Skip to main content

Posts

Showing posts with the label Jeshi la Kujenga Taifa

IJUE SIRI YA MAFANIKIO YA JKT KATIKA KILIMO

MKUU wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema pamoja na kuwa na mabadiliko ya tabia nchi lakini bado katika vipando vya Jeshi la kujenga taifa na mashamba yake kwa  na vikosi yameendelea kufanya vizuri na mazao yanastawi kwa jinsi ambavyo walikuwa wametalajia. Amesema kuwa wao walishaona changamoto hizo za mabadiliko  ya tabia nchi hivyo walishaanza kufanya mawasiliano na mamlaka ya hali ya hewa ambapo walikuwa wanapewa taarifa juu ya mabadiliko hayo hususani kwenye eneo la mvua kwamba msimu huo mvua zitawahi ama kuchelewa na kama zitawahi zitakuja kwa viwango vidogo. Amesema kuwa baada ya kupata taarifa hiyo wao kama Jeshi la kujenga taifa walikaa chinin nakuweza kujipanga na kuona aina ya mbegu ambazo zitaweza kuendana na hali ya hewa. Brigedia Mabena ameyasema hayo Agosti 7 kwenye maonyesho ya nanenane ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Mbeya wakati alipotembelea banda la JKT pamoja na mambo mengine amesema kuwa katika kikosi cha 847 KJ ni Milundikwa nakwamba pa