Skip to main content

“NAENDELEZA KAZI NINAZOZIJUA”- MEJA JENERALI MABELE



 Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT ) Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele tarehe 19/5/2022 ametimiza mwaka Mmoja madarakani huku akiendelea kutekeleza vema  azma ya Jeshi la Kujenga Taifa kujilisha pamoja na malezi ya vijana.

Aidha tarehe 19 Mei 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alimteua kwa kipindi hicho akiwa  Brigedia Jenerali Rajabu Nduku Mabele kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afsa mtendaji mkuu wa SUMAJKT  Hatua iliyokuja kufuatia  aliyekuwa Mkuu wa Jeshi hilo, Meja Jenerali Charles Mbuge kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera akichukua nafasi ya Brig Jenerali Marco Elisha Gaguti aliyehamishiwa Mtwara.

katika kipindi cha Mwaka mmoja akiwa madarakani Meja Jenerali Mabele ameendelea kutekeleza Majukumu yake kwa weledi ikiwa ni pamoja na kuliongoza vema Jeshi la Kujenga Taifa na Shirika lake la Uzalishaji Mali SUMAJKT.

Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi   la Kujenga Taifa(SUMAJKT) linaendelea kupiga hatua katika sekta ya viwanda, sekta ya ujenzi, uhandisi na ushauri, sekta ya huduma na biashara, sekta kilimo, mifugo na uvuvi.

katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele Shirika limepata mafanikio mbalimbali .

Tukianza na sekta ya viwanda, Novemba 04, 2021 Shirika lilizindua kiwanda cha kutengeneza taa  SUMAJKT Skyzon Company Limited sambamba na uzinduzi wa magari na zana na kilimo Mlalakuwa jijini Dar es salaam.

Vile vile octoba 29, 2021 Meja Jenerali Mabele alizindua kiwanda cha utengenezaji mabati SUMAJKT Roofing Company Limited ambacho hivi sasa tayari kimesimikwa mitambo jijini Dodoma.

Aidha Shirika limepiga hatua katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Pia kusimikwa mitambo ya kutengeneza viatu katika kampuni ya viatu SUMAJKT Leather Product Company Limited.

Ukamilishwaji wa jengo la biashara la SUMAJKT Tower jijini Dodoma.

Shirika linaendelea kukua kwa kasi na hayo  ni baadhi tu ya mafanikio . Kasi hii ya ukuaji wa Shirika la JKT ni faida kwa taifa na kwa vijana ambao ndio taifa la kesho na juhudi hizi zinastahili pongezi.

Meja Jenerali Mabele alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 25 Novemba 1993 na kutunukiwa Kamisheni kuwa Afisa tarehe 25 Machi 1995. Pamoja na taaluma nyingine za Kijeshi, Jenerali Mabele ana Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Biashara (Master of Business Administration), akijikita katika Usimamizi wa Mashirika yaani (Corporate Management).

Katika utumishi wake Meja Jenerali Mabele amewahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Afisa Usalama na Utambuzi katika Vikosi kadhaa, Afisa Mnadhimu Malipo na Afisa Malipo wa Kikosi Makao Makuu ya Jeshi, Mkurugenzi wa Fedha za Umma na Uhasibu (Director for Public Finance and Accounting) na baadae alihamishiwa Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT), nafasi aliyohudumu hadi kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa.

Hongera sana kwa kutimiza mwaka mmoja madarakani ambapo mafanikio hayo yaliyotajwa kwa uchache yamechangiwa na juhudi zako za kujituma, uchapakazi, matumizi mazuri ya fedha, weledi, usimamizi bora wa rasilimali watu chini yako tunajivunia mchango wako katika Jeshi la Kujenga Taifa. Asante 

Comments

Popular posts from this blog

SUMAJKT YAKABIDHI VIATU VYA SHULE JOZI 500

 Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kupitia Kampuni tanzu iitwayo SUMAJKT shoes and leather Products Co LTD. tarehe 04 Novemba 2022 limekabidhi viatu vya ngozi jozi 500 kwa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao yenye kauli mbiu “Samia nivike viatu”. Aidha, makabidhiano ya viatu hivyo yamefanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam. Akielezea historia ya kiwanda Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Mathias John amesema, Kiwanda cha  viatu na bidhaa za ngozi SUMAJKT Shoes and Leather Product Co. LTD Kilianzishwa Jul 2017 na majukumu yake yakiwa ni uzalishaji wa viatu na bidhaa mbalimbali za ngozi.  Aidha, toka kuanzishwa Kqa  kiwanda hicho kimeendelea kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa kununua vifaa na mashine za kisasa ili kuzalisha bidhaa zenye ubora.  Bidhaa zinazozalishwa ni viatu kwa ajili ya taasisi za ulinzi, viatu vya usalama (safety boots), viatu vya maofisini na viatu vya shule.  Uwezo wa kiwanda ni kuzalisha viatu jozi 500 kwa siku na Kup

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA MIRADI YA UJENZI KANDA YA ZIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata leo tarehe 28 Oktoba 22 amefanya ziara katika miradi ya ujenzi inayoendelea kujengwa kanda ya ziwa. Kanali Petro Ngata amekagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Ziwa ambayo ni mradi wa ujenzi wa jengo la uchunguzi (Dignostic Center) katika hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama , Mradi wa uondoaji wa kifusi eneo la hanga uwanja wa ndege wa Chato Mkoani Geita na Mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Msalala. Aidha, Kanali Ngata  amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuhusu ukamilishwaji wa  jengo la ofisi za Halmashauri. SUMAJKT imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali ya ujenzi nchini kupitia kampuni yake ya ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited ambayo ina kanda saba za ujenzi.

MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA ZIARA MAFINGA MKOANI IRINGA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amehitimisha Ziara yake kwa kutembelea Kikosi cha JKT Mafinga Mkoani Iringa ambapo SUMAJKT katika kikosi hicho imewekeza katika ufugaji wa mifugo mbali mbali ikiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe. Bonyeza video hiyo kuona yaliyojiri.