Skip to main content

MKUU WA JKT NA AFISA MTENDAJI MKUU WA SUMAJKT MEJA JENERALI RAJAB NDUKU MABELE AMPONGEZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMIRI JESHI MKUU MHE. SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUTIMIZA MWAKA MMOJA MADARAKANI









 SUMAJKT NI KITUO CHA BIDHAA NA HUDUMA BORA

“Kazi iendelee” ni Kauli mbiu ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan alianza nayo tangu aapishwe kushika madaraka hayo ambayo kwasasa ametimiza mwaka mmoja.


Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) halikubaki nyuma katika kuunga mkono kauli mbiu hiyo kwa vitendo, limekuwa sambamba na Serikali ya awamu ya sita kuhakikisha kazi zinaendelea kwa manufaa ya Shirika, JKT na Taifa kwa Ujumla.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele ametoa pongezi zake za dhati kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kutimiza mwaka mmoja wa uongozi, Aidha amemshukuru kwa kuendelea kuliamini SUMAJKT na kulipatia kazi mbalimbali, kupitia kampuni ya ujenzi (SUMAJKT Construction Company Ltd) ikiwemo Mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dodoma, Mradi wa ujenzi wa ofisi za mtandao wa Serikali.

Vilevile Mradi wa ujenzi wa Makamo wa Rais Mazigira na Muungano, Mradi wa ujenzi wa ofisi za Wizara ya Kilimo, Mradi wa ujenzi wa ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Mradi wa ujenzi wa Waziri Mkuu kazi, Mradi wa ujenzi wa ujenzi ofisi


ya uwekezaji, Ujenzi wa ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali, ofisi zote zinajengwa Mtumba jijini Dodoma.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele ameeleza kuwa, Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) lilianzishwa kwa amri ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Na.116 ya mwaka 1982 chini ya Sheria ya Uanzishwaji Mashirika ya Umma. Act No 23 of 1974 (Cap 119 RE 2002).

Meja Jenerali Rajabu Mabele amefafanua kuwa, SUMAJKT lilianzishwa kwa lengo la kufanya biashara na kuzalisha faida ili kuisaidia Serikali gharama za mafunzo ya Vijana wanaojiunga na JKT pamoja na Kujenga Uchumi wa Taifa.

Meja Jenerali Mabele amesema kuwa SUMAJKT kupitia Kampuni zake Tanzu na miradi yake mbalimbali limeendelea kujipambanua zaidi katika soko la ushindani kwa kuhakikisha linazalisha bidhaa na kutoa huduma bora zinazokidhi mahitaji ya wateja.

SUMAJKT kupitia faida linayoipata kutoka katika Kampuni zake Tanzu na Miradi yake mbalimbali limeendelea kuchangia gharama za kuendesha mafunzo ya vijana wanaojiunga na JKT, kutekeleza dhumuni la uanzishwaji wake.


Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Mabele ameongeza kuwa Shirika limezidi kuzalisha ajira kwa kuajiri vijana wa Kitanzania kupitia Kampuni zake Tanzu na Miradi yake mbalimbali akitolea mfano Kampuni ya Ulinzi SUMAJKT Guard Ltd hadi sasa imeajiri idadi ya vijana 14704 ambao wanafanya kazi za ulinzi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Vilevile kwa Vijana wanaojiunga na JKT baada ya kupata mafunzo ya awali ya kijeshi hujifunza stadi za kazi kupitia Kampuni hizo ikiwemo Ushonaji, Ufundi Seremala, Ufundi viatu, Ujenzi pamoja na ufugaji samaki kwa njia ya matenki, hivyo kuwasaidia kujiajiri pindi wanapomaliza Mkataba wao JKT.

Pia imekuwa kituo cha Wanafunzi kufanya mafunzo kwa vitendo (field & Internship) kutoka vyuo mbalimbali nchini. Aidha, SUMAJKT limefanikiwa Kuchangia Pato la Taifa kwa

kulipa kodi stahiki kupitia Kampuni zake Tanzu na Miradi yake mbalimbali, na kwa kutoa gawio kupitia Mfuko Mkuu wa Serikali (Hazina).

Pia Meja Jenerali Mabele ameongeza kuwa SUMAJKT Katika Uzalishaji Mali limefanikiwa kuwa na shughuli ambazo zimegawanyika katika sekta zifuatazo: -


Sekta ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi

Kilimo

Shirika linajishughulisha na mashamba makubwa ya biashara ambayo ni shamba la Alizeti Hanang Mkoani Manyara, Shamba la mahindi na maharage Tanganyika mkoani Katavi, shamba la Mpunga Chita mkoani Morogoro. Pia kuna shamba la maharage Milundikwa mkoani Rukwa, Shamba la USA River mkoani Arusha na shamba la zaidi ya ekari 12,000 ambalo Serikali imelikabidhi kwa SUMAJKT, awali lilikuwa likifahamika kwa jina la Kilombero Plantation Limited (KPL), katika shamba hilo unafanyika uzalishaji wa mpunga na mahindi, shamba hilo lina miundo mbinu ya kisasa ya umwagiliaji, mashine za kuhifadhi na kuongeza thamani mazao ya mpunga na mahindi.

