Skip to main content

PONGEZI KWA MKUU WA JKT NA SUMAJKT-DC MTATIRO






Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Julius Mtatiro, ameahidi kuongeza mikakati ya uwekezaji katika shamba la kilimo cha korosho na ufugaji wa ng'ombe, 
mbuzi na kuku linalomikiwa na Shirika la Uzalishaji 
Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) katika Wilaya ya Tunduru.

Mhe. Mtatiro, amezungumza hayo leo tarehe 22 Julai 2022, alipokuwa akizindua shamba hilo lililopo katika kijiji cha Nanjoka, Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Katika uzinduzi huo Mhe. Julius Mtatiro, ametoa pongezi kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele na pia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Petro Ngata kwa kazi kubwa
 ambayo wamedhamiria kwenye wilaya ya Tunduru. 

"Naishukuru SUMAJKT kwa kulichagua eneo hili kuendesha shughuli za kilimo pamoja ufugaji, ambazo zitakuza uchumi na kuzalisha ajira kwa wingi katika maeneo yetu mbalimbali ", alisema Mhe. Mtatiro. 

Mhe. Julius Mtatiro, amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tunduru Bw. Chiza Marando, aendelee kukaa na wataalamu kuangalia maeneo ya mkakati yaliyotengwa kwa ajili ya kilimo cha "Block Farming" ili wapewe SUMAJKT. 

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Viwanda SUMAJKT  Meja Peter Kulyakwave, akimwakilisha  Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Petro Ngata, katika uzinduzi wa shamba hilo ameeleza kuwa Shirika linatekeleza mkakati wake wa kuongeza vyanzo vipya vya mapato na kuboresha huduma mbalimbali zikiwemo kilimo cha korosho, ufugaji wa ng'ombe kwa ajili ya kuwanenepesha na kuuza, mbuzi pamoja na kuku.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa SUMAJKT Port and Services Co. Limited, Meja Joseph Marwa, ameeleza kuwa Kampuni hiyo ilikabidhiwa shamba hilo la korosho lenye ukubwa wa hekari 2180 na Shirika la Uzalishaji Mali Ia Kujenga Taifa mnamo mwaka 2017 na 
iliweka mipango ya kuelendeleza shamba hilo kwa awamu, ambapo walianza kupanda mikorosho mipya idadi 3000, lengo likiwa   kuendeleza kupanda mikorosho mipya kufikia hekari 600.

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kupitia SUMAJKT lilianza kukalia eneo hilo mwaka 2019, ambapo Kampuni ya SUMAJKT Port and Services Co. Ltd. Ilikabidhiwa kuendesha shamba hilo.




 

Comments

Popular posts from this blog

SUMAJKT YAKABIDHI VIATU VYA SHULE JOZI 500

 Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kupitia Kampuni tanzu iitwayo SUMAJKT shoes and leather Products Co LTD. tarehe 04 Novemba 2022 limekabidhi viatu vya ngozi jozi 500 kwa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao yenye kauli mbiu “Samia nivike viatu”. Aidha, makabidhiano ya viatu hivyo yamefanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam. Akielezea historia ya kiwanda Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Mathias John amesema, Kiwanda cha  viatu na bidhaa za ngozi SUMAJKT Shoes and Leather Product Co. LTD Kilianzishwa Jul 2017 na majukumu yake yakiwa ni uzalishaji wa viatu na bidhaa mbalimbali za ngozi.  Aidha, toka kuanzishwa Kqa  kiwanda hicho kimeendelea kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa kununua vifaa na mashine za kisasa ili kuzalisha bidhaa zenye ubora.  Bidhaa zinazozalishwa ni viatu kwa ajili ya taasisi za ulinzi, viatu vya usalama (safety boots), viatu vya maofisini na viatu vya shule.  Uwezo wa kiwanda ni kuzalisha viatu jozi 500 kwa siku na Kup

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA MIRADI YA UJENZI KANDA YA ZIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata leo tarehe 28 Oktoba 22 amefanya ziara katika miradi ya ujenzi inayoendelea kujengwa kanda ya ziwa. Kanali Petro Ngata amekagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Ziwa ambayo ni mradi wa ujenzi wa jengo la uchunguzi (Dignostic Center) katika hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama , Mradi wa uondoaji wa kifusi eneo la hanga uwanja wa ndege wa Chato Mkoani Geita na Mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Msalala. Aidha, Kanali Ngata  amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuhusu ukamilishwaji wa  jengo la ofisi za Halmashauri. SUMAJKT imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali ya ujenzi nchini kupitia kampuni yake ya ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited ambayo ina kanda saba za ujenzi.

MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA ZIARA MAFINGA MKOANI IRINGA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amehitimisha Ziara yake kwa kutembelea Kikosi cha JKT Mafinga Mkoani Iringa ambapo SUMAJKT katika kikosi hicho imewekeza katika ufugaji wa mifugo mbali mbali ikiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe. Bonyeza video hiyo kuona yaliyojiri.