Skip to main content

SUMAJKT YAKABIDHIWA MRADI WA UJENZI WA JENGO LA USAFISHAJI FIGO LUGALO



Kampuni ya ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited imekabidhiwa eneo  kwa ajili ya  Ujenzi wa Jengo la Usafishaji Figo, Ukumbi wa mkutano na Jengo la Uchunguzi wa magonjwa Lugalo  jijini Dar es Salaam. 

Makabidhiano hayo yamefanyika  tarehe 11 machi 2022, ambapo maandalizi ya usafishaji wa eneo hilo la Ujenzi yameanza siku hiyo.

 Eneo hilo litajengwa Ukumbi wa mkutano, Jengo la Uchunguzi wa magonjwa pamoja na Jengo dogo la 

wagonjwa baada ya matibabu.

Aidha lengo la mradi huo ni kuboresha huduma za Usafishaji Figo (Dialysis) na huduma nyingine zinazotolewa katika hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam. 

SUMAJKT kupitia Kampuni yake ya Ujenzi (SUMAJKT Construction Company Ltd) imeanza utekelezaji wa Ujenzi wa Miradi hiyo ambayo kukamilika ndani ya miezi sita.

SUMAJKT kupitia Kampuni yake ya Ujenzi (SUMAJKT  Construction Company Ltd) imekuwa ikiaminiwa kwa kukabidhiwa miradi mbalimbali ya Ujenzi na Serikali pamoja na Taasisi binafsi kwa sababu ya kukamilisha Miradi hiyo katika ubora na wakati.

Comments

Popular posts from this blog

SUMAJKT YAKABIDHI VIATU VYA SHULE JOZI 500

 Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kupitia Kampuni tanzu iitwayo SUMAJKT shoes and leather Products Co LTD. tarehe 04 Novemba 2022 limekabidhi viatu vya ngozi jozi 500 kwa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao yenye kauli mbiu “Samia nivike viatu”. Aidha, makabidhiano ya viatu hivyo yamefanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam. Akielezea historia ya kiwanda Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Mathias John amesema, Kiwanda cha  viatu na bidhaa za ngozi SUMAJKT Shoes and Leather Product Co. LTD Kilianzishwa Jul 2017 na majukumu yake yakiwa ni uzalishaji wa viatu na bidhaa mbalimbali za ngozi.  Aidha, toka kuanzishwa Kqa  kiwanda hicho kimeendelea kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa kununua vifaa na mashine za kisasa ili kuzalisha bidhaa zenye ubora.  Bidhaa zinazozalishwa ni viatu kwa ajili ya taasisi za ulinzi, viatu vya usalama (safety boots), viatu vya maofisini na viatu vya shule.  Uwezo wa kiwanda ni kuzalisha viatu jozi 500 kwa siku na Kup

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA MIRADI YA UJENZI KANDA YA ZIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata leo tarehe 28 Oktoba 22 amefanya ziara katika miradi ya ujenzi inayoendelea kujengwa kanda ya ziwa. Kanali Petro Ngata amekagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Ziwa ambayo ni mradi wa ujenzi wa jengo la uchunguzi (Dignostic Center) katika hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama , Mradi wa uondoaji wa kifusi eneo la hanga uwanja wa ndege wa Chato Mkoani Geita na Mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Msalala. Aidha, Kanali Ngata  amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuhusu ukamilishwaji wa  jengo la ofisi za Halmashauri. SUMAJKT imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali ya ujenzi nchini kupitia kampuni yake ya ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited ambayo ina kanda saba za ujenzi.

MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA ZIARA MAFINGA MKOANI IRINGA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amehitimisha Ziara yake kwa kutembelea Kikosi cha JKT Mafinga Mkoani Iringa ambapo SUMAJKT katika kikosi hicho imewekeza katika ufugaji wa mifugo mbali mbali ikiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe. Bonyeza video hiyo kuona yaliyojiri.