Skip to main content

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMEAGA KAYA ZINGINE 25 NGORO NGORO


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameaga kaya zingine 25, zenye watu 105, na amesema mpaka kufikia tarehe 18/8/2022,  jumla ya kaya 1,002 zenye watu 5,382 zimejiandikisha kwa hiari kuhama katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro na kuelekea kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoa wa Tanga,  lililotengwa na serikali kwa ajili ya wakazi hao.

Kati ya kaya hizo,  tayari kaya 624 zenye watu 3,323 zimehakikiwa na kufanyiwa uthamini na kati ya kaya hizo, kaya 106 zenye watu 536 zimeshahamia kijiji cha Msomera wilayani Handeni Mkoani Tanga.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hayo Agosti 19,2022 Mkoani Arusha sambamba na zoezi la kukabidhi hundi ya Malipo kwa wakazi wapya wa Msomera. Hafla fupi ilifanyika kwenye ofisi za mamlaka ya hifadhi  hiyo kwa nia ya kufanikisha hatua hiyo.


Aidha , Mhe. Kassim Majaliwa ameeleza kuwa, Rais Samia Suluhu Hassan amepongeza uamuzi wa wananchi hao na kwamba serikali itaendelea kuwekeza katika kuboresha miundombinu ya eneo la Msomera.


 “Napenda kumhakikishia Mheshimiwa Rais kwamba tulianza kuratibu, tunaendelea kuratibu na kuhakikisha wote walioamua kuhama wanapata faraja.”  amesema Waziri Mkuu


Amesema zoezi la kuratibu uhamaji wa hiari kuelekea Msomera limefanywa kwa utaratibu mzuri ikiwa ni pamoja na kuzingatia mazingira rafiki yaliyoko katika eneo la Msomera kwa binadamu na mifugo ambayo ni miundombinu ya barabara, umeme, maji, shule huduma za afya na huduma nyingine za kijamii ikiwemo uwezo wa umiliki wa ardhi, kilimo na malisho.


Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMAJKT kupitia kampuni yake ya ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited, ilipewa jukumu la kujenga nyumba 402 za kuhamia wakazi hao ambapo kampuni hiyo inaendelea na ujenzi huo kwa kasi na inatarajia kukabidhi nyumba hizo kwa serikali ifikapo Septemba 30, 2022.

Comments

Popular posts from this blog

UJUE MRADI WA UFUGAJI SAMAKI KWA KUTUMIA MATENKI- SUMAPONICS

 Katika video ni  mradi wa ufugaji wa samaki sato  unaojulikana kwa jina la SUMAPONICS uliopo  Mbweni JKT Dar es Salaam Tanzania.  Huu ni mradi mmojawapo kati ya miradi mingi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT). SUMAJKT Tv imetembelea mradi huo 11 March 2022 na kupata kuzungumza na Mkurugenzi Mwendeshaji wa mradi huo , na wengine kama inavyoonekana hapo. UFUGAJI SAMAKI WA MATENKI KWA KUZUNGUSHA MAJI (RE – CIRCULATION  AQUACULTURE SYSTEM – RAS) MBWENI JKT Ufugaji wa samaki kwa njia za mabwawa unahitaji rasilimali nyingi hasa ardhi, maji mengi na nguvu kazi kubwa ili kupelekea njia ya ufugaji samaki kwa matenki kwa kuzungusha maji (Recirculating Aquaculture System- RAS). RAS NI NINI? RAS ni mfumo wa kufuga samaki kwa kuzungusha maji ili kutoa uchafu pamoja na kuwaongezea hewa ya ziada samaki waliopo kwenye matenki. RAS ZA SUMAJKT Hizi ni RAS zinazotengenezwa katika mradi wa SUMAPONICS ambazo zina uwezo wa kutoa samaki wenye uzito...

KAMPUNI YA USAFI SUMAJKT CLEANING AND FUMIGATION YAPONGEZWA

Video hiyo ni Meneja wa kituo cha mabasi cha Mbezi Luis Bwana Mayira Mkama akipongeza Kampuni ya Usafi SUMAJKT Cleaning and Fumigation kwa huduma nzuri wanayotoa.  Katika mahojiano na SUMAJKT TV tarehe 09 April 2022 Meneja Mayira alisema  kuwa SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co. Limited wanatoa huduma nzuri kituoni hapo kutokana na kuwa na Watendaji wa kutosha pamoja na vitendea kazi vya kutosha tofauti na makampuni mengine ambapo mwanzoni huleta wafanyakazi wengi na baadae hupungua na eneo la kufanya usafi ni kubwa. Aidha ameeleza kuwa Uongozi wa Mbezi Luis Bus Terminal umekuwa ukishirikiana na kampuni hiyo katika kuhakikisha jukumu hilo linatimizwa ipasavyo. Meneja Mayira amezisihi kampuni zingine za usafi kuiga mfano kwa SUMAJKT. SUMAJKT Cleaning and Fumigation Company Limited ni kampuni tanzu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) iliyojizatiti katika utoaji wa huduma ya usafi na unyunyiziaji dawa.  Kampuni imejizatiti katika utoaji wa hudum...

“NAENDELEZA KAZI NINAZOZIJUA”- MEJA JENERALI MABELE

 Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT ) Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele tarehe 19/5/2022 ametimiza mwaka Mmoja madarakani huku akiendelea kutekeleza vema  azma ya Jeshi la Kujenga Taifa kujilisha pamoja na malezi ya vijana. Aidha tarehe 19 Mei 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alimteua kwa kipindi hicho akiwa  Brigedia Jenerali Rajabu Nduku Mabele kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afsa mtendaji mkuu wa SUMAJKT  Hatua iliyokuja kufuatia  aliyekuwa Mkuu wa Jeshi hilo, Meja Jenerali Charles Mbuge kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera akichukua nafasi ya Brig Jenerali Marco Elisha Gaguti aliyehamishiwa Mtwara. katika kipindi cha Mwaka mmoja akiwa madarakani Meja Jenerali Mabele ameendelea kutekeleza Majukumu yake kwa weledi ikiwa ni pamoja na kuliongoza vema Jeshi la Kujenga Taifa na Shirika lake la Uzalishaji Mali S...