Ufugaji

Shirika, linajishughulisha na Ufugaji wa ng‟ombe wa maziwa na nyama katika eneo la Oldonyo Sambu na Oljoro JKT mkoani Arusha, mafinga mkoani Iringa, na Misenyi mkoani Kagera.


Uvuvi

Shirika limeanzisha mradi wa SUMAPONICS katika kikosi cha Mbweni JKT Jijini Dar es Salaam ambao unahusika na utengenezaji na usambazaji mifumo ya kufuga samaki katika matenki (Recirculation Aquaculture System - RAS) sanjari na uzalishaji na usambazaji vifaranga wa samaki.

Sekta ya viwanda

SUMAJKT kupitia Sekta ya Viwanda inaboresha viwanda vilivyopo na kuanzisha viwanda vipya

Shirika linamiliki Viwanda vifuatavyo:-

Kiwanda cha Ushonaji (SUMAJKT Garments CO.LTD).

Kiwanda kipo katika kituo cha uwekezaji cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani JKT jijini Dar es salaam, Kiwanda hiki kinashona mavazi ya aina mbalimbali zikiwemo nguo za watu binafsi, sare za vyombo vya ulinzi na usalama, shule, kampuni na Taasisi mbalimbali.

Kiwanda cha Samani (SUMAJKT Chang’ombe Furniture Co.Ltd)

Kiwanda hiki kipo chang‟ombe jijini Dar es salaam, kinatengeneza samani za kisasa zenye ubora kwa matumizi ya nyumbani na maofisini.


Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za Ngozi

(SUMAJKT Leather Product)

kiwanda hiki kwa sasa kimeanza kwa kutengeneza viatu vya aina mbalimbali zikiwemo buti za vyombo vya ulinzi na usalama, viatu vya shule, viatu vya watoto na watu wazima. Kiwanda tajwa kipo Mlalakuwa jijini Dar es salaam. Shirika limeongeza Mashine mpya ya kisasa ya kutengeneza soli za viatu (Injection Moulding Machine). Mashine ina uwezo wa kuzalisha jozi 150 kwa saa sawa na „pair‟ 300. Pia zimenunuliwa mashine nyingine saidizi ambazo ni “Pre Heating” kwa ajili ya kukaushia malighafi zenye unyevunyevu, “Mixer” kwa ajili ya kuchanganya Malighafi, “Chiller” kwa ajili ya kupoza mashine na “Grinder” kwa ajili ya kusaga malighafi.

Kiwanda cha Maji ya Kunywa (SUMAJKT Bottling Co.Ltd)

Kiwanda hiki pia kipo Mgulani Dar es salaam ambacho kinatumia mitambo ya kisasa kuzalisha maji ya kunywa yajulikanayo kwa jina la Uhuru Peak na kinasambaza na kuuza maji yake katika maeneo mbalimbali hapa nchini.


Kiwanda cha taa (SUMAJKT Skyzone Co.Ltd)

Hiki ni kiwanda cha ubia kati ya SUMAJKT na kampuni ya Everlight Africa Co.Ltd, Kiwanda kipo Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa jijini Dar es salaam, kimekamilika kwa asilimia Tisini na Tano (95%) na mitambo yote imeishasimikwa, hivi sasa wanasubiriwa wabia ili kuanza uzalishaji wa taa za kisasa aina ya LED za barabarani, uwanja wa ndege, uwanja wa mpira, na bustani.

Kiwanda cha Mabati na Misumari (SUMAJKT Roofing Company Ltd).

Kiwanda hiki kipo jijini Dodoma, Mashine za Misumari ya kawaida na ya mabati pamoja na Mashine za kutengeneza mabati zote zimeshawasili Tanzania, wanasubiriwa wataalamu kutoka Nchini China kwa ajili ya kusimika Mashine hizo. Kiwanda kikikamilika kitakuwa kikizalisha Mabati ya aina ya Vigae, migongo midogo na mipana.

Kiwanda cha Nafaka Mlale (SUMAJKT Mlale Milling Co.Ltd)

Shirika limeingia ubia na kikosi cha Mlale JKT mkoani Ruvuma katika kiwanda cha kuchakata mahindi ambacho


kinazalisha unga safi wa sembe unaojulikana kwa jina la SUMAJKT Mlale Sembe.

