Skip to main content

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA MIRADI YA UJENZI KANDA YA ZIWA

 


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata ameendelea na ziara katika miradi mbali mbali ya ujenzi inayoendelea kujengwa na Kampuni ya ujenzi “SUMAJKT Construction Company Limited kupitia SUMAJKT Ujenzi kanda ya ziwa.

Kanali Petro Ngata katika ziara hiyo iliyoanza tarehe 28 hadi 30 Oktoba 2022 amekagua miradi mingine 

inayotekelezwa na SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Ziwa ambayo ni mradi wa Ujenzi wa hanga la Askari, Jengo la kuhifadhia maiti "Mortuary" na Jengo la wodi ya Wagonjwa Maalumu "VIP Ward" katika Hospitali ya Kijeshi Ilemela- Mwanza, 
 ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Kanda ya Ziwa lililopo Busweli-Ilemela Jijini Mwanza na kuagiza SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Ziwa iongeze kasi ya ujenzi ili ikamilishe mradi huo kwa wakati.

Aidha Kanali Petro Ngata amepongeza maendeleo ya utekelezaji wa Miradi hiyo na kuagiza SUMAJKT Ujenzi Kanda ya ziwa kukamilisha Ujenzi wa hanga  la Askari pamoja na chumba cha kuhifadhia maiti ndani ya wiki mbili kuanzia tarehe 30 Oct 22 na pia kukamilisha  Ujenzi wa "VIP Ward" ifikapo mwishoni mwa mwezi Dec 22.


SUMAJKT imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali ya ujenzi kote nchini kupitia kampuni yake ya ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited ambayo nayo imekuwa ikitekeleza miradi hiyo kupitia kanda ya karibu na eneo la mradi husika. 

SUMAJKT Construction Company Limited ina kanda saba za ujenzi ambazo ni SUMAJKT Ujenzi Makao Makuu, SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Kati, SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Mashariki, SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Magharibi, SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Kaskazini, SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Nyanda za juu Kusini na SUMAJKT Ujenzi Kanda ya ziwa.






Comments

Popular posts from this blog

SUMAJKT YAKABIDHI VIATU VYA SHULE JOZI 500

 Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kupitia Kampuni tanzu iitwayo SUMAJKT shoes and leather Products Co LTD. tarehe 04 Novemba 2022 limekabidhi viatu vya ngozi jozi 500 kwa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao yenye kauli mbiu “Samia nivike viatu”. Aidha, makabidhiano ya viatu hivyo yamefanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam. Akielezea historia ya kiwanda Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Mathias John amesema, Kiwanda cha  viatu na bidhaa za ngozi SUMAJKT Shoes and Leather Product Co. LTD Kilianzishwa Jul 2017 na majukumu yake yakiwa ni uzalishaji wa viatu na bidhaa mbalimbali za ngozi.  Aidha, toka kuanzishwa Kqa  kiwanda hicho kimeendelea kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa kununua vifaa na mashine za kisasa ili kuzalisha bidhaa zenye ubora.  Bidhaa zinazozalishwa ni viatu kwa ajili ya taasisi za ulinzi, viatu vya usalama (safety boots), viatu vya maofisini na viatu vya shule.  Uwezo wa kiwanda ni kuzalisha viatu jozi 500 kwa siku na Kup

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA MIRADI YA UJENZI KANDA YA ZIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata leo tarehe 28 Oktoba 22 amefanya ziara katika miradi ya ujenzi inayoendelea kujengwa kanda ya ziwa. Kanali Petro Ngata amekagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Ziwa ambayo ni mradi wa ujenzi wa jengo la uchunguzi (Dignostic Center) katika hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama , Mradi wa uondoaji wa kifusi eneo la hanga uwanja wa ndege wa Chato Mkoani Geita na Mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Msalala. Aidha, Kanali Ngata  amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuhusu ukamilishwaji wa  jengo la ofisi za Halmashauri. SUMAJKT imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali ya ujenzi nchini kupitia kampuni yake ya ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited ambayo ina kanda saba za ujenzi.

MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA ZIARA MAFINGA MKOANI IRINGA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amehitimisha Ziara yake kwa kutembelea Kikosi cha JKT Mafinga Mkoani Iringa ambapo SUMAJKT katika kikosi hicho imewekeza katika ufugaji wa mifugo mbali mbali ikiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe. Bonyeza video hiyo kuona yaliyojiri.