Skip to main content

JKT KUENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO ZA UPATIKANAJI WA MAFUTA YA KULA NCHINI

 Mkurugezi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa( SUMAJKT), Kanali Petro Ngata amesema Jeshi la Kujenga Taifa litaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa mafuta ya kula hapa nchini.


Ameyasema hayo wakati alipotembelea Banda la JKT katika Maonesho ya Waku- lima,Wafugaji na Wavuvi (Nanenane) yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale, Uyole Jijini Mbeya.


Kanali Ngata amefafanua kuwa, JKT limeanza kutekeleza Kilimo cha Mazao ya Kimkakati ikiwemo zao la Alizeti kwa kutumia mashamba yake makubwa katika maeneo ambayo zao hilo linastawi.


"Tumeanza na Mkakati wa Kulima kwa wingi mazao ya kimkakati, na hatua inayofuata ni kuchakata zao hilo na kupata mafuta ya Kula". Amesema Kanali Ngata


Akizungumzia namna JKT mashamba darasa ya JKT yalivyo na Manufaa, Kanali Ngata amesema JKT lina wataalamu wa kutosha waliobobea katika kutoa elimu bora ya Uzalishaji wa Mazao ya kilimo, Mifugo na Uvuvi hivyo amewataka wakazi wa Mbeya na Mikoa ya Jirani kutembelea Banda la JKT.


Nae Mwenyekiti wa Maonesho ya Nanenane Kanali Shija Lupi amewataka 

wananchi kujitokeza kwa wingi kutembelea Banda la JKT kwa lengo la kupata elimu sambamba na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na JKT pamoja na Bidhaa zinazozalishwa na Viwanda na Makampuni Tanzu ya SUMAJKT.


Sambamba na hilo, Kanali Lupi amesema Maonesho ya mwaka huu yana kauli mbiu inayoendana na Ajenda ya Kitaifa ya Sensa ya watu na Makazi hivyo amewataka wananchi kujitokeza katika zoezi la sensa kwa maendeleo ya Taifa hili.


Akitoa ufafanua wa namna ya kufanya uvuvi wenye tija, Mkurugenzi wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Kanali Peter Lushika amesema uvuvi kwa njia ya mabwawa ni sahihi kwa Jiji la Mbeya kwa sababu samaki hawahitaji baridi kali, hivyo uvuvi jwa njia ya matanki unaweza kupelekea samaki wakafa.

Maonesho ya Wakulima (Nanenane) yanaadhimishwa kila tarehe 8 ya Mwezi Agosti kwa kila mwaka nchini, lengo likiwa kutoa Elimu kwa wakulima, Wafugaji na Wavuvi ya njia bora za Uzalishaji wenye Tija.

Jeshi la Kujenga Taifa, Linashiriki maonesho hayo Kitaifa na kikanda kwa lengo la kuwafikia wananchi wa Tanzania nchi nzima ambayo ni zaidi ya asilimia 80 wanaujihusisha na kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Comments

Popular posts from this blog

SUMAJKT YAKABIDHI VIATU VYA SHULE JOZI 500

 Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kupitia Kampuni tanzu iitwayo SUMAJKT shoes and leather Products Co LTD. tarehe 04 Novemba 2022 limekabidhi viatu vya ngozi jozi 500 kwa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao yenye kauli mbiu “Samia nivike viatu”. Aidha, makabidhiano ya viatu hivyo yamefanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam. Akielezea historia ya kiwanda Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Mathias John amesema, Kiwanda cha  viatu na bidhaa za ngozi SUMAJKT Shoes and Leather Product Co. LTD Kilianzishwa Jul 2017 na majukumu yake yakiwa ni uzalishaji wa viatu na bidhaa mbalimbali za ngozi.  Aidha, toka kuanzishwa Kqa  kiwanda hicho kimeendelea kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa kununua vifaa na mashine za kisasa ili kuzalisha bidhaa zenye ubora.  Bidhaa zinazozalishwa ni viatu kwa ajili ya taasisi za ulinzi, viatu vya usalama (safety boots), viatu vya maofisini na viatu vya shule.  Uwezo wa kiwanda ni kuzalisha viatu jozi 500 kwa siku na Kup

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA MIRADI YA UJENZI KANDA YA ZIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata leo tarehe 28 Oktoba 22 amefanya ziara katika miradi ya ujenzi inayoendelea kujengwa kanda ya ziwa. Kanali Petro Ngata amekagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Ziwa ambayo ni mradi wa ujenzi wa jengo la uchunguzi (Dignostic Center) katika hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama , Mradi wa uondoaji wa kifusi eneo la hanga uwanja wa ndege wa Chato Mkoani Geita na Mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Msalala. Aidha, Kanali Ngata  amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuhusu ukamilishwaji wa  jengo la ofisi za Halmashauri. SUMAJKT imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali ya ujenzi nchini kupitia kampuni yake ya ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited ambayo ina kanda saba za ujenzi.

MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA ZIARA MAFINGA MKOANI IRINGA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amehitimisha Ziara yake kwa kutembelea Kikosi cha JKT Mafinga Mkoani Iringa ambapo SUMAJKT katika kikosi hicho imewekeza katika ufugaji wa mifugo mbali mbali ikiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe. Bonyeza video hiyo kuona yaliyojiri.