Skip to main content

Posts

Showing posts with the label SUMAJKT Construction Company Ltd

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMEAGA KAYA ZINGINE 25 NGORO NGORO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameaga kaya zingine 25, zenye watu 105, na amesema mpaka kufikia tarehe 18/8/2022,  jumla ya kaya 1,002 zenye watu 5,382 zimejiandikisha kwa hiari kuhama katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro na kuelekea kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoa wa Tanga,  lililotengwa na serikali kwa ajili ya wakazi hao. Kati ya kaya hizo,  tayari kaya 624 zenye watu 3,323 zimehakikiwa na kufanyiwa uthamini na kati ya kaya hizo, kaya 106 zenye watu 536 zimeshahamia kijiji cha Msomera wilayani Handeni Mkoani Tanga. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hayo Agosti 19,2022 Mkoani Arusha sambamba na zoezi la kukabidhi hundi ya Malipo kwa wakazi wapya wa Msomera. Hafla fupi ilifanyika kwenye ofisi za mamlaka ya hifadhi  hiyo kwa nia ya kufanikisha hatua hiyo. Aidha , Mhe. Kassim Majaliwa ameeleza kuwa, Rais Samia Suluhu Hassan amepongeza uamuzi wa wananchi hao na kwamba serikali itaendelea kuwekeza katika kuboresha miundombinu ya eneo la Msomera.  “Napenda k...

ZINGATIENI UBORA KATIKA MIRADI YA UJENZI-KANALI NGATA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amekagua Miradi tisa ya ujenzi jijini Dodoma inayojengwa na SUMAJKT Construction Company Ltd, kupitia Kanda mbali mbali. Kanali Petro Ngata, amefanya ziara hiyo jana tarehe 22 Julai 2022 alipotembelea  miradi mbali mbali ya ujenzi katika mji wa serikali Mtumba , Shule ya Mfano Iyumbu pamoja ukaguzi wa mitambo katika kiwanda cha mabati SUMAJKT Roofing Company Limited kilichopo Dodoma. Pia amekagua maendeleo ya Ujenzi wa jengo la wizara ya Katiba na Sheria, unaotekelezwa na SUMAJKT Construction Company Limited Ujenzi kanda ya Mashariki,    Pia amekagua Ujenzi wa jengo la Mwanasheria Mkuu wa Serikali unaotekelezwa na  SUMAJKT ujenzi Kanda ya Kati Dodoma, Ujenzi wa Jengo la Wakili Mkuu wa Serikali  unaotekelezwa na SUMAJKT  Makao Makuu, Ujenzi wa Jengo la Wakala wa Mtandao wa Serikali, Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya waziri mkuu, jengo la  Sera,  Ujen...