Skip to main content

KAMPUNI YA USAFI SUMAJKT CLEANING AND FUMIGATION YAPONGEZWA




Video hiyo ni Meneja wa kituo cha mabasi cha Mbezi Luis Bwana Mayira Mkama akipongeza Kampuni ya Usafi SUMAJKT Cleaning and Fumigation kwa huduma nzuri wanayotoa. 

Katika mahojiano na SUMAJKT TV tarehe 09 April 2022 Meneja Mayira alisema  kuwa SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co. Limited wanatoa huduma nzuri kituoni hapo kutokana na kuwa na Watendaji wa kutosha pamoja na vitendea kazi vya kutosha tofauti na makampuni mengine ambapo mwanzoni huleta wafanyakazi wengi na baadae hupungua na eneo la kufanya usafi ni kubwa.


Aidha ameeleza kuwa Uongozi wa Mbezi Luis Bus Terminal umekuwa ukishirikiana na kampuni hiyo katika kuhakikisha jukumu hilo linatimizwa ipasavyo.

Meneja Mayira amezisihi kampuni zingine za usafi kuiga mfano kwa SUMAJKT.


SUMAJKT Cleaning and Fumigation Company Limited ni kampuni tanzu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) iliyojizatiti katika utoaji wa huduma ya usafi na unyunyiziaji dawa.

 Kampuni imejizatiti katika utoaji wa huduma za usafi katika maeneo yafuatayo:


a. Usafi wa maofisini 

b. Usafi wa sakafu za                       majengo makubwa 

c. Usafi wa kapeti 

d. Usafi wa hospitali 

e. Usafi wa sokoni 

f. Usafi wa barabara 

g. Uzoaji taka 

h. Upandaji miti 

i.  Utunzaji wa bustani na sehemu za kupikia


Kurudisha muonekano uliopotea kuwa wa kuvutia, kama eneo lako linakosa muonekano mzuri na wakuvutia, sinki na dishi za kunawia mikono ikiwa zimepoteza muonekano wake Kampuni ya SUMAJKT Cleaning and Fumigation ipo kwa ajili ya kurudisha mwonekano mzuri wa mazingira yako.


Kampuni katika upande wa Unyunyiziaji dawa inatoa huduma kutegemeana na aina tofauti za vimelea na wadudu wa aina tofauti ambapo dawa na kemikali hutumika kwenye unyunyiziaji. 


Aina zote za dawa za unyunyiziaji kwa wadudu na vimelea ni sumu hatari kwa afya ya binadamu na wanyama.


Hivyo inashauriwa kutumia wataalamu wenye leseni zilizothibitishwa na mamlaka ya dawa na unyunyiziaji kufanya kazi hiyo.


Aidha Kampuni ina uzoefu wa kazi za usafi na unyunyiziaji dawa kwa wateja mbali mbali ikiwa na wataalamu na vifaa bora vya kisasa na imejizatiti kufanya kazi hii kwa umakini na usalama wa hali ya juu, hivyo kuwa kampuni sahihi ya usafi na unyunyiziaji dawa wa eneo lako.

Kampuni inatoa huduma ya unyunyiziaji dawa katika:


a. Mahoteli 

b. Maofisini 

c. Hospitali 

d. Migahawa 

e. Maghala 

f.  Makontena 

g. Vyuoni 

h. Majumbani 

i.  Bustani 

j.  Dawa za nafaka 


Karibuni kwa huduma bora zinazotolewa kwa viwango vya juu, Ofisi zetu zipo Mwenge mkabala na Efatha Ministry Dar es Salaam Tanzania. 


Kwa mawasiliano zaidi tunapatikana kwa simu namba +255734281585/+255712659139 au 

barua pepe :sumajktcleaning@gmail.com au info@sumajkt.go.tz

Tovuti: www.sumajkt.go.tz

Karibuni .



Comments

Popular posts from this blog

SUMAJKT YAKABIDHI VIATU VYA SHULE JOZI 500

 Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kupitia Kampuni tanzu iitwayo SUMAJKT shoes and leather Products Co LTD. tarehe 04 Novemba 2022 limekabidhi viatu vya ngozi jozi 500 kwa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao yenye kauli mbiu “Samia nivike viatu”. Aidha, makabidhiano ya viatu hivyo yamefanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam. Akielezea historia ya kiwanda Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Mathias John amesema, Kiwanda cha  viatu na bidhaa za ngozi SUMAJKT Shoes and Leather Product Co. LTD Kilianzishwa Jul 2017 na majukumu yake yakiwa ni uzalishaji wa viatu na bidhaa mbalimbali za ngozi.  Aidha, toka kuanzishwa Kqa  kiwanda hicho kimeendelea kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa kununua vifaa na mashine za kisasa ili kuzalisha bidhaa zenye ubora.  Bidhaa zinazozalishwa ni viatu kwa ajili ya taasisi za ulinzi, viatu vya usalama (safety boots), viatu vya maofisini na viatu vya shule.  Uwezo wa kiwanda ni kuzalisha viatu jozi 500 kwa siku na Kup

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA MIRADI YA UJENZI KANDA YA ZIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata leo tarehe 28 Oktoba 22 amefanya ziara katika miradi ya ujenzi inayoendelea kujengwa kanda ya ziwa. Kanali Petro Ngata amekagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Ziwa ambayo ni mradi wa ujenzi wa jengo la uchunguzi (Dignostic Center) katika hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama , Mradi wa uondoaji wa kifusi eneo la hanga uwanja wa ndege wa Chato Mkoani Geita na Mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Msalala. Aidha, Kanali Ngata  amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuhusu ukamilishwaji wa  jengo la ofisi za Halmashauri. SUMAJKT imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali ya ujenzi nchini kupitia kampuni yake ya ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited ambayo ina kanda saba za ujenzi.

MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA ZIARA MAFINGA MKOANI IRINGA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amehitimisha Ziara yake kwa kutembelea Kikosi cha JKT Mafinga Mkoani Iringa ambapo SUMAJKT katika kikosi hicho imewekeza katika ufugaji wa mifugo mbali mbali ikiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe. Bonyeza video hiyo kuona yaliyojiri.