Skip to main content

MHE. RAIS SAMIA SULUHU AMPONGEZA MKUU WA JKT




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan amempongeza Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa kukamilisha ujenzi wa Mradi wa Chuo cha Ualimu Kabanga . 

Mhe. Rais Samia Suluhu amesema hayo tarehe 17 Oktoba 2022 katika ufunguzi wa majengo ya chuo hicho kilichopo katika wilaya ya Kasulu, Mkoa wa Kigoma alipokuwa akizindua Mradi huo


Aidha mradi huo uliofadhiliwa na Serikali ya Canada Ulianza tarehe 26 Machi 2019 ambapo ulitekelezwa na Kampuni ya Ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited na kukabidhiwa rasmi kwa Wizara ya Elimu baada ya kukamilika tarehe 21 Apri 2022 kupitia Kanda ya ujenzi ya Kusini inayosimamiwa na Kanali Mbaraka Magogo ambaye ni Mkuu wa Ujenzi Kanda ya Magharibi.


Thamani ya mradi huo ni TShs 12.1 billion zikiwa ni gharama za mkandarasi na una jumla ya majengo 13 ambayo ni mabweni 2, jengo la utawala, jengo la madarasa lenye madarasa 10, Bwalo,  Ukumbi wa mikutano , jengo la maabara, ukumbi wa mihadhara, jengo la maktaba, zahanati na nyumba 4 za watumishi na  yote yakiwa ndani ya Uzio.

Pia mradi huo una miundombinu ya Biogas, Tehama, Umeme na Maji.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele ametoa kompyuta mbili kama mchango kwenye maabara ya chuo hicho ambazo amezikabidhi kwa Katibu Mkuu Elimu siku ya uzinduzi.


Mradi huo upo katika Kipindi cha uangalizi cha mwaka mmoja kuanzia tarehe 21 Aprili 2022 ambacho kitakamilika tarehe 20 Aprili 2023.



Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa Limekuwa likikamilisha ujenzi wa miradi mbali mbali kupitia Kampuni yake ya Ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited yenye kanda saba za ujenzi ambazo ni SUMAJKT Ujenzi Makao Makuu, SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Kati, SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Mashariki, SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Magharibi, SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Kaskazini, SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Nyanda za juu Kusini na SUMAJKT Ujenzi Kanda ya ziwa.

Comments

Popular posts from this blog

SUMAJKT YAKABIDHI VIATU VYA SHULE JOZI 500

 Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kupitia Kampuni tanzu iitwayo SUMAJKT shoes and leather Products Co LTD. tarehe 04 Novemba 2022 limekabidhi viatu vya ngozi jozi 500 kwa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao yenye kauli mbiu “Samia nivike viatu”. Aidha, makabidhiano ya viatu hivyo yamefanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam. Akielezea historia ya kiwanda Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda hicho Meja Mathias John amesema, Kiwanda cha  viatu na bidhaa za ngozi SUMAJKT Shoes and Leather Product Co. LTD Kilianzishwa Jul 2017 na majukumu yake yakiwa ni uzalishaji wa viatu na bidhaa mbalimbali za ngozi.  Aidha, toka kuanzishwa Kqa  kiwanda hicho kimeendelea kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa kununua vifaa na mashine za kisasa ili kuzalisha bidhaa zenye ubora.  Bidhaa zinazozalishwa ni viatu kwa ajili ya taasisi za ulinzi, viatu vya usalama (safety boots), viatu vya maofisini na viatu vya shule.  Uwezo wa kiwanda ni kuzalisha viatu jozi 500 kwa siku na Kup

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA MIRADI YA UJENZI KANDA YA ZIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata leo tarehe 28 Oktoba 22 amefanya ziara katika miradi ya ujenzi inayoendelea kujengwa kanda ya ziwa. Kanali Petro Ngata amekagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na SUMAJKT Ujenzi Kanda ya Ziwa ambayo ni mradi wa ujenzi wa jengo la uchunguzi (Dignostic Center) katika hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama , Mradi wa uondoaji wa kifusi eneo la hanga uwanja wa ndege wa Chato Mkoani Geita na Mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Msalala. Aidha, Kanali Ngata  amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuhusu ukamilishwaji wa  jengo la ofisi za Halmashauri. SUMAJKT imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali ya ujenzi nchini kupitia kampuni yake ya ujenzi SUMAJKT Construction Company Limited ambayo ina kanda saba za ujenzi.

MKURUGENZI MTENDAJI SUMAJKT KATIKA ZIARA MAFINGA MKOANI IRINGA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Kanali Petro Ngata, amehitimisha Ziara yake kwa kutembelea Kikosi cha JKT Mafinga Mkoani Iringa ambapo SUMAJKT katika kikosi hicho imewekeza katika ufugaji wa mifugo mbali mbali ikiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe. Bonyeza video hiyo kuona yaliyojiri.