Skip to main content

Posts

Showing posts with the label SUMAJKT na jamii

SUMAJKT YAKABIDHI HUNDI KUSAIDIA KUTANGAZA LUGHA YA KISWAHILI

Kaimu naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT), Kanali Shija Lupi amekabidhi hundi ya zaidi ya Milioni moja na laki nane (1,800,000/=) kwa Bwana Issack Kalumba ambaye anaendesha baiskeli katika nchi mbalimbali Barani Afrika kwa lengo la kuinua na kutangaza lugha ya kiswahili pamoja na utalii wa Tanzania kupitia majukwaa rasmi katika nchi hizo. Kanali Lupi alikabidhi hundi hiyo kwa Bwana Kalumba tarehe 04 March 2022 ofisini kwake Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa jijini Dar es salaam. SUMAJKT imetoa hundi ya kiasi hicho cha pesa kuunga mkono juhudi za Bwana Isaack Kalumba  ambaye alileta maombi SUMAJKT la kusaidiwa fedha hizo ili kuweza kutatua baadhi ya changamoto anazokutana nazo katika mzunguko wa Safari yake ya kuinua na kutangaza lugha ya kiswahili Barani Afrika. Bwana Isaack Kalumba ni Mtanzania anaeendesha baiskeli katika nchi mbalimbali Barani Afrika kwa lengo la kuinua na kuitangaza lugha ya kiswahili Afrika na kuunga mkono juhu