Skip to main content

IJUE SIRI YA MAFANIKIO YA JKT KATIKA KILIMO


MKUU wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema pamoja na kuwa na mabadiliko ya tabia nchi lakini bado katika vipando vya Jeshi la kujenga taifa na mashamba yake kwa  na vikosi yameendelea kufanya vizuri na mazao yanastawi kwa jinsi ambavyo walikuwa wametalajia.

Amesema kuwa wao walishaona changamoto hizo za mabadiliko  ya tabia nchi hivyo walishaanza kufanya mawasiliano na mamlaka ya hali ya hewa ambapo walikuwa wanapewa taarifa juu ya mabadiliko hayo hususani kwenye eneo la mvua kwamba msimu huo mvua zitawahi ama kuchelewa na kama zitawahi zitakuja kwa viwango vidogo.

Amesema kuwa baada ya kupata taarifa hiyo wao kama Jeshi la kujenga taifa walikaa chinin nakuweza kujipanga na kuona aina ya mbegu ambazo zitaweza kuendana na hali ya hewa.

Brigedia Mabena ameyasema hayo Agosti 7 kwenye maonyesho ya nanenane ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Mbeya wakati alipotembelea banda la JKT pamoja na mambo mengine amesema kuwa katika kikosi cha 847 KJ ni Milundikwa nakwamba pale kikosini wamefanikiwa kwani wameweza kufikia  waliyokusudia.

Ameongeza kuwa baada ya kuwasiliana na mamlaka ya hali ya hewa waliweza kulima mapema ,kupanda mapema mbegu ambazo ziliweza kuhimili ukame kwa hali hiyo jeshi la kujenga taifa wakawa wamefanikiwa lakini la pili niwamba wanataka kuondokana na kilimo cha kutegemea mvua hivyo jeshi hilo limekuja na mkakati wa kilimo cha umwagiliaji wameaza katika kikosi cha 837kj ni chita tayari sikimu ya umwagiliaji imeshafikia asilimia 80 za hakeri 2500 na mpango ni kuhakikisha kwamba hekari 12000 zilizopo pale zitajengewa sikimu ya umwagiliaji.


Amefafanu kwa kufanya hivyo watakuwa wanauhaki wa kile wanachokilima na wanachokivuna na katika takwimu wanazozipata kwenye mamlaka zinaonyesha kuwa kumekuwa na uhaba wa mvua kutokana na mabadiliko ya tabia nchi hivyo wao kama jeshi la kujenga taifa wanatoa rai kwa wakulima wadogo,wakulima wakati na wakulima wakubwa kuhifadhi chakula walichokipata.


"Jeshi la kujenga taifa tunahakikisha chakula tulichokipata kwa msimu huu tunaaza  kwaza kuwalisha vijana wetu na kile kilichobaki ndio tunapeleka kwa jamii ili kuhakikisha tunakabiliana na hili balaa la njaa lakini hali si mbaya sana cha msingi ni kuhakikisha chakula kinachopatikana kisiuzwe nje ya nchi."amesema Brigedia Mabena 


Nakuongeza kuwa "Changamoto iliyojitokeza imeweza kutoa fursa kwao kama jeshi kuwasiliana na mamlaka ya hali ya hewa kuhakikisha kwamba wanapewa elimu kwamba msimu ujao hali itakuwaje na pili kuhakikuisha kwamba wanaaza kwenda kwenye kilimo cha umwagiliaji kwasababu nchi yetu imebalikiwa ina mito ina mabwawa,ina maziwa hivyo kuna teknolojia ambayo haitahi gharama nyingi kwani ukipata pamp na mipira kwa ajili ya umwagiliaji unaweza kumwagilia mashamba yaliyopo karibu na mito au maziwa .




Amesema kuwa jeshi hilo kwa kushirikia na taasisi zingine ikiwemo Wizara ya kilimo kwa pamoja wanahakikisha wanapata mbegu bora na wanakwenda kuongeza kilimo cha umwagiliaji na mashamba mengi yanafikiwa na yanadhalishwa kwa ubora.


"Jeshi la kujenga taifa limeaza kuboresha shamba letu la michikichi lililopo kikosi 821  kigoma kwahiyo sasahivi wanalima na wamejipanga kulima hekari 200 na kuhakikisha kwamba tunakuza hili shamba kutokana na michikichi na pia kwaupande wa zao la alizeti kule lililopo Dodoma karibu na singida na vilevile mikoa mingine hivyo wanakuja mpango wa kuyaongeza mashamba na wanawasiliana na taasisi ya mbegu za kilimo TARI kushirikiana na watalamu waliopo katika Jeshi ili kupata kitu bora."amesema


kwa upande wake Mwenyekiti wa Maonyesho ya nanenane kitaifa JKT Kanali Shija Lupi amesema kuwa mwaka huu wanakwenda kwenye sensa ili kuangalia idadi ya watu waliopo Tanzania ambayo itachukuliwa katika mpango mzima wa kupanga mipango mizuri kwani ukingalia katika sekta ya kilimo uvuvi pamoja na shughuli zingine.


"Wito kwa watanzania nivema kushiriki zoezi la sensa ambalo linatarajia kufanya Agosti 23 ili serikali iweze kupanga vizuri shughuli za maendele hivyo nawasihi watanzania kushiriki kwani litaweza kutuvusha baada ya serikali kupanga mipango yake."amesema Kanali Lupi.

Comments

Popular posts from this blog

SUMAJKT YAKABIDHI VIATU VYA SHULE JOZI 500

 Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kupitia Kampuni tanzu iitwayo SUMAJKT shoes and leather Products Co LTD. tarehe 04 Novemba 2022 limekabidhi viatu vya ngozi jozi 500 kwa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao yenye kauli mbiu “Samia nivike viatu”. Aidha, makabidhiano ya viatu hivyo yamefanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam. Akielezea historia ya kiwanda Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Mathias John amesema, Kiwanda cha  viatu na bidhaa za ngozi SUMAJKT Shoes and Leather Product Co. LTD Kilianzishwa Jul 2017 na majukumu yake yakiwa ni uzalishaji wa viatu na bidhaa mbalimbali za ngozi.  Aidha, toka kuanzishwa Kqa  kiwanda hicho kimeendelea kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa kununua vifaa na mashine za kisasa ili kuzalisha bidhaa zenye ubora.  Bidhaa zinazozalishwa ni viatu kwa ajili ya taasisi za ulinzi, viatu vya usalama (safety boots), viatu vya maofisini na viatu vya shule.  Uwezo wa kiwanda ni kuzalisha viatu jozi 500 kwa siku na Kup

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA MIRADI YA UJENZI KANDA YA ZIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata leo tarehe 28 Oktoba 22 amefanya ziara katika miradi ya ujenzi inayoendelea kujengwa kanda ya ziwa. Kanali Petro Ngata amekagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Ziwa ambayo ni mradi wa ujenzi wa jengo la uchunguzi (Dignostic Center) katika hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama , Mradi wa uondoaji wa kifusi eneo la hanga uwanja wa ndege wa Chato Mkoani Geita na Mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Msalala. Aidha, Kanali Ngata  amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuhusu ukamilishwaji wa  jengo la ofisi za Halmashauri. SUMAJKT imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali ya ujenzi nchini kupitia kampuni yake ya ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited ambayo ina kanda saba za ujenzi.

MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA ZIARA MAFINGA MKOANI IRINGA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amehitimisha Ziara yake kwa kutembelea Kikosi cha JKT Mafinga Mkoani Iringa ambapo SUMAJKT katika kikosi hicho imewekeza katika ufugaji wa mifugo mbali mbali ikiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe. Bonyeza video hiyo kuona yaliyojiri.