Sekta ya Huduma na Biashara

SUMAJKT Port and Services Co.Ltd.

Kampuni hii inasimamia wafanyakazi wa kutwa katika Mamlaka ya Bandari (TPA) Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Kigoma, kasanga na kemondo (Kagera), kyela (Mbeya) na Mwanza.

SUMAJKT Logistic Company Ltd.

Hii ni kampuni ya uondoaji na usafirishaji mizigo bandarini ambao msingi wa uanzishwaji wake ulikuwa ni kulipunguzia Shirika gharama za uondoshaji mizigo inayowasili bandarini. Kwa sasa linafanya kwa biashara ili kuongeza pato la Shirika.

SUMAJKT Catering Co.Ltd.

Shirika linatoa huduma za Kumbi ambazo ni Uhuru unaochukua watu 1000 na Ukumbi wa Umoja unaochukua watu idadi 500 kwa ajili ya shughuli mbalimbali zikiwemo harusi, mikutano, semina na warsha. Pia inatoa huduma ya chakula na vinywaji hutolewa katika kumbi hizo, kumbi zote zinapatikana eneo la mwenge jijini Dar es salaam. SUMAJKT Auction Mart Co. Ltd

Ni kampuni inayo shughulika na Udalali, Ukusanyaji Madeni, Ushuru na kukaza hukumu za mahakama.

SUMAJKT Guard Ltd.


Kampuni hii inatoa huduma ya ulinzi binafsi katika mashirika ya Umma, Taasisi na watu binafsi nchi nzima, mpaka sasa imeajiri idadi ya wafanyakazi 14704, vijana wazalendo waliopitia mafunzo ya awali ya JKT na Mgambo. Huduma zitolewazo na Kampuni hizi zinahusisha;  Ulinzi wa milango (access control)

 Kamera za usalama (CCTV Camera)

 Mfumo wa „alarm‟ katika vyombo vya moto

 Uzio wa umeme

 Mfumo wa ufuatiliaji magari

 Mfumo wa alarm kwa ajili ya kudhibiti moto

 Mashine ya ukaguzi kwa ajili ya kudhibiti

moto

 Mashine ya ukaguzi kwa kutumia mionzi

 Ufungaji wa simu ya upepo (radio call)

 Walinzi wa usalama (security guard)

 Walinzi wa kutumia mbwa.

 Kufunga na kufungua mlango kwa umeme

(automotive gates).

SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co.Ltd.

Kampuni hii inatoa huduma ya usafi na umwagiliaji dawa za wadudu katika Taasisi binafsi, Mashirika ya Umma na kwa watu binafsi, ofisi zake zipo Mwenge jijini Dar es Salaam.

SUMAJKT Insurance broker Ltd.


Kampuni hii inatoa Bima ya Maisha na Bima zisizo za Maisha mfano bima ya afya, magari, nyumba, safari na nyinginezo.

Shule za Sekondari Jitegemee na Kawawa

Shirika linatoa huduma ya elimu Kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita kupitia Shule zake za Sekondari Jitegemee iliyopo Mgulani jijini Dar es salaam na Kawawa Sekondari iliyopo Mafinga mkoani Iringa, jitihada zinaendelea kufanyika kuhakikisha ufaulu unaongezeka.

SUMAJKT Tower - Dodoma

Shirika lipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa Ujenzi wa jengo litakalo tumika kwa ajili ya biashara kwa kukodisha Taasisi mbalimbali na ofisi za SUMAJKT katika eneo la Medeli East Manispaa ya Dodoma. Jengo linajulikana kwa jina la SUMAJKT Tower. Ni jengo la kisasa kubwa lenye ukubwa wa ghorofa tano.

Uuzaji na usambazaji wa zana za kilimo

Mradi huu umesaidia kukuza sekta ya kilimo nchini kwa kuwauzia wakulima wadogo na wakubwa Matrekta na zana mbalimbali za kilimo. Kwasasa mradi unauza Matrekta aina ya New Holland na vipuli katika eneo la mwenge jijini Dar es salaam.

Sekta ya Ujenzi, Uhandisi na Ushauri


Sekta hii inatekeleza shughuli zake kupitia Kampuni ya ujenzi (SUMAJKT Construction Co. Ltd), Kampuni ya Umeme (SUMAJKT Electrical Co.Ltd) na Kampuni ya Ushauri majenzi (SUMAJKT Consultancy Bureau Co. Ltd).

