MKUU WA JKT NA AFISA MTENDAJI MKUU WA SUMAJKT MEJA JENERALI RAJAB NDUKU MABELE AMPONGEZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMIRI JESHI MKUU MHE. SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUTIMIZA MWAKA MMOJA MADARAKANI
SUMAJKT NI KITUO CHA BIDHAA NA HUDUMA BORA “Kazi iendelee” ni Kauli mbiu ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan alianza nayo tangu aapishwe kushika madaraka hayo ambayo kwasasa ametimiza mwaka mmoja. Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) halikubaki nyuma katika kuunga mkono kauli mbiu hiyo kwa vitendo, limekuwa sambamba na Serikali ya awamu ya sita kuhakikisha kazi zinaendelea kwa manufaa ya Shirika, JKT na Taifa kwa Ujumla. Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele ametoa pongezi zake za dhati kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kutimiza mwaka mmoja wa uongozi, Aidha amemshukuru kwa kuendelea kuliamini SUMAJKT na kulipatia kazi mbalimbali, kupitia kampuni ya ujenzi (SUMAJKT Construction Company Ltd) ikiwemo Mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dodoma, Mradi wa ujenzi wa ofisi za mtandao wa Ser