Kaimu Kamanda Kikosi Mgulani JKT Meja Heri Mwakalebe amewahasa wanafunzi wa kidato cha kwanza na waliohamia shule hiyo kuepusha na makundi yasiyofaa ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao. Meja Mwakalebe ameyasema hayo leo tarehe 4 Machi 2022, akiwa Mgeni Rasmi katika ufungaji wa mafunzo ya ukakamavu na uzalendo kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza na wanafunzi waliohamia katika Shule ya Sekondari ya Jitegemee jijini Dar es Salaam. "Wanafunzi acheni kujihusisha na makundi yasiofaa ili kujiepusha kuingia katika vishawishi vya matumizi mabaya ya dawa za kulevya na tabia nyingine zisizofaa" alisema Meja Mwakalebe. Meja Mwakalebe amewataka wanafunzi hao kutumia muda wao kusoma ili kutimiza ndoto za maisha yao kwa kupata elimu bora ili kupambana na adui ujinga ambaye ni chanzo cha maradhi na umaskini. Vilevile, amewahimiza wanafunzi wa kike kujiepusha na vishawishi mbalimbali badala yake wajifunze kutoka kwa wanawake waliofanikiwa na kufanya vizuri kwa kuwa viongozi katika T