Skip to main content

Posts

Showing posts from November, 2022

SUMAJKT YAKABIDHI VIATU VYA SHULE JOZI 500

 Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kupitia Kampuni tanzu iitwayo SUMAJKT shoes and leather Products Co LTD. tarehe 04 Novemba 2022 limekabidhi viatu vya ngozi jozi 500 kwa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao yenye kauli mbiu “Samia nivike viatu”. Aidha, makabidhiano ya viatu hivyo yamefanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam. Akielezea historia ya kiwanda Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Mathias John amesema, Kiwanda cha  viatu na bidhaa za ngozi SUMAJKT Shoes and Leather Product Co. LTD Kilianzishwa Jul 2017 na majukumu yake yakiwa ni uzalishaji wa viatu na bidhaa mbalimbali za ngozi.  Aidha, toka kuanzishwa Kqa  kiwanda hicho kimeendelea kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa kununua vifaa na mashine za kisasa ili kuzalisha bidhaa zenye ubora.  Bidhaa zinazozalishwa ni viatu kwa ajili ya taasisi za ulinzi, viatu vya usalama (safety boots), viatu vya maofisini na viatu vya shule.  Uwezo wa kiwanda ni kuzalisha viatu jozi 500 kwa siku na Kup

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA MIRADI YA UJENZI KANDA YA ZIWA

  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalisahaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, ametoa maagizo ya kukamilishwa kwa wakati miradi ya ujenzi inayojengwa na Mkandarasi SUMAJKT Construction Co. Ltd Kanda ya Ziwa.  Kanali Petro Ngata akiendelea na ziara katika miradi ya ujenzi kanda ya ziwa, ametembelea  Ujenzi wa majengo ya OPD, RCH, Pharmacy na Mortuary yaliyopo katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza.  Aidha Kanali Ngata ameagiza kasi ya ujenzi iongezwe na ifanyike kwa njia ya oparesheni ambapo majengo ya "Pharmacy" na "Mortuary" yawe yamekamilika ifikapo tarehe 30 Nov 22 na "OPD" na "RCH" yakamilike ifikapo tarehe 12 Dec 22.  Vile vile Kanali Ngata amepata wasaa wa kutembelea Jengo la Halmashauri ya Bunda na kuagiza Meneja Ujenzi Kanda ya Ziwa kumuandikia Mshauri wa Mradi changamoto zote zinazosababisha ucheleweshaji wa mradi huu unaotekelezwa kwa njia ya "Force Account" ili uweze kukamilika kwa w