Shirika kupitia kampuni yake ya Ujenzi ya SUMAJKT Construction Company Limited (SUMAJKT CCL) linatekeleza miradi ya Ujenzi kupitia Kanda zake saba (7) za ujenzi ziliwekwa kimkakati katika maeneo ya Tanzania. Pamoja na miradi iliyopo chini ya Makao Makuu ya Kampuni ya Ujenzi, Kampuni inafanya shughuli zifuatazo: -

 Ujenzi wa Majengo

 Ujenzi wa Miundo mbinu ya barabara na Maji

 Ujenzi wa Miundo mbinu ya Umeme

 Inatoa huduma ya Ushauri wa Kihandisi na

Usanifu Majengo.

SUMAJKT kupitia Kampuni yake ya Ujenzi imefanikiwa kutekeleza Miradi mbalimbali yenye maslahi Kitaifa katika ubora na kwa wakati, hali ambayo imepelekea kuaminiwa na Serikali pamoja na Taasisi.

SUMAJKT Pharmaceuticals Co. Ltd

Shirika limeanzisha Kampuni ya SUMAJKT Pharmaceutical Co. Ltd (SPCL) kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali katika sekta ya Afya kama; huduma za Madawa, Vifaa


tiba, Vifaa vya uchunguzi, vifaa vya Maabara na vifaa vya huduma za uchunguzi na Tafiti mbalimbali za Afya. Aidha inalenga kufungua viwanda vya madawa, na maduka makubwa ndani na nje ya Mkoa wa Dar Es Salaam ya kutoa na kusambaza huduma na vifaa mbalimbali vya Afya katika Vituo vya Afya na Maduka yanayouza Madawa na vifaa tiba. Kwasasa Ujenzi wa jengo la Kampuni hiyo unaendelea eneo la Mwenge jijini Dar Es Salaam.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele amehitimisha kwa kusema kuwa SUMAJKT ni kituo cha Bidhaa na Huduma bora, hivyo anatoa rai kwa Serikali, Taasisi na watu binafsi kuendelea kuliamini Shirika hilo.

Aidha, kwa namna ya pekee amempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza mwaka mmoja tangu ashike madaraka hayo, na kusema kuwa Shirika la Uzalishaji Mali la Kujenga Taifa (SUMAJKT) lipo pamoja naye katika Ujenzi wa Uchumi wa Taifa “KAZI IENDELEE”.


MWISHO.


Comments

Popular posts from this blog

SUMAJKT YAKABIDHI VIATU VYA SHULE JOZI 500

 Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kupitia Kampuni tanzu iitwayo SUMAJKT shoes and leather Products Co LTD. tarehe 04 Novemba 2022 limekabidhi viatu vya ngozi jozi 500 kwa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao yenye kauli mbiu “Samia nivike viatu”. Aidha, makabidhiano ya viatu hivyo yamefanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam. Akielezea historia ya kiwanda Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Mathias John amesema, Kiwanda cha  viatu na bidhaa za ngozi SUMAJKT Shoes and Leather Product Co. LTD Kilianzishwa Jul 2017 na majukumu yake yakiwa ni uzalishaji wa viatu na bidhaa mbalimbali za ngozi.  Aidha, toka kuanzishwa Kqa  kiwanda hicho kimeendelea kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa kununua vifaa na mashine za kisasa ili kuzalisha bidhaa zenye ubora.  Bidhaa zinazozalishwa ni viatu kwa ajili ya taasisi za ulinzi, viatu vya usalama (safety boots), viatu vya maofisini na viatu vya shule.  Uwezo wa kiwanda ni kuzalisha viatu jozi 500 kwa siku na Kup

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA MIRADI YA UJENZI KANDA YA ZIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata leo tarehe 28 Oktoba 22 amefanya ziara katika miradi ya ujenzi inayoendelea kujengwa kanda ya ziwa. Kanali Petro Ngata amekagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Ziwa ambayo ni mradi wa ujenzi wa jengo la uchunguzi (Dignostic Center) katika hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama , Mradi wa uondoaji wa kifusi eneo la hanga uwanja wa ndege wa Chato Mkoani Geita na Mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Msalala. Aidha, Kanali Ngata  amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuhusu ukamilishwaji wa  jengo la ofisi za Halmashauri. SUMAJKT imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali ya ujenzi nchini kupitia kampuni yake ya ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited ambayo ina kanda saba za ujenzi.

MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA ZIARA MAFINGA MKOANI IRINGA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amehitimisha Ziara yake kwa kutembelea Kikosi cha JKT Mafinga Mkoani Iringa ambapo SUMAJKT katika kikosi hicho imewekeza katika ufugaji wa mifugo mbali mbali ikiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe. Bonyeza video hiyo kuona yaliyojiri.