Skip to main content

Posts

UHURU PEAK PURE DRINKING WATER

 
Recent posts

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMEAGA KAYA ZINGINE 25 NGORO NGORO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameaga kaya zingine 25, zenye watu 105, na amesema mpaka kufikia tarehe 18/8/2022,  jumla ya kaya 1,002 zenye watu 5,382 zimejiandikisha kwa hiari kuhama katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro na kuelekea kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoa wa Tanga,  lililotengwa na serikali kwa ajili ya wakazi hao. Kati ya kaya hizo,  tayari kaya 624 zenye watu 3,323 zimehakikiwa na kufanyiwa uthamini na kati ya kaya hizo, kaya 106 zenye watu 536 zimeshahamia kijiji cha Msomera wilayani Handeni Mkoani Tanga. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hayo Agosti 19,2022 Mkoani Arusha sambamba na zoezi la kukabidhi hundi ya Malipo kwa wakazi wapya wa Msomera. Hafla fupi ilifanyika kwenye ofisi za mamlaka ya hifadhi  hiyo kwa nia ya kufanikisha hatua hiyo. Aidha , Mhe. Kassim Majaliwa ameeleza kuwa, Rais Samia Suluhu Hassan amepongeza uamuzi wa wananchi hao na kwamba serikali itaendelea kuwekeza katika kuboresha miundombinu ya eneo la Msomera.  “Napenda k...

FANYIENI UTAFITI MAZAO YA NGANO NA ALIZETI - KANALI NGATA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, ametoa maagizo kwa Meneja wa shamba la SUMAJKT Bassotu Sajinitaji Bahati Kidenya, kufanya utafiti mzuri wa mazao ya ngano na alizeti ili shirika likiamua kuwekeza katika kilimo hicho kiwe na tija. Kanali Petro Ngata, ametoa maagizo  hayo leo tarehe  12 Augosti 2022, alipokuwa katika ziara ya kukagua shamba hilo lililopo katika kijiji cha Bassotu , Wilaya ya Hanang'i Mkoani Manyara.  Kanali Ngata ameongeza kuwa  Bassotu kuna faida kubwa endapo SUMAJKT itafanikiwa kupata eneo kubwa na kuanza na aina ya mazao mawili ambayo ni ngano na katamu (alizeti za miba). "Ngano na katamu ni mazao ambayo tukizalisha tutakuwa na uhakika wa kupata faida" ameeleza Kanali Ngata.  Aidha, Kanali Petro Ngata,  ameeleza kuwa shirika litaanza kuliwekea mipango mizuri na ya haraka shamba hilo, endapo msajili wa hazina atakubali kutoa eneo kwa SUMAJKT.      ...

IJUE SIRI YA MAFANIKIO YA JKT KATIKA KILIMO

MKUU wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema pamoja na kuwa na mabadiliko ya tabia nchi lakini bado katika vipando vya Jeshi la kujenga taifa na mashamba yake kwa  na vikosi yameendelea kufanya vizuri na mazao yanastawi kwa jinsi ambavyo walikuwa wametalajia. Amesema kuwa wao walishaona changamoto hizo za mabadiliko  ya tabia nchi hivyo walishaanza kufanya mawasiliano na mamlaka ya hali ya hewa ambapo walikuwa wanapewa taarifa juu ya mabadiliko hayo hususani kwenye eneo la mvua kwamba msimu huo mvua zitawahi ama kuchelewa na kama zitawahi zitakuja kwa viwango vidogo. Amesema kuwa baada ya kupata taarifa hiyo wao kama Jeshi la kujenga taifa walikaa chinin nakuweza kujipanga na kuona aina ya mbegu ambazo zitaweza kuendana na hali ya hewa. Brigedia Mabena ameyasema hayo Agosti 7 kwenye maonyesho ya nanenane ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Mbeya wakati alipotembelea banda la JKT pamoja na mambo mengine amesema kuwa katika kikosi cha 847 KJ ni Milundikwa na...

