Skip to main content

Posts

Showing posts with the label SUMAJKT Kilimo

PONGEZI KWA MKUU WA JKT NA SUMAJKT-DC MTATIRO

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Julius Mtatiro, ameahidi kuongeza mikakati ya uwekezaji katika shamba la kilimo cha korosho na ufugaji wa ng'ombe,  mbuzi na kuku linalomikiwa na Shirika la Uzalishaji  Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) katika Wilaya ya Tunduru. Mhe. Mtatiro, amezungumza hayo leo tarehe 22 Julai 2022, alipokuwa akizindua shamba hilo lililopo katika kijiji cha Nanjoka, Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma. Katika uzinduzi huo Mhe. Julius Mtatiro, ametoa pongezi kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele na pia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Petro Ngata kwa kazi kubwa  ambayo wamedhamiria kwenye wilaya ya Tunduru.  "Naishukuru SUMAJKT kwa kulichagua eneo hili kuendesha shughuli za kilimo pamoja ufugaji, ambazo zitakuza uchumi na kuzalisha ajira kwa wingi katika maeneo yetu mbalimbali ", alisema Mhe. Mtatiro.  Mhe. Julius Mtatiro, amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tunduru Bw.