Skip to main content

FANYIENI UTAFITI MAZAO YA NGANO NA ALIZETI - KANALI NGATA



 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, ametoa maagizo kwa Meneja wa shamba la SUMAJKT Bassotu Sajinitaji Bahati Kidenya, kufanya utafiti mzuri wa mazao ya ngano na alizeti ili shirika likiamua kuwekeza katika kilimo hicho kiwe na tija.

Kanali Petro Ngata, ametoa maagizo  hayo leo tarehe  12 Augosti 2022, alipokuwa katika ziara ya kukagua shamba hilo lililopo katika kijiji cha Bassotu , Wilaya ya Hanang'i Mkoani Manyara. 


Kanali Ngata ameongeza kuwa  Bassotu kuna faida kubwa endapo SUMAJKT itafanikiwa kupata eneo kubwa na kuanza na aina ya mazao mawili ambayo ni ngano na katamu (alizeti za miba).


"Ngano na katamu ni mazao ambayo tukizalisha tutakuwa na uhakika wa kupata faida" ameeleza Kanali Ngata. 


Aidha, Kanali Petro Ngata,  ameeleza kuwa shirika litaanza kuliwekea mipango mizuri na ya haraka shamba hilo, endapo msajili wa hazina atakubali kutoa eneo kwa SUMAJKT. 

   

Kwa upande wa Meneja wa mradi wa shamba la kilimo  cha alizeti SUMAJKT Bassotu Sajinitaji Bahati Kidenya, amesema kuwa mradi huo ulianzishwa  mwaka 2017 kwa ajili ya kuongeza mapato ya shirika na uchumi wa Taifa.


Sajinitaji Kidenya, ameongeza kuwa mradi wa shamba la SUMAJKT Bassotu , uliopo wilayani Hanang'i una jumla ya hekari 1000 kati ya hizo zinazofaa kwa kilimo kwa sasa ni hekari 500.


Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Petro Ngata, katika ziara hiyo pia alipitia katika Halmashauri ya mji wa Hanang'i, ambapo alipokelewa na  Katibu Tawala (DAS) Hanang'i Mhe. Paul Bura, ambapo ameeleza kuwa uwepo wa SUMAJKT katika kijiji cha Bassotu kumepunguza matukio ya uhalifu kwa kiasi kikubwa.


Mhe. Bura Ameongeza kuwa SUMAJKT na uongozi wa wilaya hiyo hapo awali kulikuwepo na makubaliano ya uanzishwaji wa kituo cha zana za kilimo pamoja na ujenzi wa kiwanda cha mafuta ya alizeti kwa sababu malighafi zinapatikana za kutosha.


SUMAJKT imekuwa ikijihusisha na uwekezaji wa aina mbali mbali ikiwemo kilimo.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

SUMAJKT YAKABIDHI VIATU VYA SHULE JOZI 500

 Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kupitia Kampuni tanzu iitwayo SUMAJKT shoes and leather Products Co LTD. tarehe 04 Novemba 2022 limekabidhi viatu vya ngozi jozi 500 kwa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao yenye kauli mbiu “Samia nivike viatu”. Aidha, makabidhiano ya viatu hivyo yamefanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam. Akielezea historia ya kiwanda Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Mathias John amesema, Kiwanda cha  viatu na bidhaa za ngozi SUMAJKT Shoes and Leather Product Co. LTD Kilianzishwa Jul 2017 na majukumu yake yakiwa ni uzalishaji wa viatu na bidhaa mbalimbali za ngozi.  Aidha, toka kuanzishwa Kqa  kiwanda hicho kimeendelea kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa kununua vifaa na mashine za kisasa ili kuzalisha bidhaa zenye ubora.  Bidhaa zinazozalishwa ni viatu kwa ajili ya taasisi za ulinzi, viatu vya usalama (safety boots), viatu vya maofisini na viatu vya shule.  Uwezo wa kiwanda ni kuzalisha viatu jozi 500 kwa siku na Kup

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA MIRADI YA UJENZI KANDA YA ZIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata leo tarehe 28 Oktoba 22 amefanya ziara katika miradi ya ujenzi inayoendelea kujengwa kanda ya ziwa. Kanali Petro Ngata amekagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Ziwa ambayo ni mradi wa ujenzi wa jengo la uchunguzi (Dignostic Center) katika hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama , Mradi wa uondoaji wa kifusi eneo la hanga uwanja wa ndege wa Chato Mkoani Geita na Mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Msalala. Aidha, Kanali Ngata  amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuhusu ukamilishwaji wa  jengo la ofisi za Halmashauri. SUMAJKT imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali ya ujenzi nchini kupitia kampuni yake ya ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited ambayo ina kanda saba za ujenzi.

MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA ZIARA MAFINGA MKOANI IRINGA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amehitimisha Ziara yake kwa kutembelea Kikosi cha JKT Mafinga Mkoani Iringa ambapo SUMAJKT katika kikosi hicho imewekeza katika ufugaji wa mifugo mbali mbali ikiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe. Bonyeza video hiyo kuona yaliyojiri.