ZINGATIENI UBORA KATIKA MIRADI YA UJENZI-KANALI NGATA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amekagua Miradi tisa ya ujenzi jijini Dodoma inayojengwa na SUMAJKT Construction Company Ltd, kupitia Kanda mbali mbali. Kanali Petro Ngata, amefanya ziara hiyo jana tarehe 22 Julai 2022 alipotembelea  miradi mbali mbali ya ujenzi katika mji wa serikali Mtumba , Shule ya Mfano Iyumbu pamoja ukaguzi wa mitambo katika kiwanda cha mabati SUMAJKT Roofing Company Limited kilichopo Dodoma. Pia amekagua maendeleo ya Ujenzi wa jengo la wizara ya Katiba na Sheria, unaotekelezwa na SUMAJKT Construction Company Limited Ujenzi kanda ya Mashariki,    Pia amekagua Ujenzi wa jengo la Mwanasheria Mkuu wa Serikali unaotekelezwa na  SUMAJKT ujenzi Kanda ya Kati Dodoma, Ujenzi wa Jengo la Wakili Mkuu wa Serikali  unaotekelezwa na SUMAJKT  Makao Makuu, Ujenzi wa Jengo la Wakala wa Mtandao wa Serikali, Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya waziri mkuu, jengo la  Sera,  Ujen...

WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2022

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linawaita vijana waliohitimu elimu ya Sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2022 kutoka shule zote za Tanzania bara kuhudhuria Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria. Sanjari na wito huo, JKT limewapangia makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 03 hadi June 2022. Vijana walioitwa wamepangwa katika kambi za JKT Rwamkoma-Mara, JKT Msange-Tabora, JKT Ruvu-Pwani, JKT Mpwapwa na Makutupora JKT-Dodoma, JKT Mafinga-Iringa, JKT Mlale-Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba-Tanga, JKT Makuyuni-Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila -Kigoma, JKT Itaka-Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa -Rukwa, JKT Nachingwea-Lindi na JKT Kibiti-Pwani na Oljoro JKT-Arusha. Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (Physical disabilities) waripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo. JKT inawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo.     1. ...

“NAENDELEZA KAZI NINAZOZIJUA”- MEJA JENERALI MABELE

 Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT ) Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele tarehe 19/5/2022 ametimiza mwaka Mmoja madarakani huku akiendelea kutekeleza vema  azma ya Jeshi la Kujenga Taifa kujilisha pamoja na malezi ya vijana. Aidha tarehe 19 Mei 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alimteua kwa kipindi hicho akiwa  Brigedia Jenerali Rajabu Nduku Mabele kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afsa mtendaji mkuu wa SUMAJKT  Hatua iliyokuja kufuatia  aliyekuwa Mkuu wa Jeshi hilo, Meja Jenerali Charles Mbuge kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera akichukua nafasi ya Brig Jenerali Marco Elisha Gaguti aliyehamishiwa Mtwara. katika kipindi cha Mwaka mmoja akiwa madarakani Meja Jenerali Mabele ameendelea kutekeleza Majukumu yake kwa weledi ikiwa ni pamoja na kuliongoza vema Jeshi la Kujenga Taifa na Shirika lake la Uzalishaji Mali S...

MWAKA MMOJA WA MKUU WA JKT NA AFISA MTENDAJI MKUU SUMAJKT KATIKA UONGOZI WAKE

KATIKA KUTIMIZA MWAKA MMOJA WA UONGOZI WA MKUU WA JKT NA AFISA MTENDAJI MKUU SUMAJKT HAYA NDIO YALIYOJIRI. SHIRIKA LA UZALISHAJI MALI LA JESHI   LA KUJENGA TAIFA (SUMAJKT) LINAENDELEA KUPIGA HATUA KATIKA SEKTA YA VIWANDA, SEKTA YA UJENZI, UHANDISI NA USHAURI, SEKTA YA HUDUMA NA BIASHARA, SEKTA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI. KATIKA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA WA UONGOZI WA MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA NA AFISA MTENDAJI MKUU WA SUMAJKT MEJA JENERALI RAJABU NDUKU MABELE SHIRIKA LIMEPATA MAFANIKIO MBALIMBALI . KWANZA KATIKA SEKTA YA VIWANDA. NOVEMBA 04, 2021 SHIRIKA LILIZINDUA KIWANDA CHA KUTENGENEZA TAA  SUMAJKT SKYZON COMPANY LIMITED SAMBAMBA NA UZINDUZI WA MAGARI NA ZANA NA KILIMO MLALAKUWA JIJINI DAR ES SALAAM. VILE VILE OCTOBA 29, 2021 MEJA JENERALI MABELE ALIZINDUA KIWANDA CHA UTENGENEZAJI MABATI SUMAJKT ROOFING COMPANY LIMITED AMBACHO HIVI SASA TAYARI KIMESIMIKWA MITAMBO JIJINI DODOMA. AIDHA SHIRIKA LIMEPIGA HATUA KATIKA SEKTA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI. PIA KUSIMIKWA MITAMBO YA KU...

KAMPUNI YA USAFI SUMAJKT CLEANING AND FUMIGATION YAPONGEZWA

Video hiyo ni Meneja wa kituo cha mabasi cha Mbezi Luis Bwana Mayira Mkama akipongeza Kampuni ya Usafi SUMAJKT Cleaning and Fumigation kwa huduma nzuri wanayotoa.  Katika mahojiano na SUMAJKT TV tarehe 09 April 2022 Meneja Mayira alisema  kuwa SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co. Limited wanatoa huduma nzuri kituoni hapo kutokana na kuwa na Watendaji wa kutosha pamoja na vitendea kazi vya kutosha tofauti na makampuni mengine ambapo mwanzoni huleta wafanyakazi wengi na baadae hupungua na eneo la kufanya usafi ni kubwa. Aidha ameeleza kuwa Uongozi wa Mbezi Luis Bus Terminal umekuwa ukishirikiana na kampuni hiyo katika kuhakikisha jukumu hilo linatimizwa ipasavyo. Meneja Mayira amezisihi kampuni zingine za usafi kuiga mfano kwa SUMAJKT. SUMAJKT Cleaning and Fumigation Company Limited ni kampuni tanzu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) iliyojizatiti katika utoaji wa huduma ya usafi na unyunyiziaji dawa.  Kampuni imejizatiti katika utoaji wa hudum...

HII NDIO SIRI YA MAFANIKIO YA KIWANDA CHA USHONAJI NGUO SUMAJKT GARMENTS COMPANY LIMITED

Katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali kupitia mageuzi ya viwanda Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) halikubaki nyuma katika sekta ya viwanda. Miongoni mwa viwanda vilivyoanzishwa mwaka 2017 SUMAJKT Garments ni kiwanda kimojawapo ambacho kinafanya vizuri katika soko la ushindani na kimekuwa kimbilio la jamii kutokana na umahiri katika kazi ya ushoni. SUMAJKT Garments Company Limited inafanya vizuri katika shughuli za ushonaji nguo na Kupitia Video hiyo utapata kujua shughuli zote za ushonaji nguo sambamba na kudarizi  vinavyofanyika  kiwandani hapo.  Mnamo tarehe 2/02/2022 Kamera za SUMAJKT TV zilifika kiwandani hapo kufuatilia mchakato mzima wa ushonaji nguo na kupitia video hiyo hayo ndio yaliyojiri. Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Sylvester Ntandu pamoja na Maafisa wasaidizi wake wanakuelezea utendaji kazi wa kiwanda hicho. SUMAJKT Garments Company Limited kinashona mavazi ya aina mbali mbali zikiwemo nguo za watu b...