Skip to main content

SUMAJKT YAKABIDHI VIATU VYA SHULE JOZI 500



 Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kupitia Kampuni tanzu iitwayo SUMAJKT shoes and leather Products Co LTD. tarehe 04 Novemba 2022 limekabidhi viatu vya ngozi jozi 500 kwa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao yenye kauli mbiu “Samia nivike viatu”.

Aidha, makabidhiano ya viatu hivyo yamefanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam.

Akielezea historia ya kiwanda Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Mathias John amesema, Kiwanda cha  viatu na bidhaa za ngozi SUMAJKT Shoes and Leather Product Co. LTD Kilianzishwa Jul 2017 na majukumu yake yakiwa ni uzalishaji wa viatu na bidhaa mbalimbali za ngozi. 

Aidha, toka kuanzishwa Kqa  kiwanda hicho kimeendelea kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa kununua vifaa na mashine za kisasa ili kuzalisha bidhaa zenye ubora. 

Bidhaa zinazozalishwa ni viatu kwa ajili ya taasisi za ulinzi, viatu vya usalama (safety boots), viatu vya maofisini na viatu vya shule. 

Uwezo wa kiwanda ni kuzalisha viatu jozi 500 kwa siku na Kupitia uzalishaji wa bidhaa hizo kiwanda kimeweza kuzalisha viatu kwa ajili ya watoto wa kitanzania walio shule za msingi kupitia Kampeni ya Mama ongea na mwanao 2021 yenye kauli mbiu Samia nivishe viatu. 

Aidha, Mkurugenzi  Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Mathias John mara baada ya historia hiyo fupi,  amekabidhi jozi 500 za viatu kwa   kamati inayosimamia kampeni hiyo kwa ajili ya kuwavisha wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi. 

“Nichukue fursa hii kuwakaribisha SUMAJKT kwani ni kituo cha huduma na bidhaa bora, 

SUMAJKT Shoes and Leather Product Company Limited, Tunakabidhi viatu hivi kwa taasisi ya mama ongea na mwanao na  lengo ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi hii.


 SUMAJKT tukiwa sehemu ya wazazi na walezi kwa watoto, tumeona jambo hili lililobebwa na taasisi hii ni jema na ni la jamii nzima na tumeguswa kuwainua watoto hasa wa vijijini  ili wasome kwa utulivu .

Tunaipongeza  Taasisi hii ya mama ongea na mwanao kwa kuleta tabasamu kwa watoto wa kusini na kuitakia kampeni hii mafanikio makubwa. ” alisema Maj John

Nae Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama ongea na mwanao ndg. Steven Nyerere kwa niaba ya kamati hiyo alishukuru SUMAJKT kuunga mkono kampeni yao yenye nia ya kuwavisha viatu watoto vijijini.

“Tunaishukuru SUMAJKT kwa kuunga mkono jambo letu na leo tunaweka bondi na Shirika hili . Viatu hivi hatuendi kuwakabidhi wakuu wa shule, tutawavalisha watoto sisi wenyewe na tunawakaribisha wadau mbali mbali kutuunga mkono na itapendeza kama viatu vikinunuliwa katika kiwanda cha SUMAJKT kwa sababu ni viatu vya kudumu ambavyo mtoto anaweza kuvaa hadi miaka miwili “ alisema.


Kiwanda cha viatu na bidhaa za ngozi SUMAJKT kimekuwa kikitengeneza viatu na bidhaa za ngozi halisi vya aina mbali mbali kwa matumizi ya watu wa rika tofauti.



Comments

Popular posts from this blog

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA MIRADI YA UJENZI KANDA YA ZIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata leo tarehe 28 Oktoba 22 amefanya ziara katika miradi ya ujenzi inayoendelea kujengwa kanda ya ziwa. Kanali Petro Ngata amekagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Ziwa ambayo ni mradi wa ujenzi wa jengo la uchunguzi (Dignostic Center) katika hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama , Mradi wa uondoaji wa kifusi eneo la hanga uwanja wa ndege wa Chato Mkoani Geita na Mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Msalala. Aidha, Kanali Ngata  amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuhusu ukamilishwaji wa  jengo la ofisi za Halmashauri. SUMAJKT imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali ya ujenzi nchini kupitia kampuni yake ya ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited ambayo ina kanda saba za ujenzi.

MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA ZIARA MAFINGA MKOANI IRINGA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amehitimisha Ziara yake kwa kutembelea Kikosi cha JKT Mafinga Mkoani Iringa ambapo SUMAJKT katika kikosi hicho imewekeza katika ufugaji wa mifugo mbali mbali ikiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe. Bonyeza video hiyo kuona yaliyojiri.