Skip to main content

Posts

KAMPUNI YA USAFI SUMAJKT CLEANING AND FUMIGATION YAPONGEZWA

Video hiyo ni Meneja wa kituo cha mabasi cha Mbezi Luis Bwana Mayira Mkama akipongeza Kampuni ya Usafi SUMAJKT Cleaning and Fumigation kwa huduma nzuri wanayotoa.  Katika mahojiano na SUMAJKT TV tarehe 09 April 2022 Meneja Mayira alisema  kuwa SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co. Limited wanatoa huduma nzuri kituoni hapo kutokana na kuwa na Watendaji wa kutosha pamoja na vitendea kazi vya kutosha tofauti na makampuni mengine ambapo mwanzoni huleta wafanyakazi wengi na baadae hupungua na eneo la kufanya usafi ni kubwa. Aidha ameeleza kuwa Uongozi wa Mbezi Luis Bus Terminal umekuwa ukishirikiana na kampuni hiyo katika kuhakikisha jukumu hilo linatimizwa ipasavyo. Meneja Mayira amezisihi kampuni zingine za usafi kuiga mfano kwa SUMAJKT. SUMAJKT Cleaning and Fumigation Company Limited ni kampuni tanzu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) iliyojizatiti katika utoaji wa huduma ya usafi na unyunyiziaji dawa.  Kampuni imejizatiti katika utoaji wa hudum...

HII NDIO SIRI YA MAFANIKIO YA KIWANDA CHA USHONAJI NGUO SUMAJKT GARMENTS COMPANY LIMITED

Katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali kupitia mageuzi ya viwanda Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) halikubaki nyuma katika sekta ya viwanda. Miongoni mwa viwanda vilivyoanzishwa mwaka 2017 SUMAJKT Garments ni kiwanda kimojawapo ambacho kinafanya vizuri katika soko la ushindani na kimekuwa kimbilio la jamii kutokana na umahiri katika kazi ya ushoni. SUMAJKT Garments Company Limited inafanya vizuri katika shughuli za ushonaji nguo na Kupitia Video hiyo utapata kujua shughuli zote za ushonaji nguo sambamba na kudarizi  vinavyofanyika  kiwandani hapo.  Mnamo tarehe 2/02/2022 Kamera za SUMAJKT TV zilifika kiwandani hapo kufuatilia mchakato mzima wa ushonaji nguo na kupitia video hiyo hayo ndio yaliyojiri. Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Sylvester Ntandu pamoja na Maafisa wasaidizi wake wanakuelezea utendaji kazi wa kiwanda hicho. SUMAJKT Garments Company Limited kinashona mavazi ya aina mbali mbali zikiwemo nguo za watu b...

MKUU WA JKT NA AFISA MTENDAJI MKUU WA SUMAJKT MEJA JENERALI RAJAB NDUKU MABELE AMPONGEZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMIRI JESHI MKUU MHE. SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUTIMIZA MWAKA MMOJA MADARAKANI

 SUMAJKT NI KITUO CHA BIDHAA NA HUDUMA BORA “Kazi iendelee” ni Kauli mbiu ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan alianza nayo tangu aapishwe kushika madaraka hayo ambayo kwasasa ametimiza mwaka mmoja. Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) halikubaki nyuma katika kuunga mkono kauli mbiu hiyo kwa vitendo, limekuwa sambamba na Serikali ya awamu ya sita kuhakikisha kazi zinaendelea kwa manufaa ya Shirika, JKT na Taifa kwa Ujumla. Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele ametoa pongezi zake za dhati kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kutimiza mwaka mmoja wa uongozi, Aidha amemshukuru kwa kuendelea kuliamini SUMAJKT na kulipatia kazi mbalimbali, kupitia kampuni ya ujenzi (SUMAJKT Construction Company Ltd) ikiwemo Mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dodoma, Mradi wa ujenzi wa ofisi za mtandao wa...

KAMANDA JKT ZAMBIA ATEMBELEA VIWANDA SUMAJKT

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Tanzania Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele apongezwa na Mkuu wa JKT Zambia kwa kupiga hatua katika kusimamia  uzalishajimali . Kamanda wa Jeshi la Kujenga Taifa Zambia Luteni Jenerali Maliti Solochi tarehe 15 Machi 2022 ametembelea Kiwanda cha maji SUMAJKT Bottling Company pamoja na kiwanda cha ushonaji nguo SUMAJKT Garments Company katika eneo la Mgulani JKT Dar es Salaam kuona uzalishajimali na ametoa pongezi kwa namna Shirika linavyoendeshwa na kupiga hatua chini ya Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajab Nduku Mabele. Jenerali Solochi amesema kuwa JKT Zambia limekopi kila kitu kutoka JKT Tanzania ikiwemo uanzishaji wa viwanda na kwasasa jeshi lao lina baadhi ya viwanda ikiwemo kiwanda cha maji na kiwanda cha viatu. Jenerali Solochi ameongeza kuwa mahusiano haya ya kindugu kati ya JKT Tanzania na JKT Zambia yalianzishwa na Viongozi waasisi wake ambao ni baba wa taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Keneth...

UJUE MRADI WA UFUGAJI SAMAKI KWA KUTUMIA MATENKI- SUMAPONICS

 Katika video ni  mradi wa ufugaji wa samaki sato  unaojulikana kwa jina la SUMAPONICS uliopo  Mbweni JKT Dar es Salaam Tanzania.  Huu ni mradi mmojawapo kati ya miradi mingi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT). SUMAJKT Tv imetembelea mradi huo 11 March 2022 na kupata kuzungumza na Mkurugenzi Mwendeshaji wa mradi huo , na wengine kama inavyoonekana hapo. UFUGAJI SAMAKI WA MATENKI KWA KUZUNGUSHA MAJI (RE – CIRCULATION  AQUACULTURE SYSTEM – RAS) MBWENI JKT Ufugaji wa samaki kwa njia za mabwawa unahitaji rasilimali nyingi hasa ardhi, maji mengi na nguvu kazi kubwa ili kupelekea njia ya ufugaji samaki kwa matenki kwa kuzungusha maji (Recirculating Aquaculture System- RAS). RAS NI NINI? RAS ni mfumo wa kufuga samaki kwa kuzungusha maji ili kutoa uchafu pamoja na kuwaongezea hewa ya ziada samaki waliopo kwenye matenki. RAS ZA SUMAJKT Hizi ni RAS zinazotengenezwa katika mradi wa SUMAPONICS ambazo zina uwezo wa kutoa samaki wenye uzito...