Skip to main content

SUMAJKT YAKABIDHIWA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA JAMII YA WAKAZI KUTOKA NGORO NGORO


Taasisi ya Hifadhi ya Ngorongoro ( Ngoro ngoro Conservation Area Authority ( NCAA)  imekabidhi Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga  Taifa ( SUMAJKT) Mradi wa Ujenzi wa nyumba 400 eneo la  Msomela mkoani Tanga kwa  ajili ya Makazi ya jamii ya kimasai kutoka  Ngorongoro mkoani Arusha.


Akikabidhiwa Mradi huo tarehe 21 Juni 2022, Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT kanali Petro Ngata amesema kuwa, SUMAJKT ipo tayari kukamilisha kazi hiyo kwa wakati  na kwa ufanisi.

                                    





 "Shirika hili limekuwa likipokea kazi mpya na zilizoshindwa na kampuni nyingine  na kuzikamilisha kwa weledi wa hali ya juu"alisema Kanali Ngata.


Nae Mhandisi Joshua Mwankunda kutoka NCAA amesema tayari wamekwisha kamilisha mahitaji muhimu ya awali ikiwemo Michoro, Barabara, Shule, mipaka pamoja na njia za mawasiliano.


Mhandisi Joshua ameeleza kuwa tathmini ya mradi huo inaonesha Utagharimu Fedha za Kitanzania Shilingi Bilioni Tisa(9).


"Tunaimani kubwa na SUMAJKT kwa utendaji wao watafanya kile kilichokusudiwa kwa umaridadi mkubwa".Alisema Mhandisi joshua.


Serikali imeihamisha jamii ya Kimasai iliyokuwa ikiishi Ngorongoro mkoani Arusha na kuihamishia eneo la Msomela Tanga ili kuachia eneo la Ngorongoro shughuli za hifadhi ya Taifa ziendelee .


Mradi wa Ujenzi wa nyumba 400 Kwa Makazi ya jamii ya Kimasai kutoka Ngorongoro unapangwa Kutekelezwa Kwa muda wa siku 90.

Comments

Popular posts from this blog

SUMAJKT YAKABIDHI VIATU VYA SHULE JOZI 500

 Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kupitia Kampuni tanzu iitwayo SUMAJKT shoes and leather Products Co LTD. tarehe 04 Novemba 2022 limekabidhi viatu vya ngozi jozi 500 kwa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao yenye kauli mbiu “Samia nivike viatu”. Aidha, makabidhiano ya viatu hivyo yamefanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam. Akielezea historia ya kiwanda Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Mathias John amesema, Kiwanda cha  viatu na bidhaa za ngozi SUMAJKT Shoes and Leather Product Co. LTD Kilianzishwa Jul 2017 na majukumu yake yakiwa ni uzalishaji wa viatu na bidhaa mbalimbali za ngozi.  Aidha, toka kuanzishwa Kqa  kiwanda hicho kimeendelea kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa kununua vifaa na mashine za kisasa ili kuzalisha bidhaa zenye ubora.  Bidhaa zinazozalishwa ni viatu kwa ajili ya taasisi za ulinzi, viatu vya usalama (safety boots), viatu vya maofisini na viatu vya shule.  Uwezo wa kiwanda ni kuzalisha viatu jozi 500 kwa siku na Kup

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA MIRADI YA UJENZI KANDA YA ZIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata leo tarehe 28 Oktoba 22 amefanya ziara katika miradi ya ujenzi inayoendelea kujengwa kanda ya ziwa. Kanali Petro Ngata amekagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Ziwa ambayo ni mradi wa ujenzi wa jengo la uchunguzi (Dignostic Center) katika hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama , Mradi wa uondoaji wa kifusi eneo la hanga uwanja wa ndege wa Chato Mkoani Geita na Mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Msalala. Aidha, Kanali Ngata  amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuhusu ukamilishwaji wa  jengo la ofisi za Halmashauri. SUMAJKT imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali ya ujenzi nchini kupitia kampuni yake ya ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited ambayo ina kanda saba za ujenzi.

MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA ZIARA MAFINGA MKOANI IRINGA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amehitimisha Ziara yake kwa kutembelea Kikosi cha JKT Mafinga Mkoani Iringa ambapo SUMAJKT katika kikosi hicho imewekeza katika ufugaji wa mifugo mbali mbali ikiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe. Bonyeza video hiyo kuona yaliyojiri.