Skip to main content

SUMAJKT GUARD LTD WAHITIMU MAFUNZO YA ISO

 


Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Shija Lupi, amewataka wahitimu wa mafunzo ya uandaaji wa nyaraka kwa mujibu wa kiwango cha ubora (ISO 9001:2015) kufanya kazi kwa weledi na kuwa tayari kutoa elimu waliyoipata kwa wengine ambao hawakubahatika kuhudhuria mafunzo hayo. 

Kanali Shija Lupi,  amezungumza hayo tarehe 11 Machi 2022 wakati  akifunga mafunzo ya ISO kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Petro Ngata, katika ukumbi wa mkutano Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa jijini Dar es Salaam.

"Endeleeni kujifunza ili kuongeza tija ya Utendaji kazi ndani ya shirika la Uzalishaji Mali (SUMAJKT )".alisema Kanali Lupi

Nae Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Ulinzi SUMAJKT Guard Ltd,  Kanali Joseph Masanja, amemshukuru Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, kwa kukubali kuendeshwa kwa mafunzo hayo. 

Kanali Joseph Masanja, amefafanua kuwa mategemeo ya Kampuni kwa wahitimu hao ni kuwa watawakilisha vema elimu walioipata katika kuhakikisha Kampuni inafungua milango zaidi ya kibiashara, Kitaifa na Kimataifa kwa kutanguliza masilahi mapana ya Serikali, wateja na wadau wote wanaohusika na Kampuni.

Kwa upande wa Mkufunzi wa mafunzo hayo Mhandisi Steven Minja, ameeleza kuwa SUMAJKT Guard Ltd, itanufaika na mafunzo ya ubora kiuongozi kwani Kampuni itaongeza ushindani kitaifa na kimataifa.

Mafunzo hayo ya  Uandaaji wa nyaraka kwa mujibu wa kiwango cha ubora (ISO 9001:2015) yalizinduliwa rasmi tarehe 03 Februari 2022  ambapo yalihudhuriwa na Maafisa, Askari na watumishi wa Umma wanaofanyia kazi Kampuni ya SUMAJKT Guard Ltd na  kuhitimishwa rasmi jana tarehe 11 Machi 2022.

Comments

Popular posts from this blog

SUMAJKT YAKABIDHI VIATU VYA SHULE JOZI 500

 Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kupitia Kampuni tanzu iitwayo SUMAJKT shoes and leather Products Co LTD. tarehe 04 Novemba 2022 limekabidhi viatu vya ngozi jozi 500 kwa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao yenye kauli mbiu “Samia nivike viatu”. Aidha, makabidhiano ya viatu hivyo yamefanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam. Akielezea historia ya kiwanda Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Mathias John amesema, Kiwanda cha  viatu na bidhaa za ngozi SUMAJKT Shoes and Leather Product Co. LTD Kilianzishwa Jul 2017 na majukumu yake yakiwa ni uzalishaji wa viatu na bidhaa mbalimbali za ngozi.  Aidha, toka kuanzishwa Kqa  kiwanda hicho kimeendelea kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa kununua vifaa na mashine za kisasa ili kuzalisha bidhaa zenye ubora.  Bidhaa zinazozalishwa ni viatu kwa ajili ya taasisi za ulinzi, viatu vya usalama (safety boots), viatu vya maofisini na viatu vya shule.  Uwezo wa kiwanda ni kuzalisha viatu jozi 500 kwa siku na Kup

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA MIRADI YA UJENZI KANDA YA ZIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata leo tarehe 28 Oktoba 22 amefanya ziara katika miradi ya ujenzi inayoendelea kujengwa kanda ya ziwa. Kanali Petro Ngata amekagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Ziwa ambayo ni mradi wa ujenzi wa jengo la uchunguzi (Dignostic Center) katika hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama , Mradi wa uondoaji wa kifusi eneo la hanga uwanja wa ndege wa Chato Mkoani Geita na Mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Msalala. Aidha, Kanali Ngata  amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuhusu ukamilishwaji wa  jengo la ofisi za Halmashauri. SUMAJKT imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali ya ujenzi nchini kupitia kampuni yake ya ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited ambayo ina kanda saba za ujenzi.

MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA ZIARA MAFINGA MKOANI IRINGA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amehitimisha Ziara yake kwa kutembelea Kikosi cha JKT Mafinga Mkoani Iringa ambapo SUMAJKT katika kikosi hicho imewekeza katika ufugaji wa mifugo mbali mbali ikiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe. Bonyeza video hiyo kuona yaliyojiri.