Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalisahaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, ametoa maagizo ya kukamilishwa kwa wakati miradi ya ujenzi inayojengwa na Mkandarasi SUMAJKT Construction Co. Ltd Kanda ya Ziwa.
Kanali Petro Ngata akiendelea na ziara katika miradi ya ujenzi kanda ya ziwa, ametembelea Ujenzi wa majengo ya OPD, RCH, Pharmacy na Mortuary yaliyopo katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza.
Aidha Kanali Ngata ameagiza kasi ya ujenzi iongezwe na ifanyike kwa njia ya oparesheni ambapo majengo ya "Pharmacy" na "Mortuary" yawe yamekamilika ifikapo tarehe 30 Nov 22 na "OPD" na "RCH" yakamilike ifikapo tarehe 12 Dec 22.
Vile vile Kanali Ngata amepata wasaa wa kutembelea Jengo la Halmashauri ya Bunda na kuagiza Meneja Ujenzi Kanda ya Ziwa kumuandikia Mshauri wa Mradi changamoto zote zinazosababisha ucheleweshaji wa mradi huu unaotekelezwa kwa njia ya "Force Account" ili uweze kukamilika kwa wakati uliopangwa.
Kadhalika Kanali Petro Ngata ametembelea Mradi wa ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, linalojengwa Bariadi mkoani Simiyu. Mradi huu umefikia asilimia 59 kwa ujumla wake na asilimia 90 kwa mujibu wa mkataba wa awamu ya kwanza utakaoishia kwenye uwezekaji wa paa na ameagiza mradi huu umalizike tarehe 30 Nov 22 kama ilivyopangwa.
Pia Kanali Ngata ametembelea Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Mkoa wa Simiyu ambapo ameagiza majukumu yote yanayotekelewa na Kampuni ya Ujenzi ya SUMAJKT Kanda ya Ziwa yawe yamekamilika ifikapo tarehe 31 Dec 22 kulingana na mkataba.
Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT Kanali Petro Ngata, amekuwa akitembelea miradi mbali mbali ya Shirika kutaka kujua maendeleo ya miradi hiyo na kutoa maelekezo ya kiutendaji yanayochangia miradi hiyo kukamilika kwa ubora na kwa wakati.
Comments
Post a Comment