Ujumbe wa Maafisa kutoka Chuo cha Ukamanda na Unadhimu nchini Zambia ukiongozwa na Brigedia Jenerali Humphery Nyone leo tarehe 03 Oktoba 2022 umetembelea Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Makao Makuu Mlalakuwa jijini Dar es salaam ili kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na SUMAJKT. Ujumbe huo idadi ya Maafisa 20 umepokelewa na Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Shija Lupi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Petro Elikana Ngata. Akizungumza mara baada ya kupokea Ugeni huo Kanali Shija Lupi amesema kuwa Zambia na Tanzania zimeendeleza Udugu katika Shughuli mbalimbali za Kibiashara. "nchi hizi mbili zimekua kiuchumi, mara baada ya kupata uhuru katika miaka ya 1960, na Zambia kwa mara kadhaa imekua ikiagiza bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania, ikiwemo vifaa vya ujenzi pamoja na mazao ya vyakula, lakini pia Zambia imekua mzalishaji mkubwa wa bidhaa za kilimo, kama mahindi, bidhaa za shaba na nyingine nyingi" Ai