Skip to main content

Posts

MRADI WA UJENZI MTUMBA KUKAMILIKA KWA WAKATI-KANALI PETRO NGATA

Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Petro Ngata amesema mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Serikali katika mji wa Mtumba unaotekelezwa na kampuni  tanzu ya Ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited (SCCL) utakamilika kwa wakati uliopangwa. Kanali Petro Ngata amesema hayo jana (Jumatatu, Septemba 5, 2022) wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipofika kukagua maendeleo ujenzi wa Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.  "Mheshimiwa Waziri Mkuu ameridhishwa sana na kazi tunazozifanya hapa katika mji wa serikali Sisi  SUMAJKT tunatekeleza miradi idadi tisa kwa maana ya majengo ya wizara na yote yapo katika hatua nzuri na tunakwenda na wakati kulingana na mkataba ulivyo.  Na sisi kama SUMAJKT kwa kuzingatia maelekezo aliyoyatoa Mheshimiwa Waziri Mkuu siku hii ya leo tumejipanga kuhakikisha kwamba tunakamilisha hili jukumu katika muda aliopanga Mheshimiwa Waziri Mkuu."alisema Kanali Ngata.   Nae Meneja wa Ujenzi SUMAJKT-Kanda ya Magharibi Kanali Mbaraka Magogo amesema kuwa mr

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMEAGA KAYA ZINGINE 25 NGORO NGORO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameaga kaya zingine 25, zenye watu 105, na amesema mpaka kufikia tarehe 18/8/2022,  jumla ya kaya 1,002 zenye watu 5,382 zimejiandikisha kwa hiari kuhama katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro na kuelekea kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoa wa Tanga,  lililotengwa na serikali kwa ajili ya wakazi hao. Kati ya kaya hizo,  tayari kaya 624 zenye watu 3,323 zimehakikiwa na kufanyiwa uthamini na kati ya kaya hizo, kaya 106 zenye watu 536 zimeshahamia kijiji cha Msomera wilayani Handeni Mkoani Tanga. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hayo Agosti 19,2022 Mkoani Arusha sambamba na zoezi la kukabidhi hundi ya Malipo kwa wakazi wapya wa Msomera. Hafla fupi ilifanyika kwenye ofisi za mamlaka ya hifadhi  hiyo kwa nia ya kufanikisha hatua hiyo. Aidha , Mhe. Kassim Majaliwa ameeleza kuwa, Rais Samia Suluhu Hassan amepongeza uamuzi wa wananchi hao na kwamba serikali itaendelea kuwekeza katika kuboresha miundombinu ya eneo la Msomera.  “Napenda kumhakikishia Mheshimiwa

FANYIENI UTAFITI MAZAO YA NGANO NA ALIZETI - KANALI NGATA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, ametoa maagizo kwa Meneja wa shamba la SUMAJKT Bassotu Sajinitaji Bahati Kidenya, kufanya utafiti mzuri wa mazao ya ngano na alizeti ili shirika likiamua kuwekeza katika kilimo hicho kiwe na tija. Kanali Petro Ngata, ametoa maagizo  hayo leo tarehe  12 Augosti 2022, alipokuwa katika ziara ya kukagua shamba hilo lililopo katika kijiji cha Bassotu , Wilaya ya Hanang'i Mkoani Manyara.  Kanali Ngata ameongeza kuwa  Bassotu kuna faida kubwa endapo SUMAJKT itafanikiwa kupata eneo kubwa na kuanza na aina ya mazao mawili ambayo ni ngano na katamu (alizeti za miba). "Ngano na katamu ni mazao ambayo tukizalisha tutakuwa na uhakika wa kupata faida" ameeleza Kanali Ngata.  Aidha, Kanali Petro Ngata,  ameeleza kuwa shirika litaanza kuliwekea mipango mizuri na ya haraka shamba hilo, endapo msajili wa hazina atakubali kutoa eneo kwa SUMAJKT.      Kwa upande wa Meneja wa mradi wa sh

IJUE SIRI YA MAFANIKIO YA JKT KATIKA KILIMO

MKUU wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema pamoja na kuwa na mabadiliko ya tabia nchi lakini bado katika vipando vya Jeshi la kujenga taifa na mashamba yake kwa  na vikosi yameendelea kufanya vizuri na mazao yanastawi kwa jinsi ambavyo walikuwa wametalajia. Amesema kuwa wao walishaona changamoto hizo za mabadiliko  ya tabia nchi hivyo walishaanza kufanya mawasiliano na mamlaka ya hali ya hewa ambapo walikuwa wanapewa taarifa juu ya mabadiliko hayo hususani kwenye eneo la mvua kwamba msimu huo mvua zitawahi ama kuchelewa na kama zitawahi zitakuja kwa viwango vidogo. Amesema kuwa baada ya kupata taarifa hiyo wao kama Jeshi la kujenga taifa walikaa chinin nakuweza kujipanga na kuona aina ya mbegu ambazo zitaweza kuendana na hali ya hewa. Brigedia Mabena ameyasema hayo Agosti 7 kwenye maonyesho ya nanenane ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Mbeya wakati alipotembelea banda la JKT pamoja na mambo mengine amesema kuwa katika kikosi cha 847 KJ ni Milundikwa nakwamba pa

MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA ZIARA MAFINGA MKOANI IRINGA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amehitimisha Ziara yake kwa kutembelea Kikosi cha JKT Mafinga Mkoani Iringa ambapo SUMAJKT katika kikosi hicho imewekeza katika ufugaji wa mifugo mbali mbali ikiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe. Bonyeza video hiyo kuona yaliyojiri.

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA KANDA YA UJENZI YA NYANDA ZA JUU KUSINI

Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) linatarajia kuanzisha  Kikosi  kazi  cha ujenzi wa barabara za lami ,  Ambacho kitafanya kazi sehemu mbali mbali nchini. Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali  Petro Ngata A amezungumza hayo tarehe 02 Agosti 2022, alipofanya ziara katika kanda ya ujenzi ya nyanda za juu kusini jijini Mbeya.

JKT KUENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO ZA UPATIKANAJI WA MAFUTA YA KULA NCHINI

 Mkurugezi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa( SUMAJKT), Kanali Petro Ngata amesema Jeshi la Kujenga Taifa litaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa mafuta ya kula hapa nchini. Ameyasema hayo wakati alipotembelea Banda la JKT katika Maonesho ya Waku- lima,Wafugaji na Wavuvi (Nanenane) yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale, Uyole Jijini Mbeya. Kanali Ngata amefafanua kuwa, JKT limeanza kutekeleza Kilimo cha Mazao ya Kimkakati ikiwemo zao la Alizeti kwa kutumia mashamba yake makubwa katika maeneo ambayo zao hilo linastawi. "Tumeanza na Mkakati wa Kulima kwa wingi mazao ya kimkakati, na hatua inayofuata ni kuchakata zao hilo na kupata mafuta ya Kula". Amesema Kanali Ngata Akizungumzia namna JKT mashamba darasa ya JKT yalivyo na Manufaa, Kanali Ngata amesema JKT lina wataalamu wa kutosha waliobobea katika kutoa elimu bora ya Uzalishaji wa Mazao ya kilimo, Mifugo na Uvuvi hivyo amewataka

ZIARA YA KAMATI YA UTENDAJI SUMAJKT (KUS) KATIKA UJENZI WA MJI WA SERIKALI MTUMBA.

 Mkurugenzi wa fedha wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Luteni Kanali Godfrey Kipingu, ameipongeza Kampuni ya Ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited kwa hatua ya ujenzi wa majengo mbali mbali ya serikali yanayoendelea kujengwa jijini Dodoma. Luteni Kanali Kipingu ametoa pongezi hizo tarehe 01 Agosti 2022, akiwa na Kamati ya Utendaji ya SUMAJKT (KUS) katika ziara ya Shule ya mfano iliyopo Iyumbu pamoja na majengo nane ya serikali yanayoendelea kujengwa katika mji wa serikali Mtumba Dodoma.

DC MTATIRO AZINDUA SHAMBA LA KOROSHO LA SUMAJKT TUNDUMA

 

KARIBU SUMAJKT LEATHER PRODUCTS KWA BIDHAA HALISI ZA NGOZI

 Kiwanda cha bidhaa za Ngozi SUMAJKT Leadher product kinazalisha bidhaa mbali mbali kwa kutumia ngozi halisi ikiwemo mikoba ya aina mbali mbali, mikanda, viatu vya aina tofauti yani buti kwa ajili ya makampuni ya ulinzi, viatu vya shule, viatu Vya ofisini kwa jinsia zote, tizama video hiyo uweze kuviona . karibu

PONGEZI KWA MKUU WA JKT NA SUMAJKT-DC MTATIRO

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Julius Mtatiro, ameahidi kuongeza mikakati ya uwekezaji katika shamba la kilimo cha korosho na ufugaji wa ng'ombe,  mbuzi na kuku linalomikiwa na Shirika la Uzalishaji  Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) katika Wilaya ya Tunduru. Mhe. Mtatiro, amezungumza hayo leo tarehe 22 Julai 2022, alipokuwa akizindua shamba hilo lililopo katika kijiji cha Nanjoka, Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma. Katika uzinduzi huo Mhe. Julius Mtatiro, ametoa pongezi kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele na pia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Petro Ngata kwa kazi kubwa  ambayo wamedhamiria kwenye wilaya ya Tunduru.  "Naishukuru SUMAJKT kwa kulichagua eneo hili kuendesha shughuli za kilimo pamoja ufugaji, ambazo zitakuza uchumi na kuzalisha ajira kwa wingi katika maeneo yetu mbalimbali ", alisema Mhe. Mtatiro.  Mhe. Julius Mtatiro, amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tunduru Bw.

ZINGATIENI UBORA KATIKA MIRADI YA UJENZI-KANALI NGATA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amekagua Miradi tisa ya ujenzi jijini Dodoma inayojengwa na SUMAJKT Construction Company Ltd, kupitia Kanda mbali mbali. Kanali Petro Ngata, amefanya ziara hiyo jana tarehe 22 Julai 2022 alipotembelea  miradi mbali mbali ya ujenzi katika mji wa serikali Mtumba , Shule ya Mfano Iyumbu pamoja ukaguzi wa mitambo katika kiwanda cha mabati SUMAJKT Roofing Company Limited kilichopo Dodoma. Pia amekagua maendeleo ya Ujenzi wa jengo la wizara ya Katiba na Sheria, unaotekelezwa na SUMAJKT Construction Company Limited Ujenzi kanda ya Mashariki,    Pia amekagua Ujenzi wa jengo la Mwanasheria Mkuu wa Serikali unaotekelezwa na  SUMAJKT ujenzi Kanda ya Kati Dodoma, Ujenzi wa Jengo la Wakili Mkuu wa Serikali  unaotekelezwa na SUMAJKT  Makao Makuu, Ujenzi wa Jengo la Wakala wa Mtandao wa Serikali, Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya waziri mkuu, jengo la  Sera,  Ujenzi wa jengo la ofisi ya Waziri Mkuu jen

WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2022 AWAMU YA PILI

  JESHI la Kujenga Taifa (JKT), tunatoa siku tatu kwa vijana walioitwa kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2022, ambao hawajaripoti mpaka sasa kuripoti makambi waliyopangiwa ya JKT mara moja. Pia tumetoa nyongeza ya majina ya vijana waliohitimu elimu ya kidato cha sita mwaka 2022 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2022. Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali, Hassan Mabena anatoa wito kwa vijana waliochaguliwa wa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria mwaka 2022 Awamu ya Pili ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi wiki ijayo na yataendeshwa kwa muda wa miezi mitatu.  Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele anawataka kuripoti makambini vijana wote walioitwa kuhudhuria Mafunzo ya JKT Kwa Mujibu wa Sheria kwa mwaka 2022, ambao hawajaripoti mpaka sasa mripoti makambi ya JKT mara moja. Vijana  waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti makambi ya JKT yaliyo karibu na maeneo wanayoishi. "Vijana wote waliochaguliwa  

SUMAJKT YAKABIDHIWA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA JAMII YA WAKAZI KUTOKA NGORO NGORO

Taasisi ya Hifadhi ya Ngorongoro ( Ngoro ngoro Conservation Area Authority ( NCAA)  imekabidhi Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga  Taifa ( SUMAJKT) Mradi wa Ujenzi wa nyumba 400 eneo la  Msomela mkoani Tanga kwa  ajili ya Makazi ya jamii ya kimasai kutoka  Ngorongoro mkoani Arusha. Akikabidhiwa Mradi huo tarehe 21 Juni 2022, Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT kanali Petro Ngata amesema kuwa, SUMAJKT ipo tayari kukamilisha kazi hiyo kwa wakati  na kwa ufanisi.                                       "Shirika hili limekuwa likipokea kazi mpya na zilizoshindwa na kampuni nyingine  na kuzikamilisha kwa weledi wa hali ya juu"alisema Kanali Ngata. Nae Mhandisi Joshua Mwankunda kutoka NCAA amesema tayari wamekwisha kamilisha mahitaji muhimu ya awali ikiwemo Michoro, Barabara, Shule, mipaka pamoja na njia za mawasiliano. Mhandisi Joshua ameeleza kuwa tathmini ya mradi huo inaonesha Utagharimu Fedha za Kitanzania Shilingi Bilioni Tisa(9). "Tunaimani kubwa na SUMAJKT kwa ute

KWA MAHITAJI YA OFISI ZA KISASA NA KUMBI KARIBU SUMAJKT HOUSE

SHIRIKA la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) linapangisha  jengo la kisasa ambalo  Limegharimu zaidi ya Bilioni mbili (2) katika kuhakikisha kuwa linafikia viwango vya kisasa. Jengo hilo la kitega uchumi lenye ghorofa tano katika jiji la Dodoma litachangia kasi ya ukuaji wa uchumi nchini. Jengo hilo lijulikanalo kama ‘SUMAJKT HOUSE ’ , lililopo  eneo la Ipagala Mashariki katika kiwanja namba 130 jijini Dodoma, barabara kuu kutoka jijini Dar es Salaam, lina baadhi ya ofisi zitazopangishwa kwa Taasisi mbalimbali ikiwemo Benki, Mashirika na watu binafsi kwa matumizi ya kiofisi. Ghorofa  ya chini na Mezza nine katika jengo hilo itakuwa maalumu kwa ajili ya kupangisha Benki mbalimbali zitakazokuwa na uhitaji, ambapo miundo mbinu yake imejengwa kwa kuzingatia  Ghorofa ya kwanza itatumiwa kwa ofisi za SUMAJKT .  Ghorofa ya pili na ya tatu itakuwa na ofisi zitakazopangwishwa kwa wahitaji. Aidha, ghorofa ya nne itatumika kwa ukumbi kwa matumizi mbalimbali kama mikutano, shereh