Skip to main content

WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2022 AWAMU YA PILI

 



JESHI la Kujenga Taifa (JKT), tunatoa siku tatu kwa vijana walioitwa kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2022, ambao hawajaripoti mpaka sasa kuripoti makambi waliyopangiwa ya JKT mara moja.


Pia tumetoa nyongeza ya majina ya vijana waliohitimu elimu ya kidato cha sita mwaka 2022 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2022.


Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali, Hassan Mabena anatoa wito kwa vijana waliochaguliwa wa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria mwaka 2022 Awamu ya Pili ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi wiki ijayo na yataendeshwa kwa muda wa miezi mitatu. 

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele anawataka kuripoti makambini vijana wote walioitwa kuhudhuria Mafunzo ya JKT Kwa Mujibu wa Sheria kwa mwaka 2022, ambao hawajaripoti mpaka sasa mripoti makambi ya JKT mara moja.

Vijana  waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti makambi ya JKT yaliyo karibu na maeneo wanayoishi.


"Vijana wote waliochaguliwa   waripoti makambi ya JKT yaliyo karibu na maeneo wanayoishi, isipokuwa Kambi ya Makutupora JKT iliyopo mkoani Dodoma, Chuo Cha Ungozi Cha Jeshi la Kutenga Taifa(CUJKT) iliyopo Kimbiji mkaoni Dar es Salaam na Ruvu JKT iliyopo Mlandizi mkoani Pwani, ambayo inapokea wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho yenye miundombinu ya kuwahudumia watu wa jamii hiyo,"Brigedia Jenerali Mabena.


Vijana wote wanatakiwa kuripoti makambi ya JKT kuanzia tarehe 23 hadi Juni 25 mwaka huu 2022.


Comments

Popular posts from this blog

SUMAJKT YAKABIDHI VIATU VYA SHULE JOZI 500

 Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kupitia Kampuni tanzu iitwayo SUMAJKT shoes and leather Products Co LTD. tarehe 04 Novemba 2022 limekabidhi viatu vya ngozi jozi 500 kwa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao yenye kauli mbiu “Samia nivike viatu”. Aidha, makabidhiano ya viatu hivyo yamefanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam. Akielezea historia ya kiwanda Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Mathias John amesema, Kiwanda cha  viatu na bidhaa za ngozi SUMAJKT Shoes and Leather Product Co. LTD Kilianzishwa Jul 2017 na majukumu yake yakiwa ni uzalishaji wa viatu na bidhaa mbalimbali za ngozi.  Aidha, toka kuanzishwa Kqa  kiwanda hicho kimeendelea kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa kununua vifaa na mashine za kisasa ili kuzalisha bidhaa zenye ubora.  Bidhaa zinazozalishwa ni viatu kwa ajili ya taasisi za ulinzi, viatu vya usalama (safety boots), viatu vya maofisini na viatu vya shule.  Uwezo wa kiwanda ni kuzalisha viatu jozi 500 kwa siku na Kup

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA MIRADI YA UJENZI KANDA YA ZIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata leo tarehe 28 Oktoba 22 amefanya ziara katika miradi ya ujenzi inayoendelea kujengwa kanda ya ziwa. Kanali Petro Ngata amekagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Ziwa ambayo ni mradi wa ujenzi wa jengo la uchunguzi (Dignostic Center) katika hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama , Mradi wa uondoaji wa kifusi eneo la hanga uwanja wa ndege wa Chato Mkoani Geita na Mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Msalala. Aidha, Kanali Ngata  amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuhusu ukamilishwaji wa  jengo la ofisi za Halmashauri. SUMAJKT imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali ya ujenzi nchini kupitia kampuni yake ya ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited ambayo ina kanda saba za ujenzi.

MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA ZIARA MAFINGA MKOANI IRINGA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amehitimisha Ziara yake kwa kutembelea Kikosi cha JKT Mafinga Mkoani Iringa ambapo SUMAJKT katika kikosi hicho imewekeza katika ufugaji wa mifugo mbali mbali ikiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe. Bonyeza video hiyo kuona yaliyojiri.