Skip to main content

Posts

Showing posts with the label Ziara

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA MIRADI YA UJENZI KANDA YA ZIWA

  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata ameendelea na ziara katika miradi mbali mbali ya ujenzi inayoendelea kujengwa na Kampuni ya ujenzi “SUMAJKT Construction Company Limited kupitia SUMAJKT Ujenzi kanda ya ziwa. Kanali Petro Ngata katika ziara hiyo iliyoanza tarehe 28 hadi 30 Oktoba 2022 amekagua miradi mingine  inayotekelezwa na SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Ziwa ambayo ni mradi wa Ujenzi wa hanga la Askari, Jengo la kuhifadhia maiti "Mortuary" na Jengo la wodi ya Wagonjwa Maalumu "VIP Ward" katika Hospitali ya Kijeshi Ilemela- Mwanza,   ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Kanda ya Ziwa lililopo Busweli-Ilemela Jijini Mwanza na kuagiza SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Ziwa iongeze kasi ya ujenzi ili ikamilishe mradi huo kwa wakati. Aidha Kanali Petro Ngata amepongeza maendeleo ya utekelezaji wa Miradi hiyo na kuagiza SUMAJKT Ujenzi Kanda ya ziwa kukamilisha Ujenzi wa hanga  la Askari pamoja na c

MHESHIMIWA BASHUNGWA ALIPONGEZA JKT

  Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe. Innocent Bashungwa amelipongeza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kwa kuendelea kutekeleza jukumu la malezi ya Vijana kupitia mafunzo yao ya Kujitolea na Mujibu wa Sheria yanayotolewa kwenye makambi ya JKT ili kuwajengea uzalendo pamoja na stadi za kazi na waweze kushiriki ujenzi wa Taifa. Mhe. Bashungwa amesema hayo alipofanya ziara ya kikazi iliyolenga kujitambulisha, Makao Mkuu ya JKT Chamwino, Jijini Dodoma ambapo alipata fursa ya kuongea na Maafisa, Askari, Vijana na Watumishi wa Umma wanaofanyia kazi JKT eneo la Dodoma. Mhe. Bashungwa ameongeza kuwa, Kukamilika kwa miradi ya Kilimo cha kimkakati katika shamba la SUMAJKT lililopo Mngeta na Ujenzi wa miundombinu ya Skimu ya Umwagiliaji iliyopo katika kikosi cha Chita JKT mkoani Morogoro, Italeta tija katika upatikanaji wa chakula cha kutosha na kulihakikishia Taifa Usalama wa Chakula pamoja na upatikanaji wa Mbegu bora. Ameongeza kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita imetenga bajeti ya fedha kupitia Wizara ya U

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA KANDA YA UJENZI YA NYANDA ZA JUU KUSINI

Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) linatarajia kuanzisha  Kikosi  kazi  cha ujenzi wa barabara za lami ,  Ambacho kitafanya kazi sehemu mbali mbali nchini. Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali  Petro Ngata A amezungumza hayo tarehe 02 Agosti 2022, alipofanya ziara katika kanda ya ujenzi ya nyanda za juu kusini jijini Mbeya.