Skip to main content

Posts

Showing posts with the label SUMAJKT Guard Company Ltd

SUMAJKT GUARD LTD WAHITIMU MAFUNZO YA ISO

  Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Shija Lupi, amewataka wahitimu wa mafunzo ya uandaaji wa nyaraka kwa mujibu wa kiwango cha ubora (ISO 9001:2015) kufanya kazi kwa weledi na kuwa tayari kutoa elimu waliyoipata kwa wengine ambao hawakubahatika kuhudhuria mafunzo hayo.  Kanali Shija Lupi,  amezungumza hayo tarehe 11 Machi 2022 wakati  akifunga mafunzo ya ISO kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Petro Ngata, katika ukumbi wa mkutano Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa jijini Dar es Salaam. "Endeleeni kujifunza ili kuongeza tija ya Utendaji kazi ndani ya shirika la Uzalishaji Mali (SUMAJKT )".alisema Kanali Lupi Nae Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Ulinzi SUMAJKT Guard Ltd,  Kanali Joseph Masanja, amemshukuru Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, kwa kukubali kuendeshwa kwa mafunzo hayo.  Kanali Joseph Masanja, amefafanu