAMBAMBA NA UZINDUZI WA MAGARI NA ZANA NA KILIMO MLALAKUWA JIJINI DAR ES SALAAM. VILE VILE OCTOBA 29, 2021 MEJA JENERALI MABELE ALIZINDUA KIWANDA CHA UTENGENEZAJI MABATI SUMAJKT ROOFING COMPANY LIMITED AMBACHO HIVI SASA TAYARI KIMESIMIKWA MITAMBO JIJINI DODOMA. AIDHA SHIRIKA LIMEPIGA HATUA KATIKA SEKTA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI. PIA KUSIMIKWA MITAMBO YA KUTENGENEZA