Skip to main content

MRADI WA UJENZI MTUMBA KUKAMILIKA KWA WAKATI-KANALI PETRO NGATA



Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Petro Ngata amesema mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Serikali katika mji wa Mtumba unaotekelezwa na kampuni 

tanzu ya Ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited (SCCL) utakamilika kwa wakati uliopangwa. Kanali Petro Ngata amesema hayo jana (Jumatatu, Septemba 5, 2022) wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipofika kukagua maendeleo ujenzi wa Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.

 "Mheshimiwa Waziri Mkuu ameridhishwa sana na kazi tunazozifanya hapa katika mji wa serikali Sisi 
SUMAJKT tunatekeleza miradi idadi tisa kwa maana ya majengo ya wizara na yote yapo katika hatua nzuri na tunakwenda na wakati kulingana na mkataba ulivyo. 


Na sisi kama SUMAJKT kwa kuzingatia maelekezo aliyoyatoa Mheshimiwa Waziri Mkuu siku hii ya leo tumejipanga kuhakikisha kwamba tunakamilisha hili jukumu katika muda aliopanga Mheshimiwa Waziri Mkuu."alisema Kanali Ngata. 


 Nae Meneja wa Ujenzi SUMAJKT-Kanda ya Magharibi Kanali Mbaraka Magogo amesema kuwa mradi huo umefikia asilimia 46 na upo ndani ya muda wa mkataba. Aidha, Kanali Magogo amesema kuwa
kazi hizo wanatarajia kuzikamilisha tarehe 9 Septemba 22. Nae Meneja wa Ujenzi SUMAJKT Kanda ya Kati Meja Samwel Jambo amesema " Malengo ifikapo mwezi Novemba mwaka huu ujenzi wa jengo kwa ujumla tuanze kazi ya finishing, ambayo inahusisha 
plasta pamoja na kazi zingine zote za finishing, kwa hiyo tunatarajia miezi kumi ijayo baada ya kukamilisha tutakuwa tunapambana na umaliziaji. 

 Vile vile Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni hiyo ya Ujenzi SCCL Mhandisi Morgan Nyonyi ameahidi kuwa wao kama Wakandarasi daraja la kwanza katika mradi huo watatekeleza maelekezo yaliyotolewa na Mhe Waziri Mkuu na sambamba na ujenzi wa majengo hayo. Miradi yote ya ujenzi inayotekelezwa na SUMAJKT inagharimu Tsh bilioni 150.


 

Comments

Popular posts from this blog

SUMAJKT YAKABIDHI VIATU VYA SHULE JOZI 500

 Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kupitia Kampuni tanzu iitwayo SUMAJKT shoes and leather Products Co LTD. tarehe 04 Novemba 2022 limekabidhi viatu vya ngozi jozi 500 kwa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao yenye kauli mbiu “Samia nivike viatu”. Aidha, makabidhiano ya viatu hivyo yamefanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam. Akielezea historia ya kiwanda Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Mathias John amesema, Kiwanda cha  viatu na bidhaa za ngozi SUMAJKT Shoes and Leather Product Co. LTD Kilianzishwa Jul 2017 na majukumu yake yakiwa ni uzalishaji wa viatu na bidhaa mbalimbali za ngozi.  Aidha, toka kuanzishwa Kqa  kiwanda hicho kimeendelea kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa kununua vifaa na mashine za kisasa ili kuzalisha bidhaa zenye ubora.  Bidhaa zinazozalishwa ni viatu kwa ajili ya taasisi za ulinzi, viatu vya usalama (safety boots), viatu vya maofisini na viatu vya shule.  Uwezo wa kiwanda ni kuzalisha viatu jozi 500 kwa siku na Kup

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA MIRADI YA UJENZI KANDA YA ZIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata leo tarehe 28 Oktoba 22 amefanya ziara katika miradi ya ujenzi inayoendelea kujengwa kanda ya ziwa. Kanali Petro Ngata amekagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Ziwa ambayo ni mradi wa ujenzi wa jengo la uchunguzi (Dignostic Center) katika hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama , Mradi wa uondoaji wa kifusi eneo la hanga uwanja wa ndege wa Chato Mkoani Geita na Mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Msalala. Aidha, Kanali Ngata  amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuhusu ukamilishwaji wa  jengo la ofisi za Halmashauri. SUMAJKT imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali ya ujenzi nchini kupitia kampuni yake ya ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited ambayo ina kanda saba za ujenzi.

MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA ZIARA MAFINGA MKOANI IRINGA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amehitimisha Ziara yake kwa kutembelea Kikosi cha JKT Mafinga Mkoani Iringa ambapo SUMAJKT katika kikosi hicho imewekeza katika ufugaji wa mifugo mbali mbali ikiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe. Bonyeza video hiyo kuona yaliyojiri.