Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linawaita vijana waliohitimu elimu ya Sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2022 kutoka shule zote za Tanzania bara kuhudhuria Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria. Sanjari na wito huo, JKT limewapangia makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 03 hadi June 2022. Vijana walioitwa wamepangwa katika kambi za JKT Rwamkoma-Mara, JKT Msange-Tabora, JKT Ruvu-Pwani, JKT Mpwapwa na Makutupora JKT-Dodoma, JKT Mafinga-Iringa, JKT Mlale-Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba-Tanga, JKT Makuyuni-Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila -Kigoma, JKT Itaka-Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa -Rukwa, JKT Nachingwea-Lindi na JKT Kibiti-Pwani na Oljoro JKT-Arusha. Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (Physical disabilities) waripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo. JKT inawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo. 1. Bukta ya