Kaimu naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT), Kanali Shija Lupi amekabidhi hundi ya zaidi ya Milioni moja na laki nane (1,800,000/=) kwa Bwana Issack Kalumba ambaye anaendesha baiskeli katika nchi mbalimbali Barani Afrika kwa lengo la kuinua na kutangaza lugha ya kiswahili pamoja na utalii wa Tanzania kupitia majukwaa rasmi katika nchi hizo.
Kanali Lupi alikabidhi hundi hiyo kwa Bwana Kalumba tarehe 04 March 2022 ofisini kwake Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa jijini Dar es salaam.
SUMAJKT imetoa hundi ya kiasi hicho cha pesa kuunga mkono juhudi za Bwana Isaack Kalumba ambaye alileta maombi SUMAJKT la kusaidiwa fedha hizo ili kuweza kutatua baadhi ya changamoto anazokutana nazo katika mzunguko wa Safari yake ya kuinua na kutangaza lugha ya kiswahili Barani Afrika.
Bwana Isaack Kalumba ni Mtanzania anaeendesha baiskeli katika nchi mbalimbali Barani Afrika kwa lengo la kuinua na kuitangaza lugha ya kiswahili Afrika na kuunga mkono juhudi za Serikali za kukuza na kuzungumza lugha ya kiswahili katika nchi za kiafrika.
Pia bwana Kalumba tangu aanze harakati za kutangaza kiswahili tarehe 21Oktoba 2021 Jijini Dar es salaam, ameweza kupita nchi kadhaa zikiwemo Kenya, Sudani Kusini, Uganda na Rwanda ambapo anatangaza lugha ya kiswahili kupitia majukwaa rasmi, Taasisi mbalimbali, Mashirika, Vyuo vikuu na shule mbalimbali.
Bwana Isaack Kalumba amelishukuru Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kwa kumpatia fedha hizo na kuahidi kuendelea kushirikiana na SUMAJKT katika harakati zake za kuinua na kutangaza lugha ya kiswahili ambapo kwasasa anajiandaa na safari ya kuelekea nchi za Malawi, Zambia, Zimbabwe, Botswana na nchini Afrika Kusini.
Comments
Post a Comment