MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA) KUTOA MILIONI ISHIRINI NA TISA KUKARABATI MADARASA JITEGEMEE SEKONDARI
Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndugu Alphayo Kidato ameahidi kutoa kiasi cha milioni ishirini na tisa za kitanzania kwa ajili yakukarabati Madarasa pamoja na Mabweni ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT iliyopo Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam. Ahadi hiyo imetolewa leo tarehe 29 Octoba 2022 na Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania ndugu Richard Kayombo kwa niaba ya Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ndugu Alphayo Kidato aliyemwakilisha katika mahafali hayo ya 38 ya kidato cha nne 2022. Kayombo alitoa shukrani za pongezi kwa uongozi wa shule ya Jitegemee kwa kuona umuhimu wa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwa sehemu ya familia ya Jitegemee katika mahafali ya 38 ya wanafunzi wa kidato cha nne. Pia Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndugu Richard Kayombo amewasihi wahitimu na wanafunzi wengine kuhakikisha wanaongeza nidhamu katika masomo ili w