Skip to main content

Posts

Showing posts from July, 2022

ZINGATIENI UBORA KATIKA MIRADI YA UJENZI-KANALI NGATA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amekagua Miradi tisa ya ujenzi jijini Dodoma inayojengwa na SUMAJKT Construction Company Ltd, kupitia Kanda mbali mbali. Kanali Petro Ngata, amefanya ziara hiyo jana tarehe 22 Julai 2022 alipotembelea  miradi mbali mbali ya ujenzi katika mji wa serikali Mtumba , Shule ya Mfano Iyumbu pamoja ukaguzi wa mitambo katika kiwanda cha mabati SUMAJKT Roofing Company Limited kilichopo Dodoma. Pia amekagua maendeleo ya Ujenzi wa jengo la wizara ya Katiba na Sheria, unaotekelezwa na SUMAJKT Construction Company Limited Ujenzi kanda ya Mashariki,    Pia amekagua Ujenzi wa jengo la Mwanasheria Mkuu wa Serikali unaotekelezwa na  SUMAJKT ujenzi Kanda ya Kati Dodoma, Ujenzi wa Jengo la Wakili Mkuu wa Serikali  unaotekelezwa na SUMAJKT  Makao Makuu, Ujenzi wa Jengo la Wakala wa Mtandao wa Serikali, Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya waziri mkuu, jengo la  Sera,  Ujen...