Skip to main content

MAISHA NI MAPAMBANO - Meja Misigaro

 



NAIBU Kamanda Kikosi cha Mgulani JKT, Meja Eusebius Misigaro amewakumbusha Wanafunzi wahitimu wa mafunzo ya Ukakamavu na Uzalendo katika shule ya Sekondari ya Jitegemee kuwa Maisha ni mapambano ambayo yanahitaji maandalizi mazuri na njia sahihi ya kujiandaa kupata Elimu, maarifa, fikra na ujuzi sahihi.

Meja Misigaro ameyasema hayo leo tarehe 21 Oktoba 2022 alipokuwa akifunga mafunzo ya Ukakamavu na Uzalendo kwa Wanafunzi wa kidato cha tano kwa mwaka 2022/2023 na wahamiaji wa kidato cha kwanza na kidato cha tatu.

Mafunzo ya Ukakamavu na Uzalendo wanayopatiwa wanafunzi wanaoanza Shule katika shule ya Sekondari Jitegemee yana dhima Kuu ambayo ni kumjenga Mwanafunzi na kimaadili ili elimu anayopata iweze kumsaidia kikamilifu katika kupambana na changamoto mbalimbali za maisha ya kila siku sambamba na mwanafunzi kuwa na nidhamu na maadili mema, kwani nidhamu ni msingi wa mafanikio katika maisha. 

Elimu ya darasani ni vema iende sambamba na kupandikiza chembechembe za nidhamu Kwa mwanafunzi, matokeo yake ni mwanafunzi kuwa Mtu bora katika maisha.

Aidha, Meja Misigaro, ametoa rai kwa wahitimu hao kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kama Facebook,Twitter, Whatsapp, Youtube na Instagram kwa ajili ya kujifunza mambo maovu.



Awali akitoa taarifa ya mafunzo hayo Kaimu Mkuu wa Shule Utawala, Meja Dickson Chao amesema mafunzo hayo ya Ukakamavu na Uzalendo yamechukua muda wa majuma mawili ambapo wanafunzi 105 wamehitimu ambapo kati yao wavulana idadi ni 63 na wasichana idadi ni 42.


Wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo Wanafunzi waliohitimu walipita mbele ya mgeni rasmi kwa mwendo wa Pole na mwendo wa Haraka na kisha mgeni rasmi kutoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri.


Mafunzo haya ya Ukakamavu na Uzalendo hufanywa kwa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, kidato tano na wanafunzi wanaohamia shuleni hapo kutoka  shule nyingine kabla ya kuanza kwa muhula wa masomo ambapo mafunzo hayo ni kama Jando na Unyago, Ili wanafunzi waweze kuendana na mila, kanuni na desturi za shule ya Sekondari Jitegemee.


SUMAJKT inamiliki shule za mbili za sekondari ambazo ni Jitegemee Dar es Salaam na Kawawa iliyopo Mafinga mkoani Iringa.

Comments

Popular posts from this blog

SUMAJKT YAKABIDHI VIATU VYA SHULE JOZI 500

 Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kupitia Kampuni tanzu iitwayo SUMAJKT shoes and leather Products Co LTD. tarehe 04 Novemba 2022 limekabidhi viatu vya ngozi jozi 500 kwa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao yenye kauli mbiu “Samia nivike viatu”. Aidha, makabidhiano ya viatu hivyo yamefanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam. Akielezea historia ya kiwanda Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Mathias John amesema, Kiwanda cha  viatu na bidhaa za ngozi SUMAJKT Shoes and Leather Product Co. LTD Kilianzishwa Jul 2017 na majukumu yake yakiwa ni uzalishaji wa viatu na bidhaa mbalimbali za ngozi.  Aidha, toka kuanzishwa Kqa  kiwanda hicho kimeendelea kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa kununua vifaa na mashine za kisasa ili kuzalisha bidhaa zenye ubora.  Bidhaa zinazozalishwa ni viatu kwa ajili ya taasisi za ulinzi, viatu vya usalama (safety boots), viatu vya maofisini na viatu vya shule.  Uwezo wa kiwanda ni kuzalisha viatu jozi 500 kwa siku na Kup

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA MIRADI YA UJENZI KANDA YA ZIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata leo tarehe 28 Oktoba 22 amefanya ziara katika miradi ya ujenzi inayoendelea kujengwa kanda ya ziwa. Kanali Petro Ngata amekagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Ziwa ambayo ni mradi wa ujenzi wa jengo la uchunguzi (Dignostic Center) katika hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama , Mradi wa uondoaji wa kifusi eneo la hanga uwanja wa ndege wa Chato Mkoani Geita na Mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Msalala. Aidha, Kanali Ngata  amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuhusu ukamilishwaji wa  jengo la ofisi za Halmashauri. SUMAJKT imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali ya ujenzi nchini kupitia kampuni yake ya ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited ambayo ina kanda saba za ujenzi.

MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA ZIARA MAFINGA MKOANI IRINGA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amehitimisha Ziara yake kwa kutembelea Kikosi cha JKT Mafinga Mkoani Iringa ambapo SUMAJKT katika kikosi hicho imewekeza katika ufugaji wa mifugo mbali mbali ikiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe. Bonyeza video hiyo kuona yaliyojiri.