Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2022

WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2022 AWAMU YA PILI

  JESHI la Kujenga Taifa (JKT), tunatoa siku tatu kwa vijana walioitwa kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2022, ambao hawajaripoti mpaka sasa kuripoti makambi waliyopangiwa ya JKT mara moja. Pia tumetoa nyongeza ya majina ya vijana waliohitimu elimu ya kidato cha sita mwaka 2022 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2022. Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali, Hassan Mabena anatoa wito kwa vijana waliochaguliwa wa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria mwaka 2022 Awamu ya Pili ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi wiki ijayo na yataendeshwa kwa muda wa miezi mitatu.  Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele anawataka kuripoti makambini vijana wote walioitwa kuhudhuria Mafunzo ya JKT Kwa Mujibu wa Sheria kwa mwaka 2022, ambao hawajaripoti mpaka sasa mripoti makambi ya JKT mara moja. Vijana  waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti makambi ya JKT yaliyo karibu na maeneo wanayoishi. "Vijana wote waliochaguliwa  

SUMAJKT YAKABIDHIWA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA JAMII YA WAKAZI KUTOKA NGORO NGORO

Taasisi ya Hifadhi ya Ngorongoro ( Ngoro ngoro Conservation Area Authority ( NCAA)  imekabidhi Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga  Taifa ( SUMAJKT) Mradi wa Ujenzi wa nyumba 400 eneo la  Msomela mkoani Tanga kwa  ajili ya Makazi ya jamii ya kimasai kutoka  Ngorongoro mkoani Arusha. Akikabidhiwa Mradi huo tarehe 21 Juni 2022, Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT kanali Petro Ngata amesema kuwa, SUMAJKT ipo tayari kukamilisha kazi hiyo kwa wakati  na kwa ufanisi.                                       "Shirika hili limekuwa likipokea kazi mpya na zilizoshindwa na kampuni nyingine  na kuzikamilisha kwa weledi wa hali ya juu"alisema Kanali Ngata. Nae Mhandisi Joshua Mwankunda kutoka NCAA amesema tayari wamekwisha kamilisha mahitaji muhimu ya awali ikiwemo Michoro, Barabara, Shule, mipaka pamoja na njia za mawasiliano. Mhandisi Joshua ameeleza kuwa tathmini ya mradi huo inaonesha Utagharimu Fedha za Kitanzania Shilingi Bilioni Tisa(9). "Tunaimani kubwa na SUMAJKT kwa ute

KWA MAHITAJI YA OFISI ZA KISASA NA KUMBI KARIBU SUMAJKT HOUSE

SHIRIKA la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) linapangisha  jengo la kisasa ambalo  Limegharimu zaidi ya Bilioni mbili (2) katika kuhakikisha kuwa linafikia viwango vya kisasa. Jengo hilo la kitega uchumi lenye ghorofa tano katika jiji la Dodoma litachangia kasi ya ukuaji wa uchumi nchini. Jengo hilo lijulikanalo kama ‘SUMAJKT HOUSE ’ , lililopo  eneo la Ipagala Mashariki katika kiwanja namba 130 jijini Dodoma, barabara kuu kutoka jijini Dar es Salaam, lina baadhi ya ofisi zitazopangishwa kwa Taasisi mbalimbali ikiwemo Benki, Mashirika na watu binafsi kwa matumizi ya kiofisi. Ghorofa  ya chini na Mezza nine katika jengo hilo itakuwa maalumu kwa ajili ya kupangisha Benki mbalimbali zitakazokuwa na uhitaji, ambapo miundo mbinu yake imejengwa kwa kuzingatia  Ghorofa ya kwanza itatumiwa kwa ofisi za SUMAJKT .  Ghorofa ya pili na ya tatu itakuwa na ofisi zitakazopangwishwa kwa wahitaji. Aidha, ghorofa ya nne itatumika kwa ukumbi kwa matumizi mbalimbali kama mikutano, shereh