Ujumbe wa Maafisa kutoka Chuo cha Ukamanda na Unadhimu nchini Zambia ukiongozwa na Brigedia Jenerali Humphery Nyone leo tarehe 03 Oktoba 2022 umetembelea Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Makao Makuu Mlalakuwa jijini Dar es salaam ili kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na SUMAJKT.
Ujumbe huo idadi ya Maafisa 20 umepokelewa na Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Shija Lupi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Petro Elikana Ngata.
Akizungumza mara baada ya kupokea Ugeni huo Kanali Shija Lupi amesema kuwa Zambia na Tanzania zimeendeleza Udugu katika Shughuli mbalimbali za Kibiashara.
"nchi hizi mbili zimekua kiuchumi, mara baada ya kupata uhuru katika miaka ya 1960, na Zambia kwa mara kadhaa imekua ikiagiza bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania, ikiwemo vifaa vya ujenzi pamoja na mazao ya vyakula, lakini pia Zambia imekua mzalishaji mkubwa wa bidhaa za kilimo, kama mahindi, bidhaa za shaba na nyingine nyingi"
Aidha Kanali Lupi amesema kuwa katika miundombinu bidhaa nyingi zimekua zikisafirishwa kupitia bandari ya Dar es aaalam hadi Ndola zaidi ya tani milioni 1, mafuta kupitia Bomba la TAZAMA huku nyingine zikisafirishwa kupitia reli ya TAZARA" alisema Kanali Lupi
Kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajab Mabele nikushukuru wewe pamoja na ujumbe uliombatana nao, kwa kuendelea kudumisha Udugu huu.
Naye, Meja Athman Levery kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Utafiti Luteni Kanali George Wang'ombe ameelezea chimbuko la Shirika pamoja na shughuli mbalimbali zinazofanywa kupitia sekta zake nne ambazo ni Ujenzi, uhandisi na ushauri, sekta ya kilimo ufugaji na uvuvi,
sekta ya huduma na biadhara pamoja na sekta ya viwanda.
Akielezea sekta ya viwanda amesema kuwa shirika linaboresha viwanda vilivyopo na kuanzisha viwanda vipya.
“Viwanda vilivyopo ni kiwanda cha cha Ushonaji
b. Kiwanda cha Samani, Kiwanda cha Maji ya Kunywa, Kiwanda cha taa, kiwanda cha mabati na misumari, pamoja na kiwanda cha nafaka” alisema Meja Levery
Aidha Brigedia Jenerali Humphery Nyone alishukuru kwa mapokezi mazuri waliyoyapata Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa jijini Dar es salaam.
Vilevile Brigedia Jenerali Nyone alifurahishwa na shughuli mbalimbali za Uzalishaji Mali zinazofanywa na SUMAJKT ikiwemo Kampuni ya ujenzi, Kilimo, Viwanda pamoja na Ufugaji na kuahidi kuendelea kujifunza kupitia SUMAJKT.
" Tulipokua tunakuja Tz tumeangalia wapi tumetoka Kuanzia kwa baba zetu Keneth Kaunda na Mwl. Nyerere, Ushirikiano wetu kijeshi una historia, wazo la kuwa na shirika tumelipata hapa na tumeona mnafanya vizuri sana, kuanzia biashara za aina tofauti na hivyo tunatarajia kuiga mnachokifanya ninyi.
Tunatarajia pia kushirikiana kwa mambo mengi ndio maana kama chuo tumekuja kujifunza hapa, pia tunatamani urafiki huu endelee kukua kila uchwao kwani tunategemeana kiuchumi kupitia reli ya TAZARA.
Endeleeni kufanya mnayofanya tunazisifu kazi zenu na kila mnachofanya tunaenda kukifanya”
alisema Brigedia Jenerali Nyone .
SUMAJKT imekuwa ikipokea ujumbe kutoka nchi mbali mbali wanaofika kuona shughuli za uzalishaji Mali zinavyoendeshwa na Shirika hilo.
Comments
Post a Comment