Skip to main content

WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2022



Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linawaita vijana waliohitimu elimu ya Sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2022 kutoka shule zote za Tanzania bara kuhudhuria Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.

Sanjari na wito huo, JKT limewapangia makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 03 hadi June 2022.

Vijana walioitwa wamepangwa katika kambi za JKT Rwamkoma-Mara, JKT Msange-Tabora, JKT Ruvu-Pwani, JKT Mpwapwa na Makutupora JKT-Dodoma, JKT Mafinga-Iringa, JKT Mlale-Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba-Tanga, JKT Makuyuni-Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila -Kigoma, JKT Itaka-Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa -Rukwa, JKT Nachingwea-Lindi na JKT Kibiti-Pwani na Oljoro JKT-Arusha.


Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (Physical disabilities) waripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.


JKT inawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo.


    1. Bukta ya rangi ya ‘Dark     Blue’ yenye mpira kiunoni (lastic) iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.


2. T-shirt ya rangi ya kijani 

     (Green Vest)


3. Raba za michezo zenye    

rangi ya kijani au blue.


4. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.


5. Soksi ndefu za rangi nyeusi.


6. Nguo za kuzuia baridi    kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.


7. Track suit ya rangi ya kijani au blue.


8. Nyaraka zote zinazohitajika katika udahili wa kujiunga na elimu ya Juu, zikiwemo cheti cha kuzaliwa, vyeti vya kuhitimu kidato cha Nne n.k


Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.


Orodha kamili ya majina ya vijana walioitwa, Makambi ya JKT waliyopangiwa na maeneo yaliyopo pamoja na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz 


Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele anawakaribisha vijana wote walioitwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza Uzalendo, Umoja wa kitaifa, Stadi za kazi , Stadi za Maisha na Utayari wa Kulijenga na Kulitumikia Taifa.

Comments

Popular posts from this blog

SUMAJKT YAKABIDHI VIATU VYA SHULE JOZI 500

 Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kupitia Kampuni tanzu iitwayo SUMAJKT shoes and leather Products Co LTD. tarehe 04 Novemba 2022 limekabidhi viatu vya ngozi jozi 500 kwa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao yenye kauli mbiu “Samia nivike viatu”. Aidha, makabidhiano ya viatu hivyo yamefanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam. Akielezea historia ya kiwanda Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Mathias John amesema, Kiwanda cha  viatu na bidhaa za ngozi SUMAJKT Shoes and Leather Product Co. LTD Kilianzishwa Jul 2017 na majukumu yake yakiwa ni uzalishaji wa viatu na bidhaa mbalimbali za ngozi.  Aidha, toka kuanzishwa Kqa  kiwanda hicho kimeendelea kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa kununua vifaa na mashine za kisasa ili kuzalisha bidhaa zenye ubora.  Bidhaa zinazozalishwa ni viatu kwa ajili ya taasisi za ulinzi, viatu vya usalama (safety boots), viatu vya maofisini na viatu vya shule.  Uwezo wa kiwanda ni kuzalisha viatu jozi 500 kwa siku na Kup

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA MIRADI YA UJENZI KANDA YA ZIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata leo tarehe 28 Oktoba 22 amefanya ziara katika miradi ya ujenzi inayoendelea kujengwa kanda ya ziwa. Kanali Petro Ngata amekagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Ziwa ambayo ni mradi wa ujenzi wa jengo la uchunguzi (Dignostic Center) katika hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama , Mradi wa uondoaji wa kifusi eneo la hanga uwanja wa ndege wa Chato Mkoani Geita na Mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Msalala. Aidha, Kanali Ngata  amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuhusu ukamilishwaji wa  jengo la ofisi za Halmashauri. SUMAJKT imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali ya ujenzi nchini kupitia kampuni yake ya ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited ambayo ina kanda saba za ujenzi.

MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA ZIARA MAFINGA MKOANI IRINGA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amehitimisha Ziara yake kwa kutembelea Kikosi cha JKT Mafinga Mkoani Iringa ambapo SUMAJKT katika kikosi hicho imewekeza katika ufugaji wa mifugo mbali mbali ikiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe. Bonyeza video hiyo kuona yaliyojiri.