Skip to main content

Posts

Showing posts from July, 2022

DC MTATIRO AZINDUA SHAMBA LA KOROSHO LA SUMAJKT TUNDUMA

 

KARIBU SUMAJKT LEATHER PRODUCTS KWA BIDHAA HALISI ZA NGOZI

 Kiwanda cha bidhaa za Ngozi SUMAJKT Leadher product kinazalisha bidhaa mbali mbali kwa kutumia ngozi halisi ikiwemo mikoba ya aina mbali mbali, mikanda, viatu vya aina tofauti yani buti kwa ajili ya makampuni ya ulinzi, viatu vya shule, viatu Vya ofisini kwa jinsia zote, tizama video hiyo uweze kuviona . karibu

PONGEZI KWA MKUU WA JKT NA SUMAJKT-DC MTATIRO

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Julius Mtatiro, ameahidi kuongeza mikakati ya uwekezaji katika shamba la kilimo cha korosho na ufugaji wa ng'ombe,  mbuzi na kuku linalomikiwa na Shirika la Uzalishaji  Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) katika Wilaya ya Tunduru. Mhe. Mtatiro, amezungumza hayo leo tarehe 22 Julai 2022, alipokuwa akizindua shamba hilo lililopo katika kijiji cha Nanjoka, Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma. Katika uzinduzi huo Mhe. Julius Mtatiro, ametoa pongezi kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele na pia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Petro Ngata kwa kazi kubwa  ambayo wamedhamiria kwenye wilaya ya Tunduru.  "Naishukuru SUMAJKT kwa kulichagua eneo hili kuendesha shughuli za kilimo pamoja ufugaji, ambazo zitakuza uchumi na kuzalisha ajira kwa wingi katika maeneo yetu mbalimbali ", alisema Mhe. Mtatiro.  Mhe. Julius Mtatiro, amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tunduru Bw.

ZINGATIENI UBORA KATIKA MIRADI YA UJENZI-KANALI NGATA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amekagua Miradi tisa ya ujenzi jijini Dodoma inayojengwa na SUMAJKT Construction Company Ltd, kupitia Kanda mbali mbali. Kanali Petro Ngata, amefanya ziara hiyo jana tarehe 22 Julai 2022 alipotembelea  miradi mbali mbali ya ujenzi katika mji wa serikali Mtumba , Shule ya Mfano Iyumbu pamoja ukaguzi wa mitambo katika kiwanda cha mabati SUMAJKT Roofing Company Limited kilichopo Dodoma. Pia amekagua maendeleo ya Ujenzi wa jengo la wizara ya Katiba na Sheria, unaotekelezwa na SUMAJKT Construction Company Limited Ujenzi kanda ya Mashariki,    Pia amekagua Ujenzi wa jengo la Mwanasheria Mkuu wa Serikali unaotekelezwa na  SUMAJKT ujenzi Kanda ya Kati Dodoma, Ujenzi wa Jengo la Wakili Mkuu wa Serikali  unaotekelezwa na SUMAJKT  Makao Makuu, Ujenzi wa Jengo la Wakala wa Mtandao wa Serikali, Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya waziri mkuu, jengo la  Sera,  Ujenzi wa jengo la ofisi ya Waziri Mkuu jen