Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe. Innocent Bashungwa amelipongeza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kwa kuendelea kutekeleza jukumu la malezi ya Vijana kupitia mafunzo yao ya Kujitolea na Mujibu wa Sheria yanayotolewa kwenye makambi ya JKT ili kuwajengea uzalendo pamoja na stadi za kazi na waweze kushiriki ujenzi wa Taifa. Mhe. Bashungwa amesema hayo alipofanya ziara ya kikazi iliyolenga kujitambulisha, Makao Mkuu ya JKT Chamwino, Jijini Dodoma ambapo alipata fursa ya kuongea na Maafisa, Askari, Vijana na Watumishi wa Umma wanaofanyia kazi JKT eneo la Dodoma. Mhe. Bashungwa ameongeza kuwa, Kukamilika kwa miradi ya Kilimo cha kimkakati katika shamba la SUMAJKT lililopo Mngeta na Ujenzi wa miundombinu ya Skimu ya Umwagiliaji iliyopo katika kikosi cha Chita JKT mkoani Morogoro, Italeta tija katika upatikanaji wa chakula cha kutosha na kulihakikishia Taifa Usalama wa Chakula pamoja na upatikanaji wa Mbegu bora. Ameongeza kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita imetenga bajeti ya fedha kupitia Wizara ya U
Comments
Post a Comment