Skip to main content

Posts

Showing posts with the label Wito wa Kujiunga na Mafunzo JKT kwa Mujibu wa Sheria (2022)

WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2022 AWAMU YA PILI

  JESHI la Kujenga Taifa (JKT), tunatoa siku tatu kwa vijana walioitwa kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2022, ambao hawajaripoti mpaka sasa kuripoti makambi waliyopangiwa ya JKT mara moja. Pia tumetoa nyongeza ya majina ya vijana waliohitimu elimu ya kidato cha sita mwaka 2022 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2022. Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali, Hassan Mabena anatoa wito kwa vijana waliochaguliwa wa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria mwaka 2022 Awamu ya Pili ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi wiki ijayo na yataendeshwa kwa muda wa miezi mitatu.  Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele anawataka kuripoti makambini vijana wote walioitwa kuhudhuria Mafunzo ya JKT Kwa Mujibu wa Sheria kwa mwaka 2022, ambao hawajaripoti mpaka sasa mripoti makambi ya JKT mara moja. Vijana  waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti makambi ya JKT yaliyo karibu na maeneo wanayoishi. "Vijana wote waliochaguliwa  

WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2022

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linawaita vijana waliohitimu elimu ya Sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2022 kutoka shule zote za Tanzania bara kuhudhuria Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria. Sanjari na wito huo, JKT limewapangia makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 03 hadi June 2022. Vijana walioitwa wamepangwa katika kambi za JKT Rwamkoma-Mara, JKT Msange-Tabora, JKT Ruvu-Pwani, JKT Mpwapwa na Makutupora JKT-Dodoma, JKT Mafinga-Iringa, JKT Mlale-Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba-Tanga, JKT Makuyuni-Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila -Kigoma, JKT Itaka-Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa -Rukwa, JKT Nachingwea-Lindi na JKT Kibiti-Pwani na Oljoro JKT-Arusha. Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (Physical disabilities) waripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo. JKT inawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo.     1. Bukta ya