Mkurugenzi wa fedha wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Luteni Kanali Godfrey Kipingu, ameipongeza Kampuni ya Ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited kwa hatua ya ujenzi wa majengo mbali mbali ya serikali yanayoendelea kujengwa jijini Dodoma.
Luteni Kanali Kipingu ametoa pongezi hizo tarehe 01 Agosti 2022, akiwa na Kamati ya Utendaji ya SUMAJKT (KUS) katika ziara ya Shule ya mfano iliyopo Iyumbu pamoja na majengo nane ya serikali yanayoendelea kujengwa katika mji wa serikali Mtumba Dodoma.
Comments
Post